Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Tuesday, February 12, 2013

Renata Kawala: Mrithi wa akina Filbert Bayi anayefanya vizuri nchini New Zealand

 Hadi miaka ya mwanzo ya 2000, mkoa wa Manyara (enzi hizo Arusha) ulisifika kwa kutoa wanamichezo maarufu hususani katika riadha ambao waliiletea nchi yetu heshima kubwa sana kimataifa na kushindana bega kwa bega na wanariadha kutoka Kenya na Ethiopia. Toka kizazi cha akina John Steven Akhwari, Filbert Bayi, Gidamis Shahanga, Francis Naali na Zebedayo Bayo kipite, mchezo wa riadha umekuwa ukishuka kwa kasi ya ajabu na tumekuwa wasindikizaji katika michezo ya kimataifa hasa Olimpiki na ile ya Jumuiya ya Madola.
Katika mashindano ya U16 Ranata Kawala (kulia) alishinda mbio za 800m na kuruka chini(Picha kwa hisani ya gazeti la Marlborough, February 18 2012)
  Kinachosikitisha zaidi ni kitendo cha michezo kufutwa mashuleni na kusababisha hamasa ya michezo kufa huku mamlaka husika zikiwa hazifanyi jitihada zozote za kuibua vipaji hivyo hasa huku ambako ndiko chimbuko la wanariadha mashuhuri.

Renata Kawala, binti mwenye umri wa miaka 18 aliyezaliwa Haydom kabla ya kwenda New Zealand kimasomo akiwa na umri wa miaka 9 amekuwa akifanya vizuri katika mashindano mbalimbali ya shule za huko mashariki ya mbali anakosoma.
Renata Kawala (kulia kabisa) akianza mashindano ya riadha ya kilomita 2.5 nchini New Zealand na kuibuka kidedea (Picha kwa hisani ya gazeti la Marlborough, Novemba 29 2010)
 Akiongea na Ohayoda, Renatha alionesha picha mbalimbali pamoja na nakala za magazeti maarufu nchini humo ambako amekuwa "akiuza sura" mara kwa mara kutokana na mafanikio yake katika "track" kwa kushinda riadha (kuanzia mita 3000, 800 na hata 100 na kuruka) katika ngazi zote za U16 na U 18.

Pamoja na kuishi New Zealand kwa muda mrefu zaidi kuliko hapa Tanzania, Renata anaongea kiswahili fasaha utadhani anaishi tandale na bado anajivunia kuwa Mtanzania tofauti na wabongo wengi ambao wakishaishi ughaibuni hata kwa miaka 2 hujifanya kusahau kiswahili na wengine kuamua kubadili na uraia kabisa.

Renatha amejizolea tuzo za mashindano ya Urembo, michezo mbali mbali na zaidi ameongoza katika mtihani wa High School ambayo kule ni "Form Seven" kwa kushika nafasi ya kwanza kati ya wanafunzi 360 wa shule aliyokuwa anasoma hivyo kufanikiwa kuingia Chuo Kikuu cha Victoria cha Wellington, moja ya vyuo bora zaidi nchini humo.
Renatha (katikati-picha ndogo) katika hafla inayoitwa "Combined Colleges' Formal  (Picha kwa hisani ya gazeti la The Sun Blenheim 27 June 2012)

Katika mashindano ya January 2012, Alijizolea tuzo lukuki zikiwemo kushinda 3000m, shot-put na kuruka juu kati ya tuzo zingine. 
Katika mashindano haya Renatha alishinda 800m, shot put, na Kurusha Mkuki huku akishika nafasi ya pili katika mashindano ya Pentathlon na kuruka chini
Nadhani vipaji adimu kama hivi vinahitaji kuwa "scouted" na mamlaka husika kuwasiliana nao, wengi wapo nje ya nchi na wanajisikia fahari sana kama watatambuliwa na nchi na kupewa nafasi. Renata ni moja wa vipaji vya ukweli ambavyo kama havitathaminiwa si ajabu akifikia wakati kaiva "prime" utasikia anashawishiwa na wadau wa New Zealand, ukaishia kumwona Renata Kawala akiwa Olimpiki 2016 nchini Brazil, siyo kama Mtanzania bali M-New Zealand!
Naomba mlio karibu na wahusika wa michezo hasa riadha fikisheni ujumbe kuwa kuna kipaji cha ukweli, ambacho kina uwezo wa kuwa akina Filbert Bayi mpya.

2 comments:

 1. dahhhhhhh.

  Hongera sana Renata.
  na nimefurahishwa zaidi kwa wewe kuukumbuka
  na bado kufurahia kuwa M Tanzania.

  Mwenyezi Mungu akuongezee nguvu zaidi na mafanikio Mengi.

  ReplyDelete
 2. Hongera sana Renata kwa juhudi zako uzalendo wa kuikumbuka nchi yako Tz.

  ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda