Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Friday, March 1, 2013

Kama Haujawahi kufanya maamuzi magumu maishani, bado haujakua vizuri

Nimewaza tu: Nadhani wakati Nyerere anaacha kazi ya ualimu ambayo kwa wakati ule naamini ilikuwa inamlipa sana na kuamua kuingia kwenye siasa ambayo hakuwa na "security" yoyote, marafiki, ndugu na hata watu baki walimshangaa na kumcheka. Lakini alikuwa na "ndoto" kubwa zaidi ya hiyo "security" ambayo kila mtu wa kawaida (average person) anaitafuta. Angeweza kuridhika na kazi aliyokuwa nayo na kuamua kuwanyenyekea wazungu apande cheo taratibu ili alipwe vizuri lakini yeye alikuwa na mawazo tofauti...ya kuikomboa nchi. Miaka 7 alihaha, naamini kuna wakati alipiga dash kibao kwa sababu harakati za kudai uhuru hazikuwa na ruzuku kama hizi za akina Dr. Slaa ambazo pia hupewa fedha kutoka nje na wafadhili wengine zaidi walitegemea ukarimu wa watu kuwapa chakula na fedha kiduchu!

Kama ilivyokuwa kwa Nyerere, Musa naye akaondoka nyumbani kwa farao, akaishi miaka 40 porini akichunga kondoo na mbuzi. Nadhani kwa muda wote huo Musa alikwisha kusahau kuwa anaweza tena kuwatoa waisraeli kutoka makucha ya Wamisri, lakini kilichotokea baada ya hapo wanasema "ni historia"


Yusufu naye alikuwa na ndoto kuwa mtawala na kuwa siku moja ndugu zake watapiga magoti kumzunguka. Miaka ikakatika na ndoto ikageuka kuwa "nightmares", badala ya kuwa boss anauzwa na kuwa mtumwa. Na hata alipopanda cheo kidogo na kuwa bosi wa watumwa wenzake pale kwa Potifa, akabambikiwa kesi ya ubakaji na kuishia gerezani. Nadhani alipofika hapo ndoto zote zikayeyuka kama barafu juani lakini aliyoyapitia yalimfanya kupata uzoefu, akawa Waziri Mkuu tena katika nchi ya utumwa na wakaja ndugu zake kumsujudu! Ndoto haifi japo katika hali ya kibinadamu inaweza kukawia lakini wakati wa Mungu ukiwadia, hata viwekwe vigikwazo vya NATO na UN lazima kila kitu kitimie!

Mbegu ili iote ni lazima ioze kwanza, ife ndipo itaota. Usitarajie kufikia ndoto yako (Hasa kama imetoka kwa Mungu) kirahisi, lazima ufanye maamuzi magumu, mengine magumu zaidi ya ufahamu wa akili za kawaida tena kinyume na matarajio ya wengi hasa watu ulio karibu nao. Rafiki yangu Samuel Sasali aliwahi kusema ili uruke juu zaidi yakupasa ushuke chini zaidi, kama ilivyo ukitaka kujenga ghorofa refu zaidi, nili lazima uchimbe chini zaidi....you can not reach greatness without sacrifices!
Ujumbe huu ni kwa wale wachache wenye ndoto za kufanya vitu tofauti na wale wanaofanya maamuzi magumu kila mara!
Salamu ziwafikie Mathew MndemeProsper Alfred MwakitalimaBaba XtinaBernie MponejaJohn Mnyika na woooote ambao hu...Think differently and make a difference!

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda