Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Thursday, May 8, 2014

Gidamis Shahanga: Mwanariadha wa kwanza nchini picha yake kuwekwa kwenye "Stempu"


  • ·         Alizaliwa Katesh mwaka 1957
  • ·         Alitwaa medali ya dhahabu jumuiya ya madola 1978

Katika miaka ya 1970 na 1980, Tanzania ilijaliwa kuwa na hazina kubwa sana katika mchezo wa riadha ambapo wanariadha mbalimbali walikuwa waking'aa katika anga za michezo za kimataifa.

 Wakati Filbert Bayi alipojitambulisha katika ulimwengu wa riadha akiwa na miaka 17 tu, akiwa anatokea wilayani Karatu, kilometa kadhaa kusini magharibi mwa Karatu, lulu nyingine iliibuliwa na kuiletea nchi yetu sifa kem kem. Huyu si mwingine bali ni Gidamis Shahanga, ambaye aliiletea nchi yetu medali ya dhahabu katika michezo ya Jumuiya ya Madola yaliyofanyika katika jiji la Edmonton, Canada mwaka 1978.

Shahanga ambaye alizaliwa tarehe 4 Septemba 1957, Katesh wilayani Hanang, alikuwa mbobevu katika mbio za mita 10,000 na marathon na ndiye mwanariadha wa kwanza kabisa picha yake kutumika katika stempu za posta nchini mwaka 1980
Moja ya rekodi za kuvutia za Shahanga ni kuwa mwanariadha wa pekee nchini kutetea ubingwa wa Jumuiya ya Madola (back to back) baada ya kufanikiwa kutwaa tena medali ya dhahabu katika michuano hiyo iliyofanyia Brisbane nchini Australia mwaka 1982.
Baada ya kustaafu riadha, Shahanga aliingia katika siasa na kufanikiwa kuwa diwani katika halmashauri ya wilaya ya Hanang kwa muda wa miaka 15 na pia kuwa mwenyekiti wa halmashauri hiyo kwa muda wa miaka 10 hadi mwaka 2010 alipoamua kuachana na siasa.
Hata baada ya kustaafu riadha na kujihusisha na siasa, aliendelea kujihusisha na michezo hasa riadha na kufanikiwa kuwasaidia wanariadha mbalimbali chipukizi akiwemo Wilhelm Gidabuday na wengineo wengi. Kwa sasa Shahanga ni mwenyekiti wa chama cha wanamichezo waliowahi kushiriki Olimpiki nchini (TOA).
Ni vyema serikali na wadau wa michezo nchini kuwaenzi wachezaji wa zamani walioliletea Taifa letu heshima katika michezo mbali mbali hapa nchini kama Gidamis Shahanga.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda