Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Thursday, October 17, 2013

AFYA KWANZA: Kwanini unapaswa kunywa maji mara kwa mara? Pata sababu hapa chini!

Na Mwandishi wetu

Kuna watu ambao katika maisha yao ya kila siku hawana tabia ya kunywa maji mara kwa mara . Hii ni kutokana na kuona kero ya kunywa maji kila wakati au kuona uvivu wa kubeba chupa za maji au kulazimika kufuata mahali ambapo maji yanapatikana lakini kubwa kuliko zote kati ya sababu hizo ni kutofahamu umuhimu wa kunywa maji mara kwa mara katika maisha na kwa afya ya mwanadamu.


Maji ni sehemu muhimu ya maisha ya mwanadamu na yana mchango mkubwa sana katika afya ya mwili na kama yakinywewa ipasavyo yanaweza kukuepusha na magonjwa mengi ambayo yatakufanya uishi maisha marefu .

Maji yanakufanya uendelee kuonekana mdogo
Maji yanafanya ngozi yako iwe na vimeleo au mabaki muhimu ya maji muda wote na hivyo kuondoa adha ya ngozi kuharibika kutokana na umri mkubwa . Maji kiasilia hurutubisha ngozi huku ikijazia mistari ambayo huondoa makunyanzi na kuifanya ionekane kuwa nyororo na laini.

Unywaji wa maji huondoa Msongo wa mawazo
Unaweza ukashindwa kuamini jinsi gani maji yana mchango kwenye afya ya saikolojia yako lakini ile sauti ya maji yakiwa yanachuruzika inaweza kutuliza mawazo yako na kuondoa msongo wa mawazo .

Maji yanasaidia kupunguza na kuponya mafua 
Unywaji wa maji husaidia kuondoa mafua kwa wale wenye matatizo na vumbi na uchafu na pia kunawa mikono mara kwa mara kwa maji masafi kunasaidia kuua vijidudu ambavyo huwafanya watu kupata mafua mara kwa mara .

Maji yanasaidia nywele                          
Kwa wale wadau wa masuala ya urembo hasa kina dada zaidi ya kuritubisha ngozi maji husaidia kung’arisha nywele . Kuosha nywele kwa maji ambayo hayajachemshwa kwa kutumia virutubisho vya nywele vya kutengeneza kama vile shampoo na mafuta maalum aina ya conditioner yanazifanya nywele kuwa thabiti zaidi na kuondoa uwezekano wa kung'oka hovyo hovyo huku zikiwa na mn’gao.

 Ngozi ya mwili husaidiwa sana na maji
Zaidi ya ngozi ya uso maji ni muhimu kwa ngozi ya mwili kwa ujumla . Wakati wa kuoga maji ya moto au vugu vugu hufanya ngozi ya mwili kuwa nyororo na yenye afya zaidi , maji husaidia kuondoa ukavu ambao huondoa mvuto wa asili wa ngozi na kuipa afya kwa ujumla.

 Maji husaidia kupunguza uzito wa mwili
Kwa wale wenye matatizo ya uzito wa mwili ambao wakati mwingine unaweza kuwa hatari kwa afya,  kwa kusababisha matatizo kama Presha, kisukari na magonjwa ya moyo, maji yanaweza kuwa kimbilio lako. Kwa mujibu wa utafiti , watu wazima wanaokunywa glasi nane za maji kwa siku yaani angalau glass mbili kwa kila baada ya saa kadhaa hasa kabla ya na wakati wa kula wanajikuta wakila chakula kidogo na hivyo kufanya mwili wako kupata chakula kile kile kinachohitajika na hivyo kuondoa uwezekano wa mwili wako kulimbikiza chakula kinachofanya uzito wako uendelee.

Maji huisaidia akili kufanya kazi vizuri
Mwili unapokosa maji tatizo pekee sio mtu kuhisi kiu  wakati mwingine ubongo huhisi kuchoka kirahisi na haraka pale ambapo mtu hajanywa maji muda mrefu . Hisia kama hasira , uchovu wa akili , kuchanganyikiwa humtokea mtu kirahisi wakati akiwa hajanywa maji muda mrefu na wakati mwingine hata kichwa huuuma sana lakini suluhisho la yote haya ni kunywa maji mara kwa mara .

Muwasho wa koo
Muwasho wa koo unaotokana na alegi (allergy) au mafua hutibiwa na maji , mtu anapopata tatizo hili suluhisho la haraka ni kusukutua maji yenye chumvi lakini kuepusha tatizo hili ni kuhakikisha koo halikauki kwa muda mrefu.

Maji husaidia kupigana dhidi ya magonjwa

Maji yana msaada mkubwa sana kwenye kupambana na magonjwa mwilini mwako . Ni vizuri kunywa maji mara kwa mara kuepusha mwili wako na magonjwa . Pia ulaji wa matunda husaidia kuupa mwili maji muhimu yanayokuwa kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali . Matunda kama mapapai,matikiti maji,matango,machungwa ,ndizi,maembe yanauongezea mwili maji ambayo yanakufanya ukae muda mrefu bila kuugua .

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda