Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Monday, May 6, 2013

HAIJAWAHI KUTOKEA HAYDOM: 4CCP na TTB kutoa mafunzo kwa watoa huduma na waongoza watalii Haydom

Kwa mara ya kwanza katika Historia ya Haydom na vitongoji vyake, Bodi ya Utalii yanzania (Tanzania Tourist Bord-TTB) kwa kushirikiana na Programu ya Pembe Nne za Utamaduni Haydom (Four Corners Cultural Programme-H4CCP) wameandaa mafunzo kwa watoa huduma mbalimbali na waongoza watalii walioko haydom ili kuboresha ubora wa huduma hizo na kufikia viwango vinavyotakikana na soko

Akizungumza na Ohayoda, mratibu wa programu ya Utalii wa Utamadani kutoka TTB Bwana Elirehema Maturo alisema kuwa, Kuna vivutio vingi sana vya utalii vilivyopo Haydom na karibu na maeneo ya jirani na kutoa fursa mbalimbali za kiuchumi hasa utalii wa utamaduni lakini hali ya ubora wa huduma inayotolewa na watoa huduma mbalimbali wa Haydom ni vya kiwango cha chini sana.

"Kuna vivutio vingi sana Haydom, lakini watoa huduma hasa za vyakula na nyumba za wageni bado hawakidhi viwango" alisema Maturo.

Walengwa wa Mafunzo hayo ni wafanyabiashara hasa wanaotoa huduma za vyakula, nyumba za wageni, maduka, waongoza watalii na wanaopenda kuwa waongoza watalii, wazalishaji, Taasisi zinazopenda kuboresha huduma zake kwa kuwapa mafunzo wafanyakazi wake na hata watu binafsi wanaopenda kuongeza ujuzi.

Mafunzo haya yatatolewa bure kabisa na ratiba ya mafunzo haya imetolewa (soma Tangazo chini ya habari hii).

Kwa wanaopenda kushiriki mafunzo haya wajiandikishe katika Ofisi za 4CCP zilizopo katika Kituo cha Utamaduni Haydom (mlimani) na ndani ya Hospitali ya Kilutheri Haydom (HLH) kabla ya Ijumaa tarehe 10 Mei 2013 au wasiliana kwa simu namba 0784238225

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda