Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Monday, March 4, 2013

PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI YA SIKU YA "4CCP-SHOW YOUR TALENTS COMPETITION".......

Na Nelson Faustin.
Vijana wetu wana mambo mengi mazuri sana, wakipata nafasi ya kuonesha mengi waliyonayo na kwa mwongozo sahihi wa jinsi ya kutumia vipaji vyao vizuri, tunaamini tutakuwa na kizazi endelevu na chenye manufaa kwa taifa na kwa jamii kwa ujumla ndani ya ulimwengu huu wa "it is only the strongest shall survive in this capitalist world". Jumamosi hii ya 2nd March 2013, wanafunzi wanaosoma katiak shule zinazozunguka eneo hili la haydom walipata nafasi ya kuonesha vipaji vya kila aina na wengi wao walionesha uwezo wa hali ya juu, hii ina maana kwamba, kama waliweza kufanya haya yote ina maana hata kitaaluma waweza kufanya makubwa zaidi ya haya.

Meza kuu ikifuatilia mchakato mzima kwa karibu, Wa kwanza kulia safu ya nyuma ni 4ccp co-ordinator, Mama Eliminata Awet.
Nelson, Program Organizer&Mc, Ni kawa na mengi ya kusema, Lazima kieleweke kwa vijana hawa.

Huyu dogo kutoka shule ya sekondari Haydom alikuwa "akichana" mistari balaa.

Kwaya ys Shule ya Mama Kari, ilinikumbusha mbali sana enzi za kutoa saluti kwa meza kuu

Fashion Show kutoka shule ya sekondari Dr. Olsen ilifunika mbayaaaaa

Fashion Show....."mamodo" walitokelezea katika mavazi tofauti...kuanzia vazi la Kanisani, Msikitini, Ofisini, vazi la Mkulima, daktari, vazi la mwanafunzi na vazi la ubunifu la kanga, vazi la casual, mavazi ya vijana wa kisasa..kisharobaro n.k

Vipaji vya maigizo navyo vikachukua mkondo wake....

Huyu dogo alikuwa amepiga skafu ya kile chama cha watuuuuuuuuuuuuuz! Yeye na kundi lake walichana mistari ni balaaje?

Nani kakwambia huku hakuna "acrobatics? Sarakasi zilibambaaje?

Mwl. Mbaga wa Dr. Olsen akiwa na vijana wake wa Sarakasi

Nancy naye si akachukua Mic?....utadhani Whitney Houston

Mama Kari wao wakaja na Ngoma ya Kiiraqw
Dance group la Form 6 Dr. Olsen Secondary School

Amani akasema mawili matatu kwa wanafunzi waliokuwepo. Kwa kifupi siku hii ilibamba sana. 

KIFUATACHO.....TAREHE 16 MARCH WANAFUNZI HAO WATAKUTANA TENA KWA WORKSHOP..........

1 comment:

  1. maaaaamaaaa miaa.. Brilliant work..
    loved it...

    That is all I can say for now.

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda