Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Tuesday, June 11, 2013

OHAYODA SASA LAJA GAZETINI

Hayawi hayawi sasa yamekuwa, ilianza kama ndoto lakini sasa inaenda kuwa Kweli! Lile gazeti la OHAYODA sasa litakuwa mitaani mwezi huu wa Juni 2013 tayari kuendeleza mapambano ya "nchi kavu" likisaidiana na Blog iliyokuwa ikitoa mashambulizi ya "angani"

Gazeti la Ohayoda litakuwa likitoka kila siku ya Alhamisi na litakuwa linapatikana katika maeneo ya Babati, Dareda, Magugu, Mto wa Mbu, Karatu, Arusha, Mbulu, Dongobesh, Haydom, Basotu, Qatesh, Singida, Nduguti, Hayderer, Maretadu, Endasak, Nangwa, Mang'ola na maeneo ya jirani na hayo.

Aidha, kwa wote wenye habari, matangazo au wanaopenda kuandika makala mbalimbali za kijamii, kiuchumi, kisiasa, mazingira na utamaduni wanakaribishwa ili kulifanya gazeti hili la kwanza kabisa katika mikoa ya Manyara na Singida liwe na mafanikio makubwa na kuchochea maendeleo.

Usisite, wasiliana nasi sasa kupitia
vantagedil@gmail.com au simu namba 0762395424

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda