Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Thursday, September 26, 2013

Tumerejea tena Mtandaoni

Habari za siku tele wapenzi wasomaji wetu. Awali ya yote tunapenda kuwaomba radhi kwa "kupotea hewani" kwa muda mrefu na hivyo kusababisha kukosa mambo kemkem ambayo mlikuwa mmeyazoea.
Kuadimika huko kulisababishwa na mambo kadha wa kadha, yaliyokuwa nje ya uwezo wetu na mengine ni sababu za kiufundi, lakini yote katika yote ilikuwa ni kujipanga na ujio mpya wa gazeti la Ohayoda ambalo lipo mitaani tokea mwishoni mwa mwezi June mwaka huu likiwa limesheheni mambo kede kede!
Hakika tumerejea kuwapa ile ladha ambayo wasomaji wetu popote ulimwenguni mmeizoea, yaani habari, matukio, makala na picha mbalimbali kutoka huku kwetu. Tulikuwa tumejikita kwenye jeshi la ardhini, sasa tumerudi kuitumia B52 tumalize kazi.
Kurejea huku kunakuwezesha kupata matukio na habari zote zinazoandikwa katika gazeti la Ohayoda na mengine mengi kila juma. Kwa kuanzia, tutaweka makala na habari na makala mbalimbali toka toleo la kwanza hadi sasa, ili kuwawezesha wasomaji wetu ambao hawakupata bahati ya kusoma gazeti waweze kupata utamu huo.
Unaweza pia kupata habari kupitia ukurasa wetu wa facebook kupitia www.facebook.com/ohayoda na kisha bofya like, hapo unaweza kushiriki mijadala na kuchangia au hata kushirikishana habari mbalimbali

Kama utaguswa na utapenda kutuunga mkono, tunapokea michango iwe ya maoni, fedha, habari, kiufundi, matangazo na mengineyo mengi ili tuweze kuwafikia wananchi wengi zaidi vijijini.

Kwa niaba ya Team Ohayoda, nawatakia usomaji mwema

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda