Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Wednesday, October 1, 2014

Mila na desturi za Wairaqw kuondoa laana “loo” (Sehemu ya 1)

Makala hii imeandikwa na Mzee Lous S. Qorro ambaye amefanya utafiti na kuandika vizuri aliyoyabaini.

endelea...

Jamii nyingi za Kiafrika huamini kuwa laana inaweza kuipata jamii fulani au eneo fulani. Hali hiyo si tfauti pia katika jamii ya Wairaqw Mkoani Manyara. Mara inapodhihirika kwamba kuna laana, hufanyika utaratibu wa kuiondoa laana hiyo.

Laana hutokea pale mtu anapomkosea mwezake kosa kubwa ambapo yule aliyetendewa kosa hilo, hutamka kwa kulaani au pasipo kutamka lakini ananung’unika na hivyo yule aliyetenda kosa atapatwa na laana hiyo. Laana pia hutokea kama kundi la watu katika jamii litatenda jambo la fedheha, dhuluma au makosa ya kudhalilisha katika Eneo lao.

Katika makala hii tutazungumzia laana kati ya watu au pande mbili zilizokoseana. Imethibitika katika maisha ya jamii ya Wairaqw kwamba laana ipo na inafanya kazi na kwamba athari za laana kama ilivyotamkwa na yule aliyekosewa, imeonekana dhahiri.

Katika lugha ya Kiiraqw, neno laana ni “Loo” na lugha hiyo inatokana na neno “Loa”. Loa kwa tafsiri ya kawaida ni “jua hili lililopo angani” lakini pia loa inayotafsiri kubwa zaidi nayo ni “Mungu” loa ni kama jua lililoko angani, linaheshima kubwa katika mila na desturi za wairaqw, kwa kuwa inawakilisha uwepo wa Mungu, loa inapotafsiriwa kama Mungu inasifa zote za kimungu kama kuna sifa tunazoziona katika dini ya kikristo, Kiisilamu naya Kiyahudi.

Mtu anapotoa laana kwa kutamka au kwa kunung’unika kwa neno "loa" mtu huyu anatoa ombi lake kwa Mungu ili Mungu atoe adhabu kwa yule aliyemkosea. Mungu peke yake ndiye mwenye uwezo wa kutoa adhabu kwa mkosaji.

Inapothibitika kwamba mtu amelaaniwa hufanywa utaratibu wa kuondoa laana hiyo, yule aliyelaani hukutanishwa na yule aliyelaaniwa, na kama mmoja wao au wote wawili wamekwisha kufariki, hutafutwa wawakilishi wa uzao wao kwa jinsi inavyo kubalika na hapo hufanywa ibada ya kuondoa
laana. Kwa njia mbili njia moja ni kusomwa kwa misa takatifu na njia ya pili ni matambiko ya mila na desturi ya jamii husika.

Ibada hiyo inaelekezwa kwa loa (Mungu) wakiomba laana iliyoko iondolewe. Baada ya Ibada hiyo, wahusika hupeana mikono na kula chakula pamoja kwa kuwa kabla ya hapo walikuwa mahasimu. Kwa kitendo hicho, laana itakuwa imefutika na athari yake itakuwa haipo tena.

Ibada hiyo ni rahisi, inahusu pande mbili Mahasimu na aihitaji kiongozi wa mila au wa nchi. Kama atahitajika mtu wa tatu ni wakuelekeza tu wakati mwingine uwepo wa mashahidi pia haukuwa muhimu
lakini wanaoguswa zaidi na laana ni yule aliyelaaniwa na yule aliyelaani. Dhima ya kuondoa laana inaanza kwa mlaaniwa kisha mlaaniwa anapomwendea yule aliyelaani anaowajibu wakukubali sahihisho. Hakunakumbukumbu katika jamii ya Wairaqw kwamba upande uliotoa laana wamewahi kukataa laana isiondolewe.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda