Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Friday, October 18, 2013

Michezo:Boateng hatawakilisha Ghana,Kumasi

Na Mwandishi Wetu.

Mchezaji wa kiungo cha kati wa timu ya taifa ya Ghana, Kevin-Prince Boateng atakosa mechi ya mkondo wa kwanza ya kujitafutia nafasi kwenye dimba la kombe la dunia dhidi ya Misri, kutokana na jeraha la goti.
Mechi hiyo itachezwa mjini Kumasi

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, alipata jeraha hilo wakati wa mechi ya klabu yake ya Schalke ya Ujerumani kwenye mechi za ligi ya Bundesliga.

Na baada ya kufanyiwa ukaguzi na madakatri, imegunduliwa kuwa Boateng lazima afanyiwe upasuaji kwenye goti lake la kushoto.

Kocha wa timu ya Black Stars, Kwesi Appiah, ameamua kutafuta mchezaji mwingine kuchukua nafasi ya Boateng.

Mechi za mkondo wa pili za kufuzu kwa kombe la dunia litakalochezwa nchini Brazil mwaka ujao, zitachezwa mjini Cairo, Misri tarehe 19 Novemba.
Hata hivyo, Ghana wameomba michuano hiyo kuhamishiwa kwingineko kwa sababu za usalama kufuatia hali ilivyo nchini Misri.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda