Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Monday, February 25, 2013

Papaa On Tuesday....Kama Kila Mtu angeijua Kesho Yake Angebweteka Leo

Na Sam Sasali

Ikiwa ni Jumanne yangu ya Mwisho kabisa kwa mwezi huu wa February, 2013 nina Kila Sababu ya Kumshukuru Mungu Kwa ajili ya Kunifikisha siku ya leo na Kutufikisha siku ya Leo. Siku Ya Leo nina majonzi baada ya Rafiki Yangu Onesmo Ngussa ambaye niliwahi kufanya nae Praise Power Fm Kufariki dunia yote haya ni mapenzi ya Mungu. Ninakumbuka tarehe 2 November, 2012 nilisafiri nae kutoka Dar Mpaka Mwanza na Tulipokelewa na Mama yake, hili ni Jembe ambalo halitasahaulika Kila nilipokuwa nafikiri kutengeneza Tangazo la Radio, Jina la Kwanza ilikuwa lazima awe Onesmo Ngussa a.k.a Papaa.

Weekend hii nilipata nafasi ya kufanya reflection ya mwezi January na Mwezi February ili kuona kama tunaenda sawa ama sio na plans zangu za mwaka huu nikashukuru Mungu kuna mambo yamesonga kuna mambo yamekwama, nikalinganisha na Mwaka Jana na Neema na Milango ambayo Mungu amenifungulia Mwaka huu nikaona hakika kama Mtu angeijua Kesho yake basi asingehangaika sana kujishughulika sababu anajua matokeo yatakuwa positive ama negative.


Kama kila mmoja wetu angekuwa anajua kile ambacho destiny yake kimebeba basi wengi wangebweteka na maisha yao ya leo sababu wanajua piga uwa either watakufa ama watafanikiwa sana. Umewahi kukaa mahali ukawaza miaka yako mitano iliyopita ama 10 ama 20 ukaona kuna siku ulijiuliza maswali mengi sana na kukosa majibu na uliona mauti ina thamani kuliko uzima hii yote ni kutokana na yale uliyokupata lakini leo ukitazama ulipo na ulipotoka unakumbuka jitihada ulizofanya mpaka hapo ulipo unabaki kutabasamu. Kuto Kukata tamaa kwenye maisha ni silaha pekee ambayo inaweza kukufanya ukafika mbali na kutimiza ndoto zako. Wengi wetu tukikatishwa tamaa tunabaki kusikitika na kunung'unika hakuna jitihada tunafanya, wengine wanaishia kulia ama kukaa tu sababu ya kuchoshwa na kile kinachoendelea kwenye maisha yao.
Hakuna jambo kwenye maisha linadumu milele, yamkini uliacha kazi ukadhani mambo yatakuwa safi, ghafla umeanza kukumbuka ofisi yako ya zamani wewe sio wa Kwanza Wana wa Israel walikumbuka Misri itakuwa wewe kukumbuka Mwajiri wako??Kuna watu waliolewa na expectations zikiwa juu sana kuwa maisha yatakuwa kama Paradiso matokeo yake wamekutana na Jehanamu ndogo ndani ya Muda Mfupi, Yamkini Ulichukua Mkopo ukadhani ungefanyia la maana ajabu hakuna la maana ulilolifanyia na Makato ya Mkopo yanakupa mawazo kila iitwapo leo, yamkini wewe ni mgonjwa kiasi kwamba umekataa tamaa na huoni faida ya Kuishi, lakini wacha nikuambie HATA HILO NALO LITAPITA. Ukiniuliza litapitaje pitaje hata mimi sina majibu ukweli ni kwamba Ukiwa kwenye shida maishani huwa tunadhani tuko peke yetu wneye shida na wengine wao hawana shida kuliko sisi, wewe hujasikia Form Four walipata matokeo mabaya wamejiua??kwanini??wengi wetu hatuko tayari kubeba aibu ya kile tunachokifanya kwenye maisha.
Yeyote unayemuona leo ana furaha na amani ujue kuna siku aliwahi kuwa na huzuni, kuna ndoa leo wamejawa na vicheko na furaha lakini uliza kama hapo kale wengine wao hawakulia, ukimuona leo mtu amefanikiwa muulize ilikuaje, muulize Bakharesa Kutoka kuuza Urojo mpaka Leo Kumiliki Makampuni. Kama kila mtu angekuwa anajiona kesho atakavyokuwa jitihada ya kuelekea kwenye mafanikio ingekuwa ndogo sana sababu unajua itakuwa tu. Wengine wamewahi tupiwa mizigo yao nje ya nyumba zao, wengine wamewahi kudaiwa kodi ya nyumba kwa kudhalilishwa, wengine walitamani hata kufa lakini leo maisha yao yamekuwa ya mafanikio sana. Kuna Njia kwenye maisha ninaamini lazima uipitie ingawa sio lazima saaaana upite ila ukiipita inakusababisha kwanza kumtegemea Mungu lakini Pia inakufanya ubongo wako kuwaza mara Mbili ama Mara tatu ili kuweza kutoka pale Ulipo. Shida zinaleta akili, Shida zinaleta Ugunduzi, shida zinasababisha kutusukuma kwenye mafanikio. 

Ukifukuzwa kazi leo Jua ndo hatua ya Kuelekea Kwenye Kazi Nyingine, Ukiishiwa fedha leo Jua ndo Mwanzo wa Kupata Zingine, Ukishindwa kwenye Biashara Ujue ndo Mwanzo wa Kupata Njia bora ya Kuboresha, Ukiona Ndoa inayumba ndo mwanzo wa Kugundua mapungufu yaliyopo, tujifunze kuona mambo ni changamoto na sio matatizo kwenye maisha yetu ya Kila siku.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda