Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Friday, October 18, 2013

DC Babati aunda tume ya wazee 30 wa kimila Vilima Vitatu
Na Gift Thadey.

Mkuu wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, Khalid Mandia, ameunda tume ya wazee 30 wa kimila wa Kijiji cha Vilima Vitatu kwa ajili ya kusuluhisha mgogoro wa muda mrefu wa ardhi baina ya jamii ya wafugaji ya kidatoga na  kijiji hicho.

Hatua hiyo ya Mandia kuunda tume hiyo ya wazee wa kimila 30 wa jamii ya wadatoga, wambugwe na wamasai inatokana na mgogoro huo ambapo hivi karibuni ulipelekea  nyumba kadhaa za jamii ya wafugaji wa kidatoga kuchomwa moto.

Nyumba hizo zilichomwa moto na baadhi ya wana kijiji wa Vilima Vitatu wa jamii ya wambugwe ambapo watu wawili walikamatwa wakidaiwa kuhusika na uhalifu huo. 

Akizungumza na waandishi wa habari juzi, Mandia alisema lengo la kuunda tume hiyo ambayo yeye ndiye atakayekuwa Mwenyekiti wake, ni kuhakikisha mgogoro huo unamalizwa ili kuleta hali ya utulivu kwenye kijiji hicho.

“Mgogoro huu unakuzwa na kuendelezwa na baadhi ya watu kutoka nje ya Babati hivyo tutahakikisha kupitia tume hii tunaumaliza kwani Mahakama ilitoa hukumu kwa kijiji kupewa eneo hilo siyo hao wafugaji,” alisema Mandia.

Alisema wakazi wa kijiji hicho kupitia mkutano mkuu  katika mpango wa matumizi bora ya ardhi, walitenga maeneo ya malisho, makazi, kilimo na maeneo mengine hivyo eneo hilo walitenga kwa ajili ya uhifadhi.

“Hapa ni elimu haijatolewa ipasavyo kwa hawa wafugaji na pia kuna watu wanawachochea kuwa wasitoke kwenye eneo hilo ambalo limetengwa na mkutano mkuu wa kijiji kwa ajili ya uhifadhi,” alisema Mandia.
Hata hivyo, Mandia amesikitishwa na kitendo cha baadhi ya vyombo vya habari kutangaza masuala ya kujiepusha na vurugu ili kikundi cha ugaidi cha Alshabab kisijingize eneo hilo.

"Mimi ajenda yangu haikuwa Alshabab, bali nilizungumza kwa kirefu juu ya kudumisha amani lakini wenyewe waliona jambo la maana ni Alshabab peke yake," alisema Mandia.

Pia, alisikitishwa na baadhi ya vyombo vya habari kuandika kuwa Mwenyekiti wa kijiji hicho Erasto Belela alifanyiwa fujo na kufukuzwa mkutanoni ili hali siyo jambo la kweli. 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda