Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Tuesday, January 29, 2013

Mtwara wameweza, hata kwetu inawezekana

Hatimaye serikali kwa mara ya kwanza katika Historia ya Nchi hii imesalimu amri kwa wananchi baada ya wananchi wa Mtwara kupinga kusafirisha Gesi ya Asili kutoka Mtwara na kupelekwa Dar es Salaam. Sitaki kuingia kwa undani na kuhukumu nani yupo sahihi au la, na suala la umuhimu wa kusafirisha gesi hiyo badala ya kujenga mitambo huko huko Mtwara badala ya jijini Dar es Salaam maana yawezekana Serikali ilikuwa na nia njema kabisa ya kusafirisha gesi hiyo ili iweze kutumika hata zaidi ya kuzalisha umeme, lakini hoja ya msingi hapa ni kuwa wananchi wamechoshwa kupelekeshwa na wameamua kuhakikisha rasilimali zao zinatumika kwa faida yao.
Moja ya Mabango ya wana Mtwara wanaopinga gesi kwenda Dar

Wananchi wa Mtwara wameonesha tofauti kubwa sana na Watanganyika tuliowazoea, waliweka itikadi za kidini na kisiasa pembeni na kuamua kusimamia rasilimali zao kwa faida yao huku wakijifunza kutoka kwa ndugu zao wa kanda ya ziwa ambao kuishi kwao karibu na migodi ya dhahabu badala ya kuwaletea neema kumekuwa kama laana, wameachiwa mashimo na madini ya zebaki.
Haya ndiyo maazimio yaliyofikiwa baina ya serikali na wenye nchi hao ambao sio jeshi la polisi (kupitia mabomu ya machozi na maji yanayowasha) na hata viongozi wa juu wamethubutu kuwatuliza.

  • Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Mstaafu Simbakalia kawaomba radhi wananchi wa Mtwara.
  • Waziri Nchimbi kutumia lugha kibabe na vitisho dhidi ya raia pamoja na taarifa isiyokuwa na tathmini halisi na yenye uwiano pale alipotolea mfano askari aliyevamiwa dukani/baa yake na kuibiwa pesa kiasi cha sh. 1,895,000/= na kupoteza mali ya sh. 200,000,000/= (milioni mia mbili) na kusababisha watu wagune.
  • Kawambwa kawahimiza wazazi kuwaruhusu watoto kwenda shule kupata elimu sanjari na chuo cha VETA kutoa masomo ya mitaala ya gesi sanjari na uchomeleaji baharini.
  • Tibaijuka amezungumzia kuhusu upanuzi wa mji wa Mtwara na kuleata kauli mbiu ya "Amani na Maendeleo" kutoka kwao Kagera.
  • Mwakyembe amezungumzia upanuzi wa bandari kavu na ujenzi wa reli Mtwara, Liganga, Mchuchuma hadi Mbamba Bay na kuahidi kuja Mtwara kila baada ya miezi 3 na kujadili na kutathmini changamoto.
  • Waziri Mkuu ametoa udhuru wa Waziri wa ujenzi Dk Magufuli ambaye alitakiwa kuwepo lakini hakuweza kuhudhuria.
  • Bi Mapunjo kaahidi mipango mikubwa ya ujenzi wa viwanda mkoani Mtwara.
  • Mbilinyi kaainisha idadi ya makampuni yaliyoonyesha nia ya kuja kuwekeza Mtwara (sina hakika sana kama ni Mtwara)
Wana Mtwara wameonesha inawezekana, wakati natafakari haya nikawaza ni jinsi gani mikoa ya pembezoni ilivyosahaulika japo ni ya muhimu sana katika ustawi wa nchi yetu. Ukiwauliza wakazi wengi wa mikoa hasa ya Manyara na Singida hasa Dongobesh, Haydom, Mkalama, Basotu, Nduguti, Mbulu, Bashnet, Ilongero, Mtinko na maeneo ambayo bado barabara ni za vumbi watakuambia kuwa hata hawafikirii suala la lami achilia mbali viwanda.
Manyara na singida ni wakulima na wazalishaji wakuu wa alizeti, vitunguu maji, vitunguu saumu na ngano kuliko sehemu yoyote ile nchini, lakinii hakuna viwanda hata vya kusindika vyakula. Ni wakati muafaka wa huduma hizo kuwepo badala ya kusubiri mpaka wananchi wachoke ndipo uamuzi wa dharura ufanyike huku maisha ya watu wengi yakiwa yamepotea.
Ni wakati muafaka kuwa badala ya kusafirisha ngano, akina Bakhresa waje wajenge viwanda vya unga Basotu, Katesh au Haydom. Na badala ya kupeleka mahindi Arusha, tunahitaji viwanda vya kusindika unga wa mahindi Mbulu, Haydom, Karatu, Singida na Babati. 
Singida nako pawepo na Kiwanda cha kusindika nyama za kuku maana sehemu kubwa ya kuku wanaotumika hapa nchini wanatoka Singida kama ambavyo Mtwara kuna viwanda vya korosho. 
MTWARA WAMEONESHA INAWEZEKANA, HATA HUKU KWETU NAKO INAWEZEKANA!

Monday, January 28, 2013

Papaa On Tuesday ………..Hivi Nani anamuandaa Nani Kuwa Nani?


Na Samuel Sasali a.k.a Papaa

Leo Nikiwa nimepoteza Mjomba Pekee niliyenaye baada ya wajomba wengine kufariki aliyekuwa Mkoani Ruvuma Mwl. Allan Chikuni nimeona nikutumie Papaa On Tuesday yangu ya Kwanza Kabisa Kuandika wakati naanda kuandika rasmi Papaa On Tuesday Mwaka 2010 Mwanzoni. Nakutumia kama nilivyokuwa  nimeandika kipindi hicho ndio utajua practice(s) makes perfect. 

Hivi umewahi jiuliza kwanini watu wanajiungaga na mitandao ya Kijamii kama Facebook, Tagged, Twister, marafiki huru, jamii forum e.t.c. Na Umewahi jiuliza madhara ya mitandao hiyo?afadhari marafiki huru inawat fulani hivi hahahahahhaa. Mtandao wangu wakwanza kabisa kujiunga ulikuwa darhotwire, iaseeee , aiseeeee balaaaa, nilipojiunga na facebook Nakumbuka mpaka mwaka jana wana Facebook a.k.a Tabu la Uso walio Tanzania tulikutana pale Cine Club tuliongea weeeeeh, mwaka jana nikajiunga na Wanabidii iko makini kidogo lakini mkiwa wengi mnajua vitu vingi mara nyingi sana huwa hamfanyi coz kila kitu mnataka kuki analyse kiwe na Risk 0. Nilichokuja kugundua katika maisha yangu ya kila siku na kujiuliza hibi nani anamuandaa nani kuwa nani?

Hivi nani honestly amekuwa your life mentor wako, kabisa aliona kuna kakitu ndani yako akasema atakusaidia na ukafika hapo ulipo kwa msaada wake wa hali na mali. Tuache unafika wengi tunasemaga wazazi wetu ama walezi wetu wametufikisha hapa tulipo, lakini kweli?nani amekuandaa wewe kuwa mume mwema, nani amekuandaa wewe kuwa mke mwema, nani amekuandaa leo kuwa kiongozi wa Wananchi, hivi nani anakuandaa wewe kuwa mtumishi wa Mungu, nani anakuandaa wewe “Kutulia”. Mara nyungi sana watu wanasemaga “ooh Papaa hujatulia” teh teh teh hivi nani amenifundisha kutulia teh. Nakuuliza nani?we unadhani shule inakuandaa wewe kuwa mstaarabu?hahahah Mwombeki anasema unasoma handout kisha unajiita msomi?ndo ulikuwa unajiandaa?.


Watanzania tunaogopa kujiunga na East Africa Federation kisa hatujaandaliwa, hahaha uandaliwe? uandaliwe uwe nani?uandaliwe na nani?. Zaburi sura ya 11:3 inasema “Kama msingi ukiharibika mwenye haki atafanya nini?yaani siku hizi kila mtu anajiandaa kwa ubaya rafiki yangu mmoja aliniambia ofisini “Ubaya unanguvu kuliko wema”. Leo watu wanasoma ili wale rushwa, leo watu wanajifunza ngono eti wasiaibike kwenye ndoa, leo kama wewe unafanya mema watu wanakushangaa, ukimsaidia mtu for free tu watu wansema unalako jambo, ajabu kila mtu anajiandaa kwa ubaya wengi wetu hatuamini kabisa kama kuna wema duniani.
Juzi tumeona na kusikia Kanisa la Anglikana kanda ya Kusini wametaka Askofu aliyechaguliwa atolewe kisa?eti alimwaga rushwa….teh teh teh hivi Uaskofu kumbe deal?eeenh, OK assume katoa rushwa kawa askofu, akiwa askofu atafanya nini?teh teh Padri wa Roman Catholic kalawiti, Mtume nanii anafanya ngono, watu wanalaumu bure tu, wanaume siku hizi hawashikiki, yaani anaoa lakini kazi za nje ziko pale pale, watu wanashangaa nani aliwahi kumuandaa kwa wema. Hivi unadhani mume atakaye kuoa ama mke utakayemuoa ameandaliwa?hahaha amendaliwa awe nani?ameandaliwa na nani?kuna marafiki huru kadhaa hapa wanagombea ubunge jamani lini mmeandaliwa kuwa viongozi?


Baada ya kusema hayo jibu la msingi ni “Develop Your Personal Modal”. Kweli tena kilichobaki kila mtu ajiandae kivyako. Unataka kuwa mfanyabiashara?jiandae kivyako, unataka kuoa weka juhudi mwenyewe. Wabongo tuna karama ya kukosoa kuliko kubuni. Ukibuni ndo utawasikia unajua nini?ungefanya moja mbili tatu…..sasa kama unajua si ufanye kwanza???kwani ushari lazima niufate?ajabu eti mtu usipofata Ushauri wake anakasirika, teh teh ajabu ukifata anajisifia…… unataka kuwa kiongozi, Develop Your Personal Development Modal, mambo ya mtu mwingine aje kukuandaa achana nayo we anza ili uwasaidie wengine, ukifanikiwa hautalazimisha kuelekeza watu watu wenyewe watakuwa wanakutafuta ……kama unakitu lazima unakuwa distincted from ordinary people….kama unabisha muulize Mgisa kama anaomba omba sehemu za kuhubiri, kama unacho madhabahu zinakufata, ukiona mtu anaomba mahali akamue gospel jua huna kituSipendi watu wanaomuiga Mwakasege kuongea, sipendi watu wanamuiga Mzee Kulola eti Yoooooooo, unataka niseme?unakuta kijana mdogo kama Nehemini eti anasema Yooooooo, hahahah stupid very stupid sie tukoje?hata kuongea unamuiga mtu, hata kuongea?sie jamani bongo zetu zinatusaidia kwenda haja…ajabu wengine hata haja wanakosea kulenga sijui akili zetu za nini.


Kama hujafa Never too late, jipange mwana jipange. Ukitoka aaah, nawataniaga marafiki zangu nawaambia jamani mnitumie muda huu ambao mna access na mie kabla sijawa wa wengi, itafika muda watakuwa wananiona kwa appointment lakini nani ananiandaaa?ninajiandaa mwenyeweeee na marafiki zangu wananisaidia kukaa mstari mnyoofu. Katika kule unakotaka kwenda Jua hakuna wakukufikisha umiza ubongo..Develop Your Pesonal Development Model, mumeo ama mkeo anaweza kukupeleka chaka, rafiki zako wanaweza kukupeleka chaka, wee kaa mstari kivyako.
Papaa

I am African

By Kwaku Adjekum
I am an African
Not because I was born there
But because my heart beats with Africa’s
I am an African
Not because my skin is black

But because my mind is engaged by Africa
I am an African
Not because I live on its soil
But because my soul is at home in Africa

When Africa weeps for her children
My cheeks are stained with tears
When Africa honors her elders
My head is bowed in respect
When Africa mourns for her victims
My hands are joined in prayer
When Africa celebrates her triumphs
My feet are alive with dancing

I am an African
For her blue skies take my breath away
And my hope for the future is bright
I am an African
For her people greet me as family
And teach me the meaning of community
I am an African
For her wildness quenches my spirit
And brings me closer to the source of life

When the music of Africa beats in the wind
My blood pulses to its rhythm
And I become the essence of music
When the colors of Africa dazzle in the sun
My senses drink in its rainbow
And I become the palette of nature
When the stories of Africa echo round the fire
My feet walk in its pathways
And I become the footprints of history

I am an African
Because she is the cradle of our birth
And nurtures an ancient wisdom
I am an African
Because she lives in the world’s shadow
And bursts with a radiant luminosity
I am an African
Because she is the land of tomorrow
And I recognize her gifts as sacred

Mheshimiwa tunakuomba urejee "Ntwala" hakukaliki

Moja ya Mabango ya wana Mtwara wanaopinga gesi kwenda Dar
Wakati suala la Gesi kule Ntwala bado hali ni tete, Mheshimiwa yupo majuu anatembea juu ye "Red Carpet

Wednesday, January 23, 2013

MAMBO YA DIGITALI: MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA UNAPOTAKA KUNUNUA KOMPYUTA AU LAPTOP.

Mara nyingi nimekuwa nikikumbana na hili swali, "ninataka kununua laptop, ipi ni nzuri? Ni swali ambalo pengine na wewe umekuwa ukijiuliza, mtaalamu wa teknolojia ya Habari na Mawasiliano Victor Mbombo leo anakujuza kwa undani.

Kwa Mwanafunzi, Mfanyabiashara, Mpigapicha (Photographer au videographer) Michezo ya Kompyuta (Computer Games), Mtumiaji wa Nyumbani /matumizi ya kawaida.

1. Wanafunzi 
Mambo makuu kwa mwanafuzi ni bei na kubebeka kwa laptop yenyewe. Laptop inayoweza kubebeka kutoka darasa mpaka darasa, au darasani mpaka kwa Sam muuza chipsi, ndio cha msingi , kwa hiyo kwa wanafunzi wengi huwa ni Notebooks ambazo hazina gharama kubwa, ni ndogo, inatumia nishati ndogo na ni kati tshs 450,000-700,000. Ubaya wake ni kwamba hizi huwa na screen ndogo na hutumia single-core CPUs ambazo zimepunguzwa nguvu.

Option nyingine ni laptop yenye inchi 13, nyembamba, ambayo ubebekaji (portability) yake (uwezo wa kubebeka) ni mzuri, na inapendeza zaidi wa kuandikia au kutumia ukiwa umekaa sehemu tulivu na sio haraka haraka. CPU zake ni dual-core na mara nyingi huja na optical drives. Mfano mzuri ni MacBook za Apple zenye inchi 13.

Nini Cha Kuzingatia: Walau iwe na 1GB ya RAM; 160GB au zaidi za HDD; inchi 13 au chini ya hapo.

2. Mfanyabiashara
Wale ambao mara nyingi huwa barabarani huitaji mashine iliyo haraka, inaydumu na chaji na zaidi ya yote

ThinkPad za Levono na Latitude za Dell ni mifano miwili mizuri ya laptop zilizotengenezwa zikimlenga mfanyabiashara (au kwa lugha rahisi, anayesafiri mara kwa mara) . Bidhaa zote mbili zina security nzuri na imara, pia hardware za in-built software zake zinafanya kazi vizuri na OS (Operating System) yoyote mfano windows, Ubuntu, etc (lakini sio Mac).

Ya kuzingatia: 2GB mpaka 4GB za RAM; 160GB au zaidi kwa Hard Disk; 12 mpaka 15-inch display; Windows Vista Professional au Windows 7 Professional; mobile broadband modem.

3. Mpigapicha na/au Videographer
Wachezaji wa games sio watu pekee wanaohitaji processor yenye nguvu, graphics za ukweli na hard disk space kuuuubwa. Kwa wale ambao wanatengeneza high-definition video or high-resolution photographs huitaji mashine inayojitosheleza hasa! Nimekuwa mpenzi mkubwa sana wa video producing. Miaka ya nyuma nikaanza kujifunza After Effects, FinalCut, etc. Ila kilichosumbua ilikuwa ni mashine. PC yangu RAM 1GB, hard disk 80 GB na vikolombwezo vingine vya kimaskini.

Nikaishia kwenye Windows Movie Maker 

MacBook Pro inch 15 mpaka 17 zile za Apple ndio maarufu na nzuri kwa kazi hii (japo ni ghali). MacBook ni nzuri pia kwa sababu software ya Final Cut, ambayo ndio maarufu DUNIANI kote kwa kutengeneza video, inapatikana kwenye Mac pekee. (Adobe’s Photoshop inapatikana kwenye platform tofauti tofauti, hivyo usijali).

Cha msingi hakikisha SANA SANA SANA kuwa una RAM kubwa…….. 8GB za RAM ndio penyewe. Pia hard disk ya 500GB ingependeza sana, kwa sababu redering in real-time inahitaji RAM/processor faster na inakula space hasa.

Cha kuzingatia: 4GB-8GB of RAM; Hard Disk ya 320GB yenye uwezo wa 7,200rpm, yaani 7,2000r per minute (usijali kama huelewi inamaanisha nini, wewe mwambie muuzaji hivyo ukiwa na uso mkavu..bhaaaas); 17-inch or larger display.

4. Wachezaji Games
Games za sasa hivi zinafika mpaka 20GB na hiyo setup tu! Mambo yanaanza kuwa mengi kama video card, sound drivers, na makolombwezo kibao! Kama wewe ni gamer, basi utahitaji desktop computers, zenye flexible upgradeability, faster components, na yenye uwezo wa kupoa haraka.Ila kwa siku za hivi karibuni, laptops zinazowafaa gamers zina-hit sana.

Ningependekeza kuanzia Core 2 Quad za Intel na Core i7 CPUs kwa 3D gaming, kwa sababu zina GPU nzuri ,kama GeForce N260 za Nvidia.

Ya kuzingatia: 4GB mpaka 8GB za RAM; 320GB au zaidi kwa Hard Disk; display ya inchi 17 au zaidi; bila kusahau the most important, discrete graphics GPU.

5. Mtumiaji wa Nyumbani
Mtu yoyote ambaye hayupo kwenye vipengele nilivyovitaja hapo juu anafiti hapa.Mtumiaji huyu huitaji desktop machine ambazo sio movable, Mashine hizi hutengenezwa kwa asili ya kukaa sehemu moja, ile jikoni, sebuleni, chumbani.

Zile laptop za inchi 15 bado ni maarufu ingawa zile za inchi 14 na 16 zinakuja juu siku hizi. Kila mtengenezaji wa PC hutofautiana na mwingine na huzidiana kila mmoja katika sehemu tofauti. Usikimbilie kununua mashine kuuubwa na kutumia hela nyingi. when all you needed was a simple one! 

Ya kuzingatia: 2GB mpaka 4GB za RAM; 250GB au zaidi kwenye Hard Disk; Display ya inchi 14-16; DVD burning optical drive (kwa asili ya ku-burn CD).

hayo ndio ya kuzingatia uendapo kukunua PC. Kuwa makini na kujua ni kundi lipi size yako.

HOJA BINAFSI: WALIOHUSIKA NA UUZWAJI WA NYUMBA ZA SERIKALI WACHUKULIWE HATUA

Na Joel Nanauka
Nyumba za serikali zilianza kujengwa na utawala wa ujerumani, ambazo zilikadiriwa kujengwa hadi nyumba 10,000 hapa Tanzania. Zilikuwa  inatofautiana kwa ubora, daraja la kwanza, la pili na la tatu kulingana na vyeo serikalini. Nyumba hizi zilijengwa maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam lakini ambazo ni maarufu ni zile UPANGA na OYSTERBAY. Lengo lilikuwa kuwaondolea kero ya umbali wafanyakazi kwenda ofisini, kupunguza mzigo wa gharama za ulipaji kodi kwa serikali na kuondoa kero ya makazi kwa watumishi wa serikali.

Katika awamu ya tatu lilianzishwa wazo la kuuzwa kwa nyumba hizi na Mkuu wa nchi wa wakati huo alijiuzia nyumba iliiyoko SEA VIEW Dar es Salaam. Baada ya hapo HARAMU ikageuka kuwa HALALI, nyumba zilendelea kuuzwa kwa BEI CHEE kwa vigogo mbalimbali; Wakurugenzi, majaji, makatibu wakuu, wakuu wa jeshi, polisi na magereza.


Swala hili limeshawahi kuibuliwa mara kadhaa bungeni halafu linafunikwa: Aliyekuwa mbunge wa vunjo Aloyce kimaro na Mbunge wa Simanjiro Christopher Ole Sendeka(feb 2012) kwa nyakati tofauti wamiweka bayana dhamira yao kuwasilisha hoja binafsi kuhusiana na hili: limeishiwa wapi?


Matokeo yake baadhi ya viongozi walilazimika kuishi hotelini baada ya kuteuliwa na seriklai iliiingia ghrama kubwa kulipia hoteli hizo, mfano Iliripotiwa Mh. Shamsi Vuai Nahodha baada ya kuteuliwa aliishi hotelini kwa kukosa nyumba na alikuwa akilipiwa Millioni 60 kwa mwezi.


KUNA HAJA YA JAMBO HILI KUPATA MTU JASIRI KUWASILISHWA BUNGENI LIWE WAZI, TUKIKAA KIMYA LITAJIRUDIA TENA.
NAOMBA KUWASILISHA


Tuesday, January 22, 2013

Hatimaye Mgogoro kati ya H/Mji Babati na Tanga General wafikia ukingoni

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Babati Mkoani Manyara,Mohamed Omary Farah,akizungumza mbele ya madiwani wa mji huo baada ya kuandikiana makubaliano ya kupatana nje ya Mahakama baina yao na kampuni ya Tanga General iliyokuwa inamiliki shamba la Babati Sisal Estate (kushoto) ni Mkurugenzi wa kampuni hiyo Mustafa Mohamed na (kulia) ni Mkurugenzi wa Mji wa Babati Stella Pascal (Picha na habari kwa Hisani ya Joseph Lyimo)

MGOGORO wa kesi ya muda mrefu,baina ya kampuni ya Tanga General Ltd waliokuwa wamiliki wa shamba la Babati Sisal Estate na Halmashauri ya mji wa Babati umefika ukingoni baada ya pande hizo kupatana nje ya Mahakama. Makubaliano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita,mbele ya madiwani wa halmashauri ya mji wa Babati wakiongozwa na Mwenyekiti wao Mohamed Farah na mkurugenzi wa kampuni hiyo, Mustafa Mohamed na mwana hisa mwenzake Dhiru Chauhan.


Shamba hilo lenye ukubwa wa ekari 4,399 ambalo lilikuwa linalimwa katani hivi sasa ekari 4,149 zitamilikiwa na halmashauri ya mji wa Babati na kampuni ya Tanga General watamiliki ekari 200 zilizobaki. Kampuni hiyo ilimiliki shamba hilo ikilima katani, tangu mwaka 1955 hadi mwaka 1983 walipositisha ulimaji huo na mwaka 1999 Rais Benjamin Mkapa akaifutia umiliki kampuni hiyo na shamba hilo kukabidhiwa halmashauri. 


Kutokana na hali hiyo, kampuni hiyo ilifikisha suala hilo Mahakama Kuu, kitengo cha ardhi mjini Arusha mwaka 2005 na kufungua kesi namba 22/2005 wakipinga ufutwaji wa umiliki kwa kudai kuwa ubatilishaji haukufuata taratibu za kisheria. Katika kesi hiyo,kampuni hiyo ilikuwa inaomba irudishiwe eneo hilo au ilipwe fidia ya sh800 milioni na mahakama hiyo ikaona utaratibu haukufuatwa hivyo walipwe fidia ya sh 49 milioni ila shamba hilo libaki kwenye halmashauri hiyo.

 
Hata hivyo, kamapuni hiyo haikuridhika na hukumu hiyo, hivyo ikakata rufaa mwaka 2005 kwenye Mahakama ya rufaa kwa ombi la rufaa namba 22/2005 wakipinga hukumu hiyo kwa kudai kuwa hawakutendewa haki. Wakati kesi hiyo ikiwa inasubiriwa kupangiwa jaji,ndipo jana mbele ya Baraza la Madiwani wa halmashauri ya mji wa Babati na Mohamed na Chauwan wakatia saini makubaliano ya kufuta kesi na kugawana shamba hilo. 


Akizungumza baada ya kufikia makubaliano hayo, Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Babati, Mohamed Omary Farah aliwapongeza Mohamed na Chauhan kwa uamuzi wao wa kufikia makubaliano hayo nje ya Mahakama. Farah alisema watu hao ambao ni wazaliwa wa Babati, wameonyesha uzalendo kwa kitendo chao cha kuamua kufuta kesi hiyo kwani walianza mazungumzo hayo tangu mwaka 2011 baada ya kuchaguliwa kushika nafasi zao za udiwani.


“Hivi sasa kupitia hitimisho la mgogoro huu wa muda mrefu mji wa Babati umezaliwa upya kwani wananchi watapata fursa mbalimbali kupitia viwanja ambavyo vitakuwepo kutokana na shamba hilo,” alisema Farah.
Hata hivyo, Mwenyekiti huyo aliwataka watumishi wa idara ya ardhi kupitia mipango miji, kuhakikisha kuwa wanawaelekeza wananachi ipasavvyo kuhusiana na ujenzi kwani makubaliano hayo ni ushindi kwa mji wa Babati.
Alisema kuwa eneo la shamba hilo litagawanywa kwa wananchi ambao watauziwa na kununua viwanja ili waweze kujenga nyumba za kuishi na nyumba za biashara kwa ajili ya kuuendeleza mji wao usiwe wazi.


Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Tanga General Ltd, iliyokuwa inamiliki shamba hilo Mustafa Mohamed, alisema anashukuru mgogoro huo umefikia mwisho hivyo watafuta shauri lao Mahakamani.
“Nawashukuru wote waliohusika hadi tukaweza kufikia muafaka huu nje ya Mahakama,akiwemo Mwenyekiti wa halmashauri ya mji na wengineo hivyo tunachohitaji ni ushirikiano kwa yote tuliyokubaliana,”  alisema Mohamed.
Alisema kupitia makubaliano haya anataraji haki itapatikana kwa wote kwani ni muda mrefu mgogoro huo umekuwepo hadi kusababisha baadhi ya shughuli zao kusimama ila wanashukuru kila mmoja ameridhika kuhusiana na shamba hilo.

Papaa On Tuesday......Uonavyo Nafsini Mwako Ndivyo Ulivyo


Na Samuel Sasali

Ninakila Sababu ya Kumshukuru Mungu kula Inapoitwa leo kwa ajili ya Upendo wake kwangu kwenye maisha yangu, ninamshukuru Sababu nina ishi vile atakavyo na sio kama watu wengi watakavyo maana kwenye Kiswahili tunajifunza methali inayosema "Miluzi Mingi Inampoteza Mbwa" we unadhani uwongo??we ishi kama watu wanavyotaka nakuambia utapotea sana. Jua kwanini Upo na Unapaswa Kufanya Nini kwenye maisha utafurahia maisha yako.

Kwenye maisha nimekutana na watu wengine walitakiwa kuwa Wanajeshi wamekuwa Viongozi wa dini, nimekutana na watu walitakiwa kuwa Waalimu Kwa sababu mbali mbali wamekuwa Askari wa Barabarani, kuna watu walitakiwa kuwa Askari Magereza wamekuwa wake za Wachungaji kwani we unadhani bongo maisha yana formula??wengi tunafanya kazi ili tupate hela, kuna wacheza movie wengi sana wako maofisini, kuna waandishi wa habari wengi sana wanauza mitumba, kuna wabunifu wengi sana mambo wako sehemu kwa ajili ya kuganga njaa, kwani we hujijui unapaswa kwa nani??wengine wameajiriwa katika kazi ambazo kwa kweli hawafurahii wanaenda maofisini huku wamekunja nyuso siku wanayocheka ni siku ya Mshahara tu lakini ndani ya mioyo yao wanajua kabisa hawana furaha wanachofanya kwa sasa.

Wewe Unajiona ni nani ndani yako??Kwanini hujaanza kufanya unavyojiona??maana katika kuona tunatofautiana kuna wengine wanajiona wao ni kama mapanzi na kuna wengine wanajiona wao ni kama Simba. Katika maisha ukishinda nafsi yako ujue hakuna cha kukuzuia katika maisha. Wengi tumeshindwa kuwa vile tunavyojiona ndani, vile unavyojiona ndani inaweza kukufanya Ukafurahia ama Ukanyong'onyea maana mtu aonavyo nafsini mwake ndivyo alivyo. Kuna watu wanapokuwa wanawaza mambo mbalimbali wao wanajiona kabisa hawawezi, anatazama changamoto mbalimbali akijumlisha akitoa anajiona kabisa amefeli zoezi hata kabla hajalifanya, we hujawahi kukutana na mtu anasema "mimi nilijua tu kuwa nitashindwa", mara nyingi sana tunakuwa na picha ya ndani pengine tunashinda ama tunashindwa katika mambo fulani.

Unavyojiona nafsini mwako ndivyo ulivyo, kuna mambo ukitazama unaona kabisa unaweza kufanya na ukafanya vizuri, kuna watu wanajua yaani wakiamua kabisa wakiamua ile kutoka ndani ya mioyo wanaweza fanya mambo mazuri sana, kuna watu wanajua kabisa yaaani wakiamua ile ki kweli kweliiiii wanaweza kuimba sana, kuna watu wakiamua ile kikweliii Kweliii Wanaweza Kufanya maajabu, utasikia mtu anasema "Mi Nikiamua Mimi, Mtashangaa" ajabu sana huyu mtu unashangaa haamui. Huyu Mtu kuna picha anaiona ndani yake ambayo mtu mwingine haioni vile ilivyo, tatizo sasa hofu, shaka, wasi wasi swali linakuja "What If mambo yasiwe vile ninavyodhani", nafsi inaona picha kubwa ya kuweza ila akili inaanza ushuhuda.

Hofu na mashaka na wasi wasi na kuto kujiamini kumesababisha watu wengi sana katika maisha wasiamue ile kikweliii Kweliii, huwezi kuishinda hofu as longer you have an Option, huwezi kuamua Kikwelii Kweliii sababu unajia mbadala, Ukimuona Mtu ameamua Kikwelii Kweliii Ujue amekataa Kutosheka na Afadhari. Ukitosheka na Afadhari kwenye maisha hauwezi kuthubutu, utakuwa unajiona kabisa wewe ni Simba lakini Unamatendo ya Mbuzi, Ikitazama Simba wengine unajiona kabisa mbona mimi ni Simba??lakini ikifika saa ya kuunguruma kama Simba unalia Meeee Meee Kama Mbuzi. Ukijitazama nafsini mwako unajua Kabisa Uwezo wa Kufanya zaidi ya hapo unapofanya sasa unao lakini hujawahi jiuliza kwa nini haufanyi kwa kiwango kile kile??we unadhani uko huvyo ulivyo sababu huwezi??huitaji mtu wa pili kukuthibitishia kuwa unaweza unajua kuwa unaweza na nafsi yako inakushihudia kuwa unaweza issue sasa kuishinda hofu.

Yaani mtu ana hofu kubwa ya kuogopa hofu ambayo haipo, utamsikia mtu anasema mara niamue kikwelii kweliii Ibumeeee, itokee negative sijui itakuaje?tuna mawazo mengi sana yanayoshindana na nafsi zetu, nafsi inasema Unaweza akili inasema hujaona wenzio wamechemsha, nafsi inasema unaweza kufanya zaidi, akili inasema utajichosha bure, Ukiweza Ishinda nafsi yako na akili yako jua hakuna wa kukuzuia, ugomvi wa nafsi na akili hauwezi kuisha kwenye maisha maana mwili unajipendelea sababu uko njee nafsi inataka kujilipua uende kule unakopaswa kwenda ndio maana Biblia ikaandika "roho/nafsi i radhi lakini mwili ni dhaifu" achana kabisa na mtu wa nje anasababu milioni 5 za kutokufanya kitu kimoja ambacho nafsi na roho yako viko tayari kufanya.

Unajiona wewe ni nani na kwanini hujaanza fanya kile ambacho wewe unajiona unapaswa kuwa, ukitazama vizuri utagundua kwanza haujauamua kuwa vile unavyotaka kuwa na pili una hofu ya kule unakotaka kuwa unahisi mambo yanaweza kuwa sio mambo ukabaki kujuta, umeona heri ubake hapo hapo ulipo kwenye maisha kuliko uende usikokujua, mwaka huu hautaakuwa tofauti sana na mwaka jana, waliofanya mapya ni wale walioamua kufanya mambo mapya, risk takers watu wanaothubutu ndio ambao hupiga hatua katika maisha yao. Mtu aonavyo nafsini mwake ndivyo alivyo.

Monday, January 21, 2013

Matukio Muhimu ya mwaka 2012 katika Picha

Mwaka 2012 ulikuwa na "matukio mengi" sana na yakukumbukwa hasa na wasomaji wa Ohayoda. Moja kubwa ikiwa ni OHAYODA yenyewe kuanza kuwepo hewani mnamo Mwezi Mei 2012, na kuanzia hapo imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wasomaji wake wanapata kile wanachostahili. Matokio yaliyopamba mwaka 2012 ni pamoja na Kampeni ya upandaji miti Haydom, Tamasha la Utamaduni, Ziara ya Balozi wa Namibia nchini, Vuguvugu la wananchi kuwaondoa viongozi wasiowajibika na Tuzo mbalimbali ambazo 4CCP na Ohayoda zilizojinyakulia kutoka Norwegian Church Aid (NCA) 

Wanafunzi wa shule mbalimbali za msingi na sekondari za Haydom wakibeba mabango yenye jumbe mbalimbali wakati wa kampeni ya upandaji miti "The Green Campaign"
Balozi wa Namibia Nchini akijaribu kurusha mshale, alipotembelea  Mongo wa Mono, Yaeda Chini. Ziara iliyoratibiwa na 4CCP


Kwa hakika mwaka 2012 ulikuwa na "Nuksi" kwa Bryson Emmanuel aliyekuwa mwenyekiti wa Serikali ya kijiji cha Haydom. Bryson aliondolewa kwa nguvu ya Umma baada ya "wenye nchi" kumpigia kura ya kutokua na imani naye na uchaguzi mpya unatarajiwa kutangazwa mwaka huu

Mwanasheria wa H/W ya Mbulu ambaye pia ni Afisa Ardhi wa Wilaya Bw. Deogratius Mathiya akifafanua jambo wakati wa vuguvugu kumng'oa Bw. Bryson. Anayepiga picha ni Charles Masanyika wa ITV

Mwaka 2012 4CCP ilifanya kazi na kupata ushirikiano mkubwa sana kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Mbulu ndugu Anatoly Choya, hapa blogger alikuwa akijadiliana jambo na "rais" wa wilaya alipotembelea kituo cha utamaduni cha Haydom

Blogger na Mratibu Msaidizi wa 4CCP wakikagua nakala za filamu zinazoonesha historia na maisha ya Wairaqw, wadatooga, wahadzabe na Wanyiramba/wanyisanzu iliyotayarishwa na 4CCP 

Mkuu wa Wilaya ya Mbulu akipanda mti katika kampeni ya upandaji miti Haydom

Katibu Mkuu wa KKKT dayosisi ya Mbulu (kushoto) akiwa na Mhasibu wa Dayosisi hiyo na dereva wa Askofu wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa washirika wa NCA uliofanyika katika kituo cha TEC Kurasini jijini Dar es Salaam

"Bosi" wangu ambaye ni mratibu msaidizi wa 4CCP alifanya kweli kwa kuhakikisha kuwa mwaka 2012 haupiti bila kubariki ndoa yake. HONGERA ELIMINATA! 4CCP na Ohayoda inawatakia maisha mema na mumeo

4CCP ilitia fora katika maonesho wakati wa Mkutano mkuu wa mwaka wa washirika wa NCA. Kutoka kushoto ni Pendo, Nizar (wote wa NCA), Blogger, Eliminata na Simon Meigaro (CCT) na kwa nyuma ni Tony wa AEE

Filamu iliyoandaliwa na 4CCP ikizinduliwa wakati wa Mkutano mkuu wa mwaka wa NCA. Kutoka kushoto ni Mwakilishi wa BAKWATA(jina halijapatikana), Bi. Trine (mwakilishi wa NCA nchini), Askofu Zebedayo Daudi wa KKKT D/Mbulu, Eli,inata Awet na Mama Mosha ambaye ni Meneja Miradi wa NCA

Blogger akijibu maswali kutoka kwa wakaguzi wa Maonesho huku Eliminata Awet akifuatilia mchakato kwa karibu. 4CCP iliibuka kidedea

Simon Meigaro akiileza jambo huku Nelson Faustin, Nizar na Sarah wakipiga picha pamoja na Blogger....ilikuwa rahaaa utamuuu

4CCP na ohayoda zilijinyakulia tuzo mbili kutoka kwa NCA. 4CCP ilishinda tuzo ya maonesho bora na tuzo ya ubunifu kwa kupitia Ohayoda kwa kuandika habari za vijijini hasa utawala bora, mazingira, utamaduni na elimu!

Timu ya 4CCP na ohayoda ikipokea zawadi wakati wa Mkutano Mkuu wa NCA Desemba 2012

Zawadiiiii...Tumeshinda

Pengine mafanikio makubwa kuliko yote kwa mwaka 2012 ni kufanyika kwa Tamasha la Utamaduni Haydom ambalo lilikuwa la kwanza kabisa na kuwavutia watu kutoka sehemu mbalimbali nchini. Mwaka 2013 tunatarajia kuwa na Tamasha kubwa zaidi kuanzia tarehe 2 mpaka 8 Septemba 

Monday, January 14, 2013

Papaa On Tuesday........Everyone Has A Story....Its a Matter Of Time

 Na Samuel Sasali
Ninawasalimu Kupitia Jina la Bwana Wangu Yesu Kristo siku hii Ya Leo. Nimatumaini Yangu Ya Kuwa wewe ni Mzima na Unaendelea Vema na Shughuli za Ujenzi Wa Taifa. Mwenzi January leo tunaugawa nusu kwa nusu ndio mwaka 2013 umeanza na kasi yake. Ninajua ni mwezi ambao kama unatafuta kukopa hela basi ujue unahitaji kuwa na vyanzo vya uhakika visivyopungua 15 maana ni mwezi ambao majority ya maisha ya kawaida ya Mtanzania tupo kwenye kuishiwa maana kwetu kujifunza kuwa kila mwezi january ni mwezi mgumu ni zoezi linalohitaji kugeuzwa nia. Kwa maombi maalum ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Vya Dar-es-Salaam, nimelazimika kufanya mwendelezo wa Papaa On Tuesday niliyoandika Mwaka Jana.


Kwenye maisha yetu haya ukiona mtu leo anaendesha gari, amejenga nyumba, ana huduma yake, amejenga kanisa, ameolewa. Kila Mmoja wetu anachokitu cha kusema. Ukimuona tu mtu unaweza kusema mambo yake yalikuwa mteremko sana wewe unapata tabu peke yako duniani. Kumbe laiti kama ungejua everyone has a story to tell.

Kuna watu huwa wanapenda kusema "afadhali ya Wewe", unapimaje afadhali??afadhali ni suala la Mtazamo kwa maana ninachojua afadhali zetu hazifanani, afadhali yako sio yangu, afadhali kama anasa, inawezekana Anasa kwangu kumbe kwako kawaida, haya ni maisha yetu ya kila siku katika maisha kila siku eti afadhali ya Jana. Kuna watu wamenyong'onyea kabisa kwenye maisha kama sio wamenyong'onyeshwa na wengine hapa duniani nakuona wao ndio hawafai katika maisha wao hawana bahati. Pengine kazi walizotegemea wamekosa, Tender walizotegemea Wamekosa, Wateja Waliowategemea Wamekimbia, Shule walizotegemea wamefukuzwa, Ndoa walizotegemea zingekuwa furaha leo kila Mtu analala kwake, Watumishi wa Mungu waliowategemea Wamewatenda, Wanaume ama Wanawake waliodhani Wange date wote Kumbe Wamewakosa, yaani kila Ukijitafakari wewe ndio unajiona taka taka, Watu wanakuona Unatabasamu Kila Ukiwa nao laiti kama Wangepata Access ya Moyo Wako nakuona wingu la Simanzi ulilolibeba basi wangepaswa kukupa ambulance ya Faraja kila sekunde. Kumbe Nyuso zetu zinaficha sana yaliyo ndani ya Mioyo yetu. Mwaka 2013 unaouona kama ni mrefu sana safari kwako imeanza na Ukakasi mwingi sana wa kutosha.
Kila Mmoja wetu ana sehemu ametoka, kuna watu ukisikiliza Historia zao, walikotoka lakini pale walipo sasa basi utaamini afadhali zetu hazifanani. Kwenye Maisha haya tunayoishi usione tu watu leo wanavaa tai, wengine wanavaa high hills ukatamani kuwa kama wao, thubutu yako ukiona mtu leo amekaa kwenye kaofisi unamwambia "heri wewe mwenye kazi" laiti kama ungalijua huyu mtu ilimgharimu nini leo kukaa kwenye hiyo ofisi usingediriki kumtamani wakati huo pengine ndio ungemkatisha tamaa.
Kuna watu leo wana ndoa nzuri sababu kuna wengine Mungu ameamua kuwapa faraja ya mioyo yao maana yake, hapo kabla mioyo ilikuwa ina viraka vya kutosha sana ya kuumizwa, kuna watu Mungu amewapa leo kazi nzuri kama faraja ya kule walikopitia, kuna watu wakikuambia historia za maisha yao utaona wameongezea chumvi ili kunogesha kumbe ni kweli. Kuna Wengine duniani ni Miujiza kila mume akikumbuka Mke aliyempa anatoa machozi maana ni "Muujiza". Kuna wengine Wazazi Wakituona Watoto wao Wanakumbuka Muujiza Mungu aliyotenda kwenye maisha yao.
Mimi ni Muujiza kwetu, mimi ni jibu la Maombi, mimi sio mtoto wa matokeo ya "Uzazi Wa Mpango". Baba yangu alipomuoa Mama Yangu, ndugu za Baba yangu hawakuwa Wamempenda Mama Yangu kwa sababu kadha wa Kadha hata kwenye harusi ya baba na Mama, Familia ya Kina baba wengi walikacha kwenda kwenye harusi kama sio wote. Shangazi yake na Baba alimwambia baba yangu kwa kuwa ameamua kuoa mwanamke wasie ridhia basi kama Itatokea Wakapata mtoto kwenye maisha yao akakate kidole gumba cha Shangazi yake. Unaweza pata picha unaenda kuanza maisha unaenda kuoa huku kila mtu amekunenea mabaya na wakitaraji mabaya yakupate ili wakucheke. Baada ya Ndoa ya baba na Mama ilipita Miaka ambayo ubongo ungeanza kusema yamkini hatutapata Mtoto, na wakati huo mama yetu alikuwa na afya mgogoro baada ya miaka kadhaa kupita bila mtoto. Mama aliwahi niambia akaingia katika maombi kumwambia Mungu Kwanza amponye, then ampe Kicheko kwenye maisha yake, sababu amekuwa mtu wa kudharauliwa sababu ameamua kumngojea Mungu, akiwa kwenye maombi akafanya nadhiri kwa Mungu akasema "Kama Mungu Ukinipa Mtoto, Ninaomba Mtoto Wangu Wa Kwanza Awe Wa Kiume, Nitamtoa huyo Mtoto Kwako Kama Sadaka, na Nitamwita Jina Lake Samuel, Sababu Samuel Maana yake Nalimuomba Kwa Bwana na Nikamtoa Kwa Bwana". Baada Ya Maombi hayo na baada ya Miezi Michache kupita Mama yangu Akapona Ugonjwa wake na Kisha akapata Ujauzito, Mtoto aliyezaliwa akaitwa Samuel Ze Blogger. Kila Mama yangu anaponitazama leo anakumbuka Mungu alivyomfuta machozi katikati ya waliomdharau leo ukiona hiki kichwa Cha Blogger kinatoa madesa ya ukweli, unasema "Lina Heri Tumbo Lililokuzaa" Ukitaka kupata mtoto kama mimi au zaidi ya mimi there is a PRICE to Pay.
Kuna watu sababu ya aibu na shida zinazowakabili waliwahi kujuta kwanini walizaliwa na kwanini walizaliwa katika Ukoo huo waliozaliwa, kujuta hakujawahi kumsaidia mtu kama sio kuamua kutenda. Maisha yetu kila mmoja kwa sehemu yake ni full adventure. Kuna familia zingine umeolewa ama umeoa huko basi full tegemezi yaani wanawategemea mpaka aibu ya kuwanyima inapotea kabisa. Kuna watu tumewahi ama Mtaa, Kuna watu wamewahi ama ofisi, kuna watu wamewahi kimbia nchi kama sio Mkoa kutokana na aibu na hali za maisha, bora kubeba mabox Uingereza kuliko kuwa dereva wa dala dala Bongo watu wamekimbia nchi zao, Watu Wamekimbia ndoa zao, life is full oF Stories, Kama tungekuwa tunaandika Biblia kutoka kule ulikotoka mpaka ulipo basi ungeweza tengeneza Sura Kadhaa katika Kitabu Cha Mwanzo. Niliwahi Kuandika kwenye Papaa On Tuesday moja kuwa "God's Ways Are Zigzag" yaani njia za Mungu zimepinda pinda sana Safari Ya Siku 40 inaweza kukugharimu Miaka 40 kama wana wa Israel, Haijalishi ni Miaka Mingapi lakini Kanani Utaingia.
Kuna Watu wako Bongo na pengine hawafanyi kazi nzuri kama wewe unayofanya na umewazi kipato lakini huwezi amini wamewajengea wazazi wao kama sio mzazi wake mahali pa Kujistiri, Kuna watu Wana hali mbaya sana lakini wao ndo Nguzo Za Familia, Kuna Watu nakumbuka nimesoma nao Chuo, Boom analopata ndilo anasomeshea mdogo wake nae apate Elimu. Unaongea nini wewe unayelalamika Mshahara hautoshi kutwa kucha kumbe tu unaongeza matumizi ya kutoka kupanda Bajaj kwenda Taxi kisa mshahara umepanda, kuna watu hawajawahi kuwa na kitu kinaitwa Mshahara kwenye maisha yao, wamekuwa Wakiomba Kila siku Usiku na Mchana Wapaje Japo Nusu ya Mshahara Wako unaopata na Wanaamini Wangefanya Maajabu duniani, mbaya kwako ni afadhali ya mtu duniani.
Huwezi Jua thamani ya Kitu Mpaka Utakapokuwa umepoteza kile ulichonacho cha sasa. Chukua dakika kadhaa tafakari maisha yako kwa muda, au tafakari mtu unayemfahamu na unatamani kuwa kama yeye, Muulize Kama hana Kitu Cha Kukuambia. Mimi nina amini Its a matter Of time.
Its a Matter Of Time, mwombe Mungu Kisha Komaa na Kile unachokifanya. Kulia haitakusaidia na haijawahi Msaidia Mtu, na hata Ukilia Lia Strategically , Usilie Kihasara, Umewahi Msikia Mtu anayeitwa Batmayo kwenye Biblia Usikie aliliaje alipazaje Sauti. Unakuta mtu ana shida analia mpaka anatia huruma kisha unamuuliza "Nikusaidiaje katika hili" anasema "hata Sijui". Batmayo ye alilia "Mwana Wa Daudi Unirehemu" Yesu akamuuliza 'Unataka Nikufanyie Nini?".."Nataka Kuona" akasema "Ona" Kitu na Box hapo hapo. Usipate tabu sana kujilaumu na kupoteza muda kuwaza namna ulivyojikwa Kimaisha na Kuanguka bali waza namna gani ninasimama na Kuendelea na Maisha. Lililokupata kuna mtu amewahi pata kama hilo pengine kubwa zaidi ya hilo lakini Mungu ni Mwaminifu na Mungu sio Anna Makinda. Every One has a Story.....Its a Matter Of Time.
Everyone has a Story......Its a Matter Of Time.....Think Differently and Make a Difference.
Papaa Ze Blogger.
0713 494110.

Wednesday, January 9, 2013

Tumerejea kutoka kwenye Mapumziko ya Mwisho wa Mwaka

Heri ya mwaka mpya 2013 wapenzi wasomaji wa Ohayoda!
Kwa takribani mwezi mzima timu nzima ya Ohayoda ilikuwa katika mapumziko ya Krismasi na Mwaka mpya hivyo wasomaji wetu wamekosa mambo mengi ambayo yamekuwa yakitokea katika jamii yetu, mambo ambayo wamekuwa wakitegemea Ohayoda kuwa mstari wa mbele kuwaletea.


Aidha tunapenda kuwashukuru wasomaji wetu kwa kuwa nasi toka tulipoanza takribani Mwezi Mei mwaka jana, wasomaji wetu wamekuwa sababu ya sisi kupata ujasiri na ari ya kusonga mbele na kuthubutu kuwaletea mambo kem kem wakati mwingine kukumbana na vitisho, kukatishwa tamaa na hata kukosa sababu au msukumo wa kufanya kutoka ndani..

Mwaka 2012 umekuwa na mafanikio makubwa sana kwetu, kwanza kabisa uthubutu wa kuanza hatua ya kwanza na kuandika makala ya kwanza...kisha ya pili....ya tatu...huku tukiwa hatujui hatua inayofuata itakuwaje na wasomaji wetu watatupokea vipi, baada ya mwezi moja, ilikuwa ni zaidi ya muujiza kwani hata pasipo matangazo na tukiwa tunaandika kutoka Haydom, Ohayoda ilipasua anga na kujipatia umaarufu mkubwa na kukusanya wasomaji mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi, tukazidi kupata msukumo na kuendelea kuandika makala na habari mbalimbali tukazidi kusonga mbele.......

Kati ya habari ambazo zilikuwa na mvuto kwa wasomaji wetu mwaka 2012 ni pamoja na Mashindano ya Urembo ambapo Miss Haydom Lucy Stephano aliweza kuiwakilisha vyema Haydom katika ngazi zote hadi kufikia kushinda taji la Miss Photogenic Tanzania 2012. Habari ya Hhando Samo kujiteka na kusababisha dhahma kubwa katika mji wa Haydom na Viunga vyake, Makala za sintofaham, ujio wa Balozi wa Namibia nchini, Tamasha la Utamaduni Haydom na Makala Mbalimbali ya utamaduni hasa Historia na Maisha ya Wairaqw, wadatoga, Wanyiramba na Wahadzabe.

Kubwa zaidi ambalo pengine wasomaji wetu hawakupata fursa ya kufahamu ni Ohayoda kusinda tuzo ya Ubunifu iliyotolewa na Shirika la Misaada la Kanisa la Norway (Norwegian Church Aid-Tanzania), tuzo ambayo bila wasomaji wetu tusingeweza kuipata na hii tuzo ni kwa ajili ya wasomaji wetu, ni zawadi ambayo wasomaji wetu wametupa kwa kutambua mchango wetu katika kuleta mabadiliko chanya katika jamii yetu na kuweza kujenga jamii yenye haki, usawa, uwazi. amani na utulivu. Ni imani yetu kuwa kwa mwaka 2013 tutazoa tuzo nyingine nyingi zaidi.

Mwaka ndio umeanza ikiwa ni siku ya nane toka mwaka 2012 uishe, tunatamani kuwaletea mengi lakini bbila ushiriki wako hatutafika malengo yetu, tafadhali kama unalolote la kushirikiana nasi, iwe ni kutoa habari au kushiriki katika uandishi wa makala mbalimbali iwe ya kisiasa, michezo, elimu, utamaduni, afya au hata matangazo, usisite kuwasiliana nasi kwa namba za simu hapo juu. USHIRIKI WAKO NI ZAIDI YA MUHIMU

Mungu Ibariki Afrika
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Ohayoda
Mungu ubariki mwaka 2013 uwe na mafaninikio makubwa kwetu wote. Amen
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda