Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Thursday, October 17, 2013

Mang’ola wafunga ofisi ya Kijiji

Na Sophia Fundi
Wananchi wa kijiji cha Mang’ola Barazani, wilayani Karatu Mkoani Arusha, wamefunga ofisi ya kijiji chao wiki iliyopita, kwa kile walichodai kuwa mwenyekiti wa kijiji hicho ameuza ardhi ya wananchi.
Wakizungumza kwa jazba wananchi hao mbele ya Mkuu wa wilaya hiyo Felix Ntibenda walimtuhumu mwenyekiti wa kjiji hicho Jakob Welwel kwa kuwasaliti na kuuza ardhi ya kijiji yenye ukubwa wa ekari 35 kwa kampuni ya utalii ya Kibo.
Walidai kuwa ardhi hiyo ni  ya wananchi wa kijiji hicho lakini mwenyekiti huyo ameingia mkataba na kampuni hiyo bila kuwashirikisha wananchi kwa kutumia mikutano mikuu ya kijiji.
Pamoja na wananchi hao kufunga ofisi ya kijiji kwa siku nne, wananchi hao waliandamana hadi katika eneo hilo lenye mgogoro na kuzuia shughuli zozote kufanyika katika eneo hilo .
Akizungumza baada ya kupokea malalamiko ya wananchi mkuu wa wilaya Felix Ntibenda aliyefuatana na kamati ya ulinzi ya wilaya alisema kuwa kuuza ardhi ya wananchi bila makubaliano ni kosa hivyo aliwaahidi wananchi hao kulitatua tatizo hilo.
Ntibenda alisema kuwa ataunda tume itakayoanza kazi zake leo ya kuchunguza tuhuma hizo dhidi ya mwenyekiti wa kjiji ambaye pia ni diwani wa kata ya Mangola kama ni za kweli na kama ni kweli atachukuliwa hatua.
Alidai kuwa kufunga ofisi ya kijiji ni kosa la jinai hivyo aliutaka uongozi wa zamani unaotuhumiwa kupisha tume kufanya kazi zake na ofisi kufunguliwa kwani shughuli za maendelea za wananchi zinakwama.
Mwandishi wa gazeti hili alifanikiwa kumpata mwenyekiti huyo ambaye pia ni diwani kuhusiana na tuhuma hizo alidai kuwa tuhuma hizo si za msingi kwani eneo hilo ni la kwake na yeye aliuza kama eneo lake halali na si la kijiji.


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda