Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Tuesday, February 12, 2013

Papaa On Tuesday.....Kama Tunaona Uvivu Kuziba Ufa Tusitegemee Kupata nguvu ya Kujenga Ukuta


Na Sam Sasali a.k.a Papaa
Wakati Nchi yetu ya Tanzania siku ya Jana imeingia katika doa lingine la Umwagaji damu wa issue za kidini eti Waislam wamewavamia Wakristo kwa kufungua Bucha ya Nyama, katika fujo hizo Mchungaji wa EAGT amepoteza maisha na Waislam Wawili Wamepoteza Maisha kisa na Mkasa kuchinja nyama tunafanya masikhara na huu ufa kuujenga sasa utatugharimu kuujenga ukuta baadae.

Miaka ya nyuma nilipoanza kufanya kazi Serikalini neno la Kwanza kujifunza kuongea na watu waliokuwa wanakuja kwenye Ofisi ya Mkurugenzi ilikuwa "njoo kesho" ofisi nzima nilisikia kila kitu wanasema "njoo kesho" nikajikuta na mimi nimejifunza kusema "njoo kesho" ikifika kesho ninajikuta nimerundika kazi za jana kama kumi ambazo actually zilitakiwa kufanyika jana, pole pole ikaanza kujengeka kuwa tabia. Mambo mengi yanayoendelea leo ni hayakutokea ghafla tuliyadharau pole pole sasa yamekuwa matatizo sugu ambayo kuyatatua imekuwa ni changamoto si tu sababu ni magumu lakini gharama ya kuyaondoa ni kubwa zaidi kuliko tungeyafanya mwanzoni wakati yanaanza.


Kuna tabia nyingi sana ambazo pengine mimi ninazo ama wewe unazo ambazo kwa sasa zimeshakuwa sugu kwenye maisha yetu si kwa sababu tu zimetokea ghafla lakini pole pole zimekuwa ni sugu kwenye maisha yetu. Kuna wanawake ambao wanachukiwa na asilimia kubwa ya wanawake wenzao na pengine na wanaume na watu wameanza kuwakwepa sababu ya Umbeya. Tabia ya kutoa maneno huku kuyapeleka upande wa pili tena kwa kuyaongezea chumvi imesababisha kutengwa na kuogopwa na watu wengi, unakuta mtu akiwa na umbeya hawezi kunyamaza akiwa na neno atanunua hata vocha asambaze ujumbe, ndoa zimetikisika sababu ya mdomo upeke peke, mara kadhaa either umesutwa ama watu walikaa kikao kukuchana sababu tu mdomo, umejaribu kuacha tabia umejikuta umenyamaza wiki moja wiki ya pili uko pale pale, tabia hii ilianza pole pole gharama ya kuiacha ni kubwa zaidi, yamkini wengine tabia ya Kiburi, siku zote sisi tunataka kuwa juu, tunadharau watu sababu ya kipato chao, tunadharau watu sababu ya elimu zao tunadharau watu kwa vile tu walivyo sio Standard zetu, yamkini tumewakataa hata wachumba sababu ya viburi vyetu tabia hizi mbaya zimetufanya kwa namna moja ama nyingine kuto kusonga mbele.


Siku chache zilizopita nilikuwa na kesi mezani kwangu ya watu waliokuwa wakihitaji msaada watabia aliyokuwanayo mkaka, kwa muda mrefu sana huyu mume amekuwa akijisikia raha ya tendo la ndoa akijichua kwa mkono wake au mkewe akimchua kuliko wakishiriki njia ya kawaida, hali imekuwa ni mbaya zaidi sababu kuna nyakati mkaka anajichua hata wakikaa sebuleni. Katika kuongea nao Mkaka alinieleza kuwa amekuwa addicted kabisa na kujichua hawezi kukaa siku ipite bila kujichua katika kutafuta chanzo tukakibaini chanzo ambacho kwa awali haikuonekana kama kitakuja kuwa tatizo lakini pole pole alidharau huo ufa sasa kasheshe anataka kubomoa ukuta ambao una gharama kubwa zaidi. Hujawahi kutana na Mwanaume kwenye ndoa ana mke mzuri anapata kila kitu kutoka kwa mkewe lakini kutwa kucha yeye anavizia ma house girl??Katika shughuli zangu niliwahi kutana na Mwanamke ambaye yeye anasikia raha ya tendo la ndoa iwapo ataingiliwa kinyume cha maumbile, akifanya kwa njia ya kawaida hawezi fika kunako kilele na raha ya tendo iwapo tu utabadili njia na kuingia njia ya nyuma, huyu ni mdada aliyekuja kwangu nimsaidie kutoka katika hali ya namna hiyo ambayo inamuuma na anatamani kuiacha tatizo sasa anaachaje??nimekutana na kesi nyingi sana ambazo mwanzoni watu ama mtu alizichukulia pouwa akajua hakuna madhara lakini matokeo yake sasa amekuwa muhanga wa hiyo tabia umepoteza furaha ya maisha na ndoa na kazi kwa sababu ya tabia ambazo hauzipendi lakini umejaribu kuziacha lakini umejikuta gharama yake ya kuibomoa inaweza gharimu maisha yako ya sasa na furaha.

Kuna mambo ambayo yanaendelea leo kwenye maisha yetu na Taifa letu ama kwenye familia zetu tunadhani ni madogo na yanaweza kutatuka kirahisi hata hapo baadae na tunasahau kuwa mazoea hujenga tabia. Tabia uliyonayo leo ilianza kujengwa kwenye mazoea. Vifo tunavyovisikia leo vinaanza kuzoeleka, tutazoea watu kufa kisha itabadilika kuwa tabia Mungu na aepushilie mbali. Matatizo mengi yanayoendelea leo kwenye maisha yetu ya kawaida maisha yetu ya mahusaiano ya kimapenzi, biashara na kazi either yamejengwa ama yamebomolewa na mazoea. Mtu anayezoelea mazuri anastawisha kile akifanyacho anayejizoea ubaya ni kwa uangamifu wake mwenyewe. Unakuta mtu mdada ama mkaka anahangaika leo kupunguza kitambi ama unene ni rahisi sana kuongezeka kuliko kupungua, ukianza kuona uvivu kupunguza kilo 2 usitegemee kabisa kama unaweza punguza kilo 5 kirahisi. Tunapuuzia kwa kudhani kesho tutatatua, tunadhani kesho ndio siku nzuri ya kufanya kuliko leo, kama kuna linalowezekaa leo kwanini lingoje kesho. Kukaa na huzuni na jambo moyoni linaweza kukukosesha raha ya milele kuliko ukalisema mara moja. Wana Saikolijia wanaamini njia moja wapo ya kuwa na afya njema ya akili ni kuyasema matatizo uliyonayo, kuongea ni tiba kubwa kuliko kulazwa hospitali.

Tafakari leo mambo mangapi umeshindwa kuyafanya na kukuletea madhara kwa sababu tu uliamua ku-buy time ama kwa vile tabia hiyo imeshajengeka ndani yako imeathiri aina ya marafiki ulionao wanakuona uko sivyo,imeathiri marafiki zako wa kukusaidia sababu wanaona hausaidiki, imeathiri mahusiano uliyonayo kwa sababu ukiamuni "hivyo ndivyo ulivyo".Think differently and Make A Difference.

Ze Blogger.
0713494110

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda