Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Sunday, April 28, 2013

Redds Miss Haydom 2013: Eliwakembeta a.k.a Sharon amrithi Agnes Michael

Hatimaye Agnes Michael (Redds Miss Haydom 2012) amepata mrithi wa kiti chake baada ya Eliwakembeta Samwel maarufu kama Sharon kuibuka kidedea katika king'ang'anyiro cha kumsaka mlimbwende wa Haydom akiwabwaga chini washiriki wengine 7 katika shindano lililofanyika katika ukumbi wa CCM mjini Haydom Ijumaa tarehe 26 Aprili 2013.

Kwa Ushindi huu, Eliwakembweta anaingia kwenye rekodi ya kuwa mlimbwende wa pili kutwaa taji hilo baada ya Agnes Michael kutwaa taji hilo wakati shindano hilo lilipofanyika kwa mara ya kwanza hapa Haydom. Eliwakembweta amejishindia fedha taslimu shilingi laki moja na zawadi kedekede ikiwemo doti tatu za vitenge vya "waksi"

Katika Shindano hilo, Sarah Balanga alitwaa taji la Haydom Redds Miss Talent 2013 na kumrithi Lucy Stephano aliyetwaa taji hilo mwaka jana na kufanikiwa kuwa mshindi wa pili (First Runner-up) na Lightness akaibuka mshindi wa Tatu (Second runner-Up)

Shindano hilo lililoandaliwa na kampuni ya FMR Entertainment chini ya Mkurugenzi wake Bwana Sinjela na Meneja wake Bwana Babuu ambapo burudani kali iliporomoshwa na kundi la Platinums na kudhamini Familia ya Patty wa Hamandos huku warembo wakiandaliwa na Lucy Stephano aliyekuwa Miss Haydom No.2 mwaka 2012 ambaye pia anashikilia taji la mrembo mwenye mvuto zaidi katika picha nchini Tanzania yaani Redds Miss Photogenic Tanzania mwaka 2012 huku Baby wa Kiwi Salon Haydom akiwa ndiye aliyewapamba warembo.
Pata Uhondo kamili katika picha......
Mshindi wa tatu Lightness (Kushoto) na mshindi wa Pili ambaye pia alishinda tuzo ya Haydom Miss Talent 2013 Sarah Balanga (Kulia)

Vijana wa Platinumz wakivunja vitu jukwaani

Sharon (Mwenye No 1) baada ya kutangazwa Mshindi, Kulia ni Sarah na Lightness (kushoto)

Sharon akiwa na furaha baada ya kushinda

Miss Haydom No. 2 2012 Lucy Stephano ambaye pia anashikilia taji la Miss Mbulu, Miss Manyara No 3, Miss Northern Zone na Redds Miss Photogenic Tanzania 2012 Lucy Stephano (Kulia= akipanda jukwaani akiwa na Miss Haydom 2012 Agnes Michael tayari kukabidhi mataji kwa washindi wapya

Agnes Michael kabla ya Kukabidhi taji kwa Sharon Samuel


Sharon akiwafurahi baada ya kuvikwa taji la Miss Haydom 2013


Mkuu wa Kituo cha Polisi Haydom OCS Mfero (wa pili kulia) akikabidhi zawadi kwa Sharon baada ya kutangazwa Mshindi, kushoto ni Meneja wa FMR Entertainment Mr. Babuu

Washiriki wa Redds Miss Haydom 2013 wakiwa katika picha ya pamoja baada ya Sharon Kutangazwa Mshindi

Je Sharon ataweza kufuata nyayo za Lucy Stephano? Tuvute Subira....Picha zaidi za matukio yaliyotukia usiache kusoma Ohayoda.

2 comments:

  1. WOW!!!
    Contratulations to miss haydom 2013 Sharon (Eli) you are beautiful hun and im sure you will win miss mbulu pia! Congratz ones again, as well as this to all those women who participated you all look amazing and beautiful :)

    ReplyDelete
  2. Hivi vitu na Huko kwetu vimefika lini ?

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda