Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Monday, May 6, 2013

Mwalimu Agnes Karengi afanya "Thanks Giving Party"

Katika ibada ya jumapili tarehe 5 Mei 2013, mwalimu Agnes Karengi akisindikizwa na familia yake pamoja na ndugu, jamaa na marafiki kutoa shukrani kwa kumaliza muda wake wa utumishi baada ya kuitumikia nchi kwa utumishi uliotukuka kuanzia mwaka 1976 hadi mwezi Novemba mwaka 2012 alipostaafu akiwa na miaka 60.

Baada ya ibada iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) usharika wa Haydom, hafla fupi ilifuatia ambapo kwaya za Upendo na Umoja zilihudumu nyumbani kwake katika kitongoji cha Qaway mjini Haydom huku kukiwa na "makulaji kidekede".

Mwalimu Agnes Karengi alianza utumishi wake mwaka 1976 ambapo alifundisha shule ya Msingi Mewadan kabla ya kuhamishiwa shule ya msingi Harar ambako alifundisha hadi mwaka 1980 alipohamishiwa shule ya msingi Haydom ambako alifundisha hadi alipostaafu mwaka 2012 akiwa na umri wa miaka 60.

Mwalimu huyu ambaye "ametoa ujinga" wa wengi hapa Haydom, kwa muda wa miaka 32 amekuwa mwalimu wa darasa la kwanza hivyo kuwa kipenzi cha watu wengi waliopata bahati ya kusoma shule ya msingi Haydom. Wengi wanamkumbuka kwa "viboko vyake" hasa akina Goodluck Membi, Dr. Fanuel Bellet, Mary Mkony, Dr. Filemon Joshua, Neema Isaack, Daudi Mayyega na wengine wengi ambao walisoma shule hii iliyopo mitaa ya Gangay.

Kama kawaida, kamera ya Ohayoda ilikwepo eneo la tukio na imeweza kunyaka matukio kadha wa kadha
Mwalimu Karengi akiwa na moja wa kina mama waliojumuika naye

Mwalimu Hellena Massay Kushoto akiwa na Mwalimu Kivaria Msuya. Mwl Massay alikuwa mwanafunzi wa Mwl Karengi na kisha kufanya kazi pamoja. 


Dr. Peter Mnyau akiwa na......walipowasili kwa usafiri wao

Kwaya ya Umoja ikiwasili nyumbani ikiongozwa na Editha Lottoa, Samuel wa Posta na Mama Noah genda

Wakati wa Maakuli

Blogger nilikuwepo eneo la tukio

Kila mtu akawa "busy" na sahani na "soda"..chezea kitu cha ubwabwa wewe?

Kwaya ya Upendo ikiongozwa na Mama Naman na mama Mary

Kwa mbali kulia namwona mama Mchungaji na kushoto kabisa ni Lighty..wengine blogger hakuweza kuwafahamu lakini wote ni wanakwaya wa kwaya ya Umoja

Hiki kikosi kiliongozwa na George wa Bariki

Madakitari Philemon na Peter...

Picha ya pamoja na Kwaya ya Upendo.... Huyu jamaa (kulia kabisa) huwa ananifurahisha sana maana ni kijana pekee na mwaaume pekee anayeimba kwenye hii kwaya inayoundwa na kina mama "walioenda umri"

Mama Mzazi wa Mwalimu Karengi....kisia umri wake kama unaweza

Kwaya ya Umoja nayo ikatumbuiza naye akaunga "tela"

Babu Noah Genda naye hakuwa nyuma kumkaribisha Mwalimu uzeeni

Hii ndo picha ya Siku ya jana....Shughuli haijakamilika bila kupiga ubwabwa wa kutosha

Bibi na wajukuu

Vitukuu

Mama na Mwana

Ohayoda inamtakia mwalimu Agnes Karengi mafanikio na furaha tele katika maisha mapya aliyoyaanza rasmi!

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda