Ninakila
sababu ya Kumshukuru Mungu kwa siku ya leo kwa kuweza kunipa nafasi hii
muhimu kuongea na Marafiki kwa njia hii ya Fasihi Andishi. Wakati
Tukisubiri Matokeo Ya Uchaguzi Kenya Basi Ipo haja ya Kujifunza Kutoka
kwa wenzetu katika Kile Wanacho Kifanya.
Najua
wengine ni kizazi cha dot com hapa hawajasoma methali wala hawajui
tafsiri zake, lakini wengi pia Watoto wa Mahospitalini utajulia wapi
mambo ya maneno kama Wakunga??Leo nataka tuongelee methali hii ya
"Usitukane Wakunga Wakati Uzazi Ungalipo". Kwanza Kutukana ni kuongea
maneno machafu, kuongea maneno mabaya, maneno ya dharau kwa Wakunga.
Wakunga ni Watu waliokuwa Wakiwasaidia Wanawake wakati wa kujifungua
kipindi hicho zama hizo kabla ya hospitali zetu, sikuhizi tunasema
Wakunga wa Jadi, na Wakunga wa laptop. Neno Uzazi Ungalipo ilikuwa ni
kama nahau ya kueleza kuwa hicho kitu unachokidharu leo utakihitaji tena
siku nyingine, huu ni uhitaji endelevu. Maana hasa ya Methali hii
ilikuwa kutoa fundisho kuwa Leo Hii wewe ni Mjamzito, Kisha Unawatukana
Wale wanaokusaidia Kuzaa, Unasahau kuwa kesho na Kesho kutwa utashika
mimba tena wale wale uliowatukana siku za nyuma unakutana nao tena uso
kwa uso.

Mojawapo
ya mambo yanayodhihirisha tabia ya mtu ni kuwa "Pesa", Mhe. Chenge
anaita Vijisenti. Kuna maneno mengi sana yametungwa kuhusiana na fedha,
Biblia inasema Fedha ni Jawabu la Mambo yote, Fedha ni Sabuni ya roho,
Kwenye udhia ingiza rupia, hii yote ni kuonesha namna gani fedha inaweza
badilisha uchafu wa roho ya mtu.
Kwenye
Kizazi chetu fedha inakupa nafasi hata katikati ya Vijana wenzio, fedha
inakuletea marafiki na wanafiki, fedha inakufanya uitwe Handsome au
sweetybaby hata kama haufananii hayo, fedha imewavulisha nguo Wake za
watu na waume za watu, fedha imepelekea Maaskofu na Maimam kuchukuiana,
wengi wetu tumebadilika pale tunapotoka hatua moja ya mafanikio kwenda
hatua nyingine.

Dharau
kwetu iko karibu kuliko heshima, pale mtu anapoanza kupata mafanikio.
Kuna watu tumecheza nao, tumesoma nao, tulikuwa pamoja, kama ni Wanandoa
Walipendana wakiwa hawana kitu, mafanikio yalipoingia tu kwenye ndoa,
unakuta mmoja anabadilika na kumlaumu mwenzake kuwa ndo kapuku wa
kutupa. Kuna watu waliwahi pata kazi kwenye Ofisi moja wakaondoka kwa
dharau na makelele wakisema Ofisi hiyo wote ni Walugaluga, hawana mbele
wala nyuma, ndugu yangu usinyee kambi, siku adui akikupiga ukashindwa
kurudi.
Hivi
kwanini umadharau mtu eti sababu wewe umepiga hatua mbele na wenzio
umewaacha nyuma, kuna mdada alimpenda Mpenzi wake ambaye alikuwa si
lolote wala si chochote, huyu mdada akampenda, akamkazania arudi shule
akasoma, mdada akamtafutia mkaka pa kukaa, baadae akatamani mtu wake
ajitegemee akamtafutia na kazi, siku zote huyu kaka alionesha mapenzi ya
hali ya juu kwa huyu mdada, alipoaanza kazi akajua kuvaa tai, akajua
nini maana ya Salary Slip, akajua nini nguvu ya Mshahara huyu Jamaa
akaanza ku change, mara busy na kazi, mara kasafiri kikazi, ghafla
dharau zikaingia kisa anamshahara mkubwa kuliko wa huyo dada, akaanza
matusi kuwa eti mdada ana bahati kuwa na yeye, yeye ni level zingine, na
huyu mdada si standard yake, dharau kebe wa kebe, mwisho wa siku Mkaka
akamwambia mdada unataka nikulipe shilingi ngapi kwa fadhira zako ili
kila mtu aende na maisha yake, maana amegundua Mdada sio type yake, tehe
tehe ulisikia wapi Fadhira inalipwa Dharau, Uliwahi sikia Wema Unalipwa
na Matarumbeta??Akatukana Wakunga Wakati Bado anajua kesho atashika
tena Mimba ya Maisha.

Yule
Mdada hakutaka kulipwa chochote aliumia akaumia akalia na kulia mpaka
akakonda sababu ya maneno ya mtu mbaye amemsaidia kutoka mahala pa chini
sana, Mungu sio Filikunjombe, Jamaa sababu ya tamaa ya fedha akawa
anaiba ofisini, ghafla ikajulikana Vijana wa mjini wanasema "Kikanuka"
tena kwa harufu ya choo cha uswazi, akafukuzwa kazi, Mwanawane wale
wooote aliokuwa aliokuwa anadhani ndo type yake wakamkimbia, kama story
ya Mwanampotevu Kijana akazingatia moyoni mwake akaona arudi kwa mdada,
ha ha ha ha wakati we unasema "Cha Nini, Wenzio Wanasema Watapata Lini"
mdada alishaolewa zake zamaniiii, Kijana akarudi Kitaa full adabu, kisa
na Mkasa anatukana Wakunga.
Ukipata
fedha usidharau watu ukajiona wewe ni bora kuliko wasiokuwa nazo,
Ukipata nafasi ya kusoma na usiwaone wale wasiosoma sio kitu, hata kama
ni Wazazi wako, huwezi kujifanya wewe ndo wewe ukawaambia Wazazi wako
hawajaenda shule, kumbuka walinyima wewe uende shule, unapata Mshahara
Unakula wote, kisa mshahara hautoshi, kawa taarifa yako hata wao ulikuwa
haitoshi lakini walijipinda usome unaona Kero ukipewa matatizo ya home
itakula kwako, we tukana wakunga kimoyo moyo kuwa "wamezidi". Ukipata
Mchumba au hata Boyfriend ama Girl Friend basi usijione wewe
ndo Beautiful kuliko Cleopatra, unawaona wenzio wasiopata watu ni
"Magume gume". Ukiolewa wenzio wakikosa bahati usianze nyodo "Siongei na
Wasio na Ndoa", Ukipata kazi sehemu nyingi bora kuliko hapo ulipo,
usiondoke na mbwembwe za matarumbeta, hii dunia bwana huwezi jua.

Dharau
haziwezi kutupeleka mahali popote, unayemdharau leo hujui kesho yake
itakuaje, hapa ni duniani na malipo ni hapa hapa unachopanda ndicho
utakachovuana, mbwembwe na majigambo ni utoto wa hali ya Juu ukikua
utaacha, Sasa kwanini kufanya dharau sababu ya mafanikio
yasiyodumu??hukuwahi sikia ama kuona watu waliokuwa na nyodo na mbwembwe
wazazi wao wakiwa hai ghafla wazazi wakafaraki??hukuwahi sikia watu
waliokuwa wanafanya mbwembwe na kufuru sababu ya wapenzi wao ghafla
kikaumana??hujawahi sikia mtu aliondoka kwenye ofisi moja kwa mbwembwe
huko alikokwenda kikanuka??
Yangu mimi ni macho, ninarudia kusema
Usitukane Wakunga Wakati Uzazi Ungalipo.
Think Differently Make A Difference
Papaa0713 494110
No comments:
Post a Comment