Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Friday, October 18, 2013

Gama achachamaa na mpango wa matokeo makubwa sasaNa Mwandishi wetu


Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama,  amesema utekelezaji wa mpango wa matokeo makubwa sasa” Big Result Now” hautatekelezeka kwa watendaji wa serikali kuchelewa kuingia katika vikao huku akiwataka kubadili utendaji kazi wa mazoea.

Gama ametoa kauli hiyo baada ya kukerwa na  baadhi ya watendaji wa serikali kuchelewa katika vikao vya kazi huku akimtaka katibu tawala wa mkoa Dk. Faisal Issa kuhakikisha anasimamia kuanza kwa vikao kulingana na muda uliopangwa.

Akizungumzana wakati wa kuapishwa kwa viongozi wa elimu ngazi ya Halmashauri kwa ajili ya kusimamia mpango wa matokeo makubwa sasa “Big Results Now”  kwa sekta ya elimu, Gama alimtaka katibu tawala huyo kufunga milango ya ukumbi mara baada ya yeye kuingia.

“Sasa RAS pamoja na kazi nzuri unayoifanya, tukubaliane vikao vyetu vinavyokuja ni vikao vya kazi hakuna kikao cha kubabaisha, tukikubaliana tukutane saa mbili na nusu iwe hivyo, potelea mbali afadhali tufanye kikao na watu wawili wengine tuwahoji kwa nini hawakufika kwenye vikao na naomba RAS nikiingia kwenye ukumbi funga mlango,” alisema Gama.

Alisema mpango wa matokeo makubwa sasa, bila kuwa na nidhamu ya utendaji kazi na mabadiliko katika kufanya kazi kwa mazoea, hautakuwa na maana.

Akizungumzia mpango huo kwa upande wa sekta ya elimu, Gama alisema katika kutekeleza maagizo ya Waziri Mkuu aliyoyatoa mwanzoni mwa Septemba  tayari amezungumza na walimu ambao ndio wataalam katika utekelezaji wa mpango huo na kukutana na changamoto mbalimbali.

Awali katika taarifa yake Afisa elimu mkoa wa Kilimanjaro Ruth Malisa alisema mkoa wa Kilimanjaro umeitikia wito wa kitaifa na unashiriki ipasavyo katika utekelezaji wa mpango huo katika sekta katika sekta ya elimu.

 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda