Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Tuesday, March 19, 2013

Papaa On Tuesday.....Kujilaumu Bila Kuchukua Hatua Hakujawahi Kumsaidia Mtu.


Kama haujawahi Kujilaumu kwenye maisha yako basi umewahi kulaumiwa, lawama is unkwepable hazikwepeki, kuna wengine kila siku wanalaumiwa wao, na kuna wengine kila siku wanalaumu wao, na kuna wengine wanalaumiana wenyewe kwa wenyewe. Hakuna Lawama inayokuja bila sikitiko kwenye maisha, Lawama ni Kujuta, na Lawama inaondoa uwajibikaji kwa mlaumu ana kutaka upande unaolaumiwa uone kabisa jinsi ambavyo umepelekea mambo yawe ndivyo sivyo.

Ukiona watu wanakulaumu ujue wanataka ua-admit kuwa ukubali umepelekea kwa namna moja ama nyingine lililokusudiwa lisipatikane, ukiona kuna lawama ujue matarajio ya watu hayajafikiwa, ukiona kuna pongezi ujue Mr. Lawama kaenda likizo kwa muda. Usipopata pongezi ujue utapata lawama haya ni maisha yetu ya kila siku. Watanzania kwa ujumla tumekuwa tukiilaumu Serikali kwa kushindwa kuwapa Maisha Bora Kila Mtanzania, Kuna watu wamekuwa wakiwalaumu wazazi wao kuwa yamkini isingekuwa kutoka familia fulani nisingekuwa hivi nilivyo, yamkini kuna wanafunzi wamekuwa wakiwalaumu walimu wao kushindwa kuwasaidia kufika wanakotaka kufika, kuna wanandoa ambao kila siku, kila mwezi lazim mmoja alaumiwe kwa kuzorotesha mapenzi ndani ya nyumba, wapenzi wapya nao wanalaumiana kwa kila mtu ku demand mabadiliko ili kuboresha mahusiano, maderava wanalaumu barabara za mijini kusababisha foleni, Waumini wanalalamikia Wachungaji wao kwa kuwa nyuma ya maendeleo, Waajiriwa wanawalaumu Waajiri kwa ajili ya mishahara midogo, ajabu sana Ofisini wewe unalalamika kuwa maisha magumu, Ukienda nyumbani na wewe unalalamikiwa mambo hayaendi kila mtu analaumu, lawama hazikwepeki kuna maeneo mengi sana lawama zimejaa, maana hata walimu na madaktari wanalaumiwa pia.

Lawama ina stage nyingine inaitwa kujilaumu, ukilaumiwa na watu utasikitika na utatiwa moyo wakati mwingine utaomba na msamaha mambo yataisha na yataendelea, ila kinachotesa sana watu ni Kujilaumu. Kujilaumu huwa kuna kuja hasa kama tarajio la jambo lilikuwa juu kuliko uhalisia, ama mambo yanapokuwa sivyo ulivyotarajia na uamuzi uliufanya wewe mwenyewe unabaki hauna wa kumlaumu unabaki kujilaumua ama unaye wa kumlaumu na kwa sehemu na wewe unako ka sehemu ka kujilaumu kwa maamuzi uliyowahi yafanya kwenye maisha. Kuna mtu ninamfahamu aliwahi acha kazi mahali fulani baada ya kusikia tetesi kampuni inafilisika akaamua kwenda sehemu nyingine baada ya kupata ahadi kede kede alipokwenda kule baada ya miezi sita mambo yakaanza kwenda sivyo kwenye kampuni mpya na kule alikotoka mambo yakaanza kunyoka, kurudi anatamani lakini aliondoka na mbwembwe nyingi sana alibaki kujilaumu kwa kile kilichotokea, kuna watu wengi sana wanajilaumu namna ambavyo wamekuwa wakitumia hela vibaya wamekuwa na akili sana wakiwa hawana fedha wanaandaa na bajeti kabisa kasheshe inakuja akishashika hela anajikuta mambo ya msingi hafanya na yale yasiyoyamsingi ndo umeyafanya kwa kiwango cha juu kabisa mwisho wa siku unabaki kujilaumu.
 

Mara kadhaa nimekutana na watu ambao wanajilaumu tabia zao mpaka wanajichukia, kuna watu wametamani sana kubadilika kwenye maisha yao wengine wamejikuta mara kadhaa wanafanya mambo ya aibu na yasiyofaa matokeo yake ndani ya mioyo yao wamebaki kujilaumu kwa kile kinachokifanya. Kuna watu wanajilaumu sana kwa makosa yao waliyowahi fanya zamani, wanajilaumu kwa makosa waliyoyafanya na kupelekea wengine kupata watoto wa mapema, kuna wengine wanajilaumu kwa masomo yao waliyoyasoma baada ya muda sasa wamegundua walisoma kitu ambacho kinawakosesha kupiga hatua.
Kuna wengine wanajilaumu kwa sababu ya Ndoa walizonazo kwao siku za furaha ni nyingi kuliko majonzi, wanasema laiti kama ningejua nisingekubali na inauma zaidi iwapo alishauriwa lakini akakomalia sasa anakosa wa kumlaumu anabaki kujilaumu mwenyewe, wengine wanajilaumu kwa makosa yao yaliyopelekea pengine kuachwa na wapenzi wao, kuna rafiki yangu mmoja alikuwa na mchumba mzuri sana siku moja huyu jamaa akafumaniwa na mpenzi wake akifanya mapenzi na mfanyakazi wa ndani anayewasaidia kufanya usafi nyumbani kwa huyu mkaka, mdada akaamua kumuacha mpaka kesho jamaa anajilaumu sana kwa kosa alilolifanya limemwachia simanzi badala ya furaha. wengine wanajilaumu kwa uzembe waliowahi ufanya hapo zamani na kupelekea maisha waliyonayo sasa, maisha yetu yajayo yanategemea sana maamuzi yetu ya leo.

Ukweli wa mambo ulivyo Lawama au Kujilaumu hakujawahi msaidia mtu, unafanya nini baada ya kugundua kosa na kujilaumu, wengine wamedumu katika hali walizonazo na wengine kupoteza furaha sababu bado kila wakikumbuka na kujilaumu machozi yanawatoka, wanakuwa wagonjwa na wengine pressure zinapanda ama kushuka. Utaendelea kulaumua ama kujilaumu mpaka lini??kujilaumu ama Kulaumu hakutabadilisha hali halisi ya kilichopo ama kilichokuwapo hapo awali ni lazima uchukue hatua ya kuelekea kwenye mabadiliko ya akili yako nafsi yako na moyo wako na mwili wako utambue kuwa kubweteka na lawama hakuna msaada. Kama kuna jambo linalohitaji kusamehe samehe and let it go, kama ni suala la kuanza kutendea kazi anza kutendea kazi, kama ni suala linalohitaji elimu tafuta namna ya kupata hiyo elimu. 
 
Wewe ndiye unayewajibika na maisha yako na furaha ya maisha yako. Mwombe Mungu akusaidie yeye ndiye mweza wa wote. Biblia inasema Njooni Kwani Ninyi Nyote wenye kulemewa na mizigo nami nitawapumzisha. Wanaoitwa kwenda kupumzishwa ni waliolemewa, kama hujalemewa usimcheke aliyelemewa mzigo wake umekuwa mzito kuliko nguvu alizonazo na Ukishapumzika si utapata nguvu kuna Possibility kubwa sana ukaendelea kubeba mzigo wako mpaka utakapokulemea tena. Kama ni jambo linalohitaji Ushauri usife na tai shingoni, usitake uonekane kuwa mambo ni safi wakati unaweza pata msaada kutoka kwa watu wanaoweza kukusaidia. Dunia Yako Ndio Chaguo lako.


Kujilaumu na Kulaumu hakutakupa Suluhu ya tatizo lililopo isipokuwa hatua unayochukua baada ya hapo ndio inayoweza kuleta mabadiliko na mafanikio katika maisha. 
Think Differently and Make a difference.
Papaa On Tuesday Imekujuia Kwa Hisani Kubwa Kabisa Ya

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda