Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Tuesday, February 12, 2013

Renata Kawala: Binti mwenye miaka 18 anayeipepeusha bendera ya Haydom na Tanzania huko New Zealand

Nilikutana na Renata jijini Dar es Salaam mwezi uliopita akiwa njiani kuelekea New Zealand baada ya kumaliza likizo yake ya miezi 2 ambayo aliitumia kikamilifu kwa kufanya shughuli za kijamii nyumbani. Kwa muda mfupi kabla ya kukwea pipa kwenda mashariki ya mbali,Ohayoda iliweza kufahamu mambo mengi sana ambayo msomaji wetu yatakupa hamasa.
Renata (wa pili kulia) akiwa na viongozi wa kijiji cha Ng'wandakw baada
ya kukamilika ujenzi wa bomba la maji ambalo alitoa kama mchango wake 
 Renata alizaliwa miaka 18 iliyopita na kusoma shule ya msingi Haydom kuanzia darasa la kwanza hadi la tatu na mwaka 2002 akiwa na miaka 9 alihamia New Zealand kuendelea na masomo ambapo mwaka 2012 alimaliza kidato cha saba (Form Seven) na kuibuka kidedea kwa kushika nafasi ya kwanza kati ya wanafunzi 360, matokeo ambayo yamemwezesha Renata kuchaguliwa kuingia Chuo Kikuu cha Victoria kilichopo Wellington ambao ni mji mkuu wa nchi hiyo ambayo inasifika kwa wanyama wanaoitwa Kiwi. Kwa mujibu wa mtandao wa http://www.4icu.org Chuo Kikuu cha Victoria Wellington kinashika nafasi ya 6 kwa ubora nchini humo.
Kifamilia zaidi: Kutoka kushoto ni mama yake Renata (Rose Kawala), Renata, John (kaka), swahiba wangu sana Cesilia na Robin.

"Nimezaliwa na kukulia huku japo niliondoka nikiwa mdogo, lakini mimi ni Mtanzania na najivunia kuwa Mtanzania. Hata nikiwa mbali na nyumbani nimekuwa nikikusanya hela ili niweze kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo nyumbani kila ninapopata nafasi" alisema Renata akiongea kiswahili fasaha sana tofauti na "wabongo" wengine ambao hujifanya wamesahau kiswahili baada ya kuishi nje kwa mwaka moja.

Binti huyu ambaye hapendi makuu na muda wote anatabasamu, awali hakutaka kabisa Ohayoda kuandika habari zake hasa juu ya mafanikio aliyoyapata katika tasnia ya urembo nchini New Zealand na katika michezo, na hata alipofika nchini mwezi Desemba mwaka 2012 alifanya shughuli zake kimyakimya na baada ya ushawishi mkubwa sana alikubali na kuruhusu Ohayoda iweze kuandika mambo kadha wa kadha yanayomhusu.
Machalii wa Haydom wakipiga "ubwabwa" wakati wa hafla ya kumpongeza Renata kwa kuchaguliwa kuingia Chuo Kikuu cha Victoria Wellington nchini New Zealand, hafla ilifanyika nyumbani kwao Haydom

Renata akiwa na Baby wakati wa hafla ya kumpongeza 

Watu kibao walikwepo kumpongeza Renata. Hapa akiwa na mjomba wake John Kawala, nyuma ni Thomas
Rose Kawala (kushoto) ambaye ni mama Mzazi wa Renata akifurahi  pamoja na mzee Edward Mnyau (katikati) na mama Mkubwa wake Anna Kawala
Kuselebuka kwenda mbele, mwenye suti ni Mwalimu George Dahhmay, mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Haydom
Wakati wa likizo yake, Renata aliweza kuchangia miradi kadha wa kadha ya kijamii, ambako alieleza kuwa akiwa shule amekuwa akifanya kazi (part time) huku akisoma na fedha hizo alizihifadhi ili ziweze kuwasaidia wananchi huku nyumbani.

Renata alichangia zaidi ya shilingi milioni 1 ambazo zilitumika kununua bomba za kusambaza maji kutoka katika tanki kubwa la maji lililopo Ng'wandkw, mradi ambao upo chini ya Kanisa Katoliki Jimbo la Mbulu kupitia DMDD.

Sehemu ya vifaa ambavyo Renata alivigharimikia, kwa kuunganisha bomba la maji kutoka kwenye tenki hadi karibu zaidi na wananchi
Tenki ambalo limejengwa kwa mchango mkubwa kutoka DMDD na Renata kuunganisha bomba kama inavyoonekana pichani
Sehemu ambalo "bomba la Renata" limepita
Ohayoda inatoa pongezi za dhati kwa Renata kwa kuthamini nyumbani na kuchangia maendeleo ya nyumbani japo ameishi sehemu kubwa ya maisha yake zaidi ya kilometa 8000 upande mwingine wa dunia, na pengine angekuwa na kila sababu ya kubadili uraia na kuwa raia wa nchi hiyo ambayo imejaa asali na maziwa, lakini akaamua kuchagua kuwa Mtanzania.

Renata akipokea zawadi kutoka kwa wananchi wa Ng'wandakw kwa kuwasaidia kufikisha maji karibu na makazi yao

Renata akikabidhi mchango wake kwa mhasibu wa DMDD kwa ajili ya ujenzi wa bomba.
 Ohayoda inatoa wito kwa wadau mbalimbali hasa walioko nje ya nchi na mijini, ambao wamesahau kuwa huku nyuma wamewaacha babu, bibi na hata wazazi wao wanaishi katika mazingira magumu na kukosa huduma muhimu za jamii. Renata amechonga barabara, wengine tuige mfano huo, mchango wako mdogo unaweza kubadili maisha ya wengi vijijini. Tuachane na utamaduni wa kijinga wa kuchangia mamilioni kwa ajili ya harusi wakati fedha hizo zingeweza kuwapatia wananchi wa kijiji kimoja maji safi na salama au wanafunzi wakapata vitabu badala ya kutumia hela zote ndani ya siku moja na bado wanandoa wanabaki na mzigo mkubwa wa madeni.
Renata akiwa na Afisa Elimu (Sekondari) wa Wilaya ya Mbulu Bwana Hadu (kushoto) na kulia ni Afisa Misitu wa Wilaya ya Mbulu bwana Richard Bamuhiga alipotembelea ofisi zao

Renata akiwa na baba mkubwa wake Michael Massay ambaye ni Afisa Kilimo wa Wilaya ya Mbulu
Bibi yake Renata (katikati). Hapa ni kijijini Mbulumbulu wilayani Karatu mapema mwaka huu. 
"Eti" alikuwa hajawahi kupanda bodaboda, atakuwa na mengi ya kusimulia huko Mashariki ya Mbali
Ohayoda inamtakia Renata mafanikio mema anapoanza masomo yake ya Chuo Kikuu, tunaamini atazidi kuwa chachu ya maendeleo siyo tu huku Haydom, bali pia Tanzania kwa ujumla. tunaamini kuwa Watanzania waliopo nje ya nchi hasa rafiki zangu akina Mwombeki Fabian, Amani Kitali, Steven Habakuki, George Martin Maemba, Cesilia Kawala na wasomaji wote wa Ohayoda watakuwa wamepata changamoto kutoka kwa Renata.

3 comments:

 1. Dahhhhhh
  we mtoto wewe unatufanya sisi wa kubwa
  tujisikie vibaya hapa..

  Safi sana, mfano mzuri sana umeonyesha.
  na nina hakika wengi watafaidi sana na ulicho kifanya.

  Na Mungu atazidi kukuongezea busara , hekima na mema yote. Ubarikiwe sana.

  ReplyDelete
 2. Great challenge for all of us tanzanians! no matter where you live.

  ReplyDelete
 3. Imekaa Poa sana hii duh ndio naisoma leo oi oi oi

  Hii Sir Name Kawala looks familiar

  ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda