Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Thursday, October 17, 2013

Askari 29 wa Burunge WMA wahitimu mafunzo

Na Andrew Joseph

Askari 29 hifadhi ya jamii ya Burunge WMA Wilayani Babati Mkoani Manyara, wamepatiwa mafunzo yenye lengo la kunusuru wanyamapori kutokana na ujangili uliokithiri katika maeneo hayo.
Akifunga mafunzo hayo wiki iliyopita, Mkuu wa hifadhi ya Taifa ya Tarangire Stephano Qolli alisema mafunzo hayo yamewajengea uwezo askari hao ikiwemo mbinu ya ukamataji watuhumiwa na kuwafikisha katika vyombo vya dola. 

Qolli alisema kupitia mafunzo hayo hifadhi ya jamii ya Burunge itakuwa na sura tofauti kwa ulinzi wa maslahi na mazingira ndani na nje ya hifadhi na kufanya uhifadhi shirikishi ili kushirikisha jamii katika uhifadhi kwa ujumla.

Alisema askari hao watadhibiti shughuli zote zinazoendeshwa ndani ya hifadhi ya Burunge na kuhakikisha kuwepo kwa manufaa makubwa kwa jamii na kuboresha utendaji kazi na kuwajali kimaslahi.

“Tunaamini mafunzo haya ni chachu ya kunusuru wanyama pori na tunatoa rai kwenu mkahamasishe jamii juu ya uhifadhi na kila mmoja kushiriki kuhakikisha kuwa Burunge inastawi vizuri na mapato yanaongezeka,” alisema Qolli

Hata hivyo, Mhifadhi utalii wa hifadhi ya Taifa ya Tarangire, Beatrice Kessy alisema mafunzo hayo yamewajengea uwezo zaidi askari hao 29 hivyo watayatumia kikamilifu katika kutimiza wajibu wao tofauti na hapo awali.Kessy alisema mafunzo kama hayo kwa askari hao 29 wa hifadhi ya jamii ya Burunge, yatafanyika kwenye hifadhi za jamii WMA za Ikoma wilayani Serengeti mkoani Mara, Mbomipa mkoani Iringa na Enduiment mkoani Kilimanjaro.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda