Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Friday, October 18, 2013

Hhasama walia na wachimbaji haramu wa dhahabuNa Augustino Floriani 


Wananchi wa kijiji cha Hhasama kata ya Nahsey Wilayani Mbulu Mkoani Manyara, wameiomba Serikali iingilie kati mgogoro wa mara kwa mara kuhusu wachimbaji haramu wa madini ya dhahabu kijijini hapo.

Wakizungumza na Ohayoda wananchi hao wamewalalamikia wachimbaji wadogo wadogo wanaochimba madini ya dhahabu wakidai kuwa wanaleta usumbufu na uharibifu wa mazingira katika kijiji hicho.

Mmoja kati ya wananchi hao Thomas Daffi alisema pale wanapochimbwa ni karibu sana na vyanzo vya maji na hayo ndio maji wanayoyategemea pale kijijini kwa matumizi ya kila siku na wachimbaji wanaosha madini karibu kabisa na maji hii ni hatari kwa afya zao.

Kwa upande wake, Mjumbe wa Mkutano mkuu wa CCM Taifa NEC wilaya ya Mbulu, Flatey Gregory Massay naye aliungana na wananchi katika kuitaka Serikali ishirikiane na wananchi wa eneo husika ili kutokomeza kero na migogoro hiyo na kusitisha uchimbaji huo.

Pia, Ohayoda lilifanya mahojianao na Mbunge wa jimbo la Mbulu, Mustapha Akonay kuhusu uchimbaji wa madini katika eneo hilo na alisema kuwa mpaka sasa hakuma mtu wala kampuni kwa mujibu wa sheria aliyeruhusiwa kufanya shughuli za uchimbaji wa madini.

 “Hadi hivi sasa mpaka ninavyoongeza na wewe kisheria hakuna mtu aliye ruhusiwa kufanya shughuli za uchimbaji wa madini katika eneo hilo na kama wapo hao ni wavamizi,’’ alisema Akonay.

 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda