Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Monday, March 4, 2013

"Haydom 4ccp-Champion Club", Tumeanza, Tunakua, Tunaandaa Kizazi "Kombozi".Sir Nelly, Kikazi zaidi.
Ilianza kama ndoto, Ndoto ambayo ilipaswa kuwa kweli na kwa Neema za Mungu imekuwa kweli. Tarehe 8 September mwaka 2012 tulifanya mkutano/semina ya kwanza ya wanafunzi/vijana ambayo ilikua na lengo la kuwasaidia vijana kataka maswala mbalimbali.

 4CCP ilipokea kwa mikono miwili hitaji la kuwa na programu maalumu ya vijana na wanafunzi, programu ambayo itasaidia katika kuwafikia wanafunzi na vijana ambao kwa namna Haydom ilivyo ni eneo ambalo kwa namna moja au nyingine licha ya kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi ambao ni taifa la kesho kuna changamoto mbalimbali za kimazingira na kwa sababu hiyo kuna "clues" za muhimu sana kuhusu maisha ya kitaaluma na kujipanga kimaisha wanafunzi hawa wanahitaji ili waweze kupambana na changamoto zilizopo duniani ambazo zinabadilika siku baada ya siku na zinatarajiwa kuwa kubwa zaidi kadiri ya miaka inavyokwenda mbele.
Jopo la Majaji wakifuatilia Mashindano kwa makini.,
Jumamosi ya tarehe 2/3/2013 tulifanya mkutuano wa nne ambao ulipewa jina la "4ccp-Champion Meeting 2013 Season II, Show Your Talents Concert Phase I". Katika tukio hili, zaidi ya wanafunzi 500 kutoka katika shule za sekondari Dr.Olsen, Mama Kari na Haydom walikutana katika ukumbi wa mikutano wa 4ccp-Pavillion uliopo eneo la "Cultural centre" katika mashindano maalumu ya kuonesha vipaji mbalimbali shindano linaloratibiwa na 4ccp.
Mratibu 4ccp akiongea na vijana.
Team ya 4CCP ikishirikiana bega kwa bega na walimu pamoja na wadau mbalimbali tulifanikiwa kuwakutanisha wanafunzi na zaidi ya vikundi 30 kutoka katika shule zote tatu vilifanya mambo ya kutisha.

Katika mashindano haya ambayo yanatarajiwa kuendelea tena mwezi wa tano na kufikia kilele chake mwezi wa tisa mwaka huu wakati wa tamasha la pili la utamaduni Haydom (2nd 4ccp-HCF). Vipaji mbalimbali vilishuhudiwa kama vile, kuimba, maigizo, comedy, uchoraji, dance, sarakasi, actionary, handcraft, rap, kutunga na kuimba mashari, ngoja za utamaduni, fashion show and designing, taarabu na vibwagizo vinginevyo vingi.


Ni hatua kubwa sana kwa 4ccp na kwa haydom kwa ujumla kwani ni programu ambayo inaonekana kuwa msaada mkubwa sana kwa vijana na kwa maono tuliyonayo tuntarajia kufika shule nyingi sana za mkoa wa Manyara zikiwemo na za msingi pamoja na vyuo mbalimbali.

Wanafunzi wa Mama Kari secondary School.


Let's Dance.......
Lengo la kuwa na programu hii ni katiaka kuleta hamasa ya taaluma miongoni mwa wanajamii huku tukiweka macho na masikio yetu kwa taifa hili chipukizi. Katika programu hii tunatarajia kuwa mambo mbalimbali kama vile kuleta mahusiano mazuri ya dini mbalimbali, kuinua mawazo ya ki-jariamali, kuwajengea wanafunzi mawazo ya kizalendo zaidi,nk. 

Tunatarajia kuwa na wasemaji mbalimbali kama vile kina Chris Mauki, Sam sasali, Rose Mushi, Prosper Mwakitalima  na wengineo wengi ambao kila mwezi watakuwa wakiwasha moto ndani ya dhamira na akili za taifa hili chipikizi ili kuokoa taifa la Tanzanzania kwa miaonogo michache ijayo. 

Sisi tunafanya huku tulipo, wewe Je????????
Tusakasarike best.....
Kila mmoja ana wajibu wa kuandaa taifa hili chipukizi, shukrani za dhati kwa familiya ya 4ccp, uongozi wa shule ya sekondai Haydom, sekondari ya DR. Olsen na Mama Kari secondary School, viongozi wa kiroho na wadau wote, bila kuwasahau wanafunzi ambao bila kusita wanapokea kwa mikono miwili programu hii kwa kushiriki kikamilifu, Mkutano mwingine utakuwa tarehe 16 March mwka huu ambapo tunatarajia kuwa maandalizi ya essay competition......

I am because you are-4ccp

By Nelson Faustine-Program Organizer....
Karibu Haydom...........

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda