Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Friday, October 18, 2013

MICHEZO:Dereva wa F1 Maria Villota afarikiNa Mwandishi Wetu.


Dereva mashuhuri mwanamke wa mashindano ya langalanga Formula 1 Maria De Villota amepatikana amefariki ndani ya chumba cha hoteli moja mjini Seville, Hispania.

Shirika la utangazaji la Uingereza BBC ilieleza kuwa msemaji wa polisi alisema."Tunachukulia kilikua kifo cha kawaida, lakini hatuwezi kuthibitisha chochote na uchunguzi utafanywa kuhusu kifo chake"

De Villota, mwenye umri wa miaka 33,alikua dereva wa akiba wa langalanga. Alipofuka jicho lake la kulia katika ajali ya mwezi wa Julai mwaka jana alipokua akifanya mazoezi na timu ya Marussia
.
Alipata majeraha mabaya kichwani na usoni baada ya kugongana na lorry katika jimbo la Cambridgeshire, Uingereza lakini aliruhusiwa kuanza tena kuendesha gari.

Iliarifiwa kuwa De Villota, binti wa dereva wa zamani wa mashindano ya Formula 1, Emilio De Villota,alikwenda Seville kuzindua kitabu kuhusu maisha yake.Timu na madereva wa langalanga wameelezea kushtushwa kwao na msiba huo.
Jenson Button wa Uingereza amesema. "inasikitisha sana. Msichana huyu amekumbwa na masaibu mengi sana, kupita yale yanayowakumba watu wengi duniani. Ni habari zilizotushtua timu nzima na jamii nzima ya mbio za langalanga."

"tulimuona mwaka huu mjini Barcelona.Tukifanya kazi kwa wakfu wa kuwasaidia watoto na alikua wa kwanza kujitolea na kuwashawishi madereva wengi kujiunga nasi.Alikua akichangia mengi kwa jamii ."


 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda