Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Thursday, February 21, 2013

Mary Nagu achunguzwa kwa Rushwa Uchaguzi wa NEC Hanang

Na Joseph Lyimo
Katesh

AHADI ya Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula ya kufuatilia wajumbe wa Nec wanaodaiwa kutoshinda  kihalali kwenye wilaya zao,imeanza kutekelezwa baada ya ujumbe kutoka Dodoma kufika wilayani Hanang’ Mkoani Manyara kufuatilia suala hilo. 
Wajumbe hao wawili ambao ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) wa wilaya ya Iringa ambaye pia ni mwanasheria wa chama hicho na mjumbe wa maadili kutoka Dodoma waliwahoji wana CCM juzi wilayani Hanang

Wajumbe hao walifika wilayani humo baada ya kuagizwa kutoka Dodoma kwa ajili ya kufuatilia mgogoro wa muda mrefu wa baina ya Mbunge wa jimbo hilo Dk Mary Nagu na Waziri Mkuu mstaafu Fredrick Sumaye. Katika uchaguzi wa kugombea nafasi ya ujumbe wa NEC wilayani humo uliofanyika mwaka jana Nagu alishinda nafasi hiyo kwa kupata kura 648 na Sumaye akapata kura 481.

Baada ya matokeo hayo kutolewa baadhi ya wana CCM wa wilaya hiyo waliandika barua kwa Mwenyekiti wa CCM Jakaya Kikwete wakipinga mwenendo wa uchaguzi huo wakidai kuwa ulitawaliwa na rushwa. Walidai kuwa mmoja kati ya wagombea hao alikuwa anagawa rushwa ya kuanzia sh100,000 na kuwapa kiapo cha kuwalambisha asali ili achaguliwe kwenye nafasi hiyo ya mjumbe wa Nec.

Kutokana na hali hiyo ndipo juzi wajumbe wawili kutoka makao makuu ya CCM Dodoma wakatumwa wafike wilayani Hanang’ kwa ajili ya kufuatilia suala hilo ambapo watu zaidi ya 10 waliokuwa wanalalamika walihojiwa na wajumbe hao. Miongoni mwa malalamiko yao ni rushwa kutawala kwenye wilaya hiyo hadi kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 CCM ikapoteza viti 13 vya madiwani vilivyochukuliwa na Chadema kata 12 na CUF ikachukuwa kata moja.

Mmoja kati ya walioandika barua hiyo ya malalamiko alisema kuwa pia Katibu wa CCM wa wilaya hiyo Allan Kingazi alihojiwa na wajumbe kwa kudaiwa kuongeza matawi hewa yaliyomsaidia kushinda mgombea mmoja. Alisema zaidi ya Kingazi na Dk Nagu walihojiwa kwa zaidi ya saa mbili pia aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM wa wilaya hiyo,ambaye anadaiwa kuwa ndiye alitumika kuwapa hongo wajumbe naye alihojiwa kwa saa mbili. 

Alisema baada ya kumaliza kuwahoji watu hao wajumbe hao waliondoka na kudai kuwa wanapeleka mrejesho kwenye kamati ya maadili ya CCM Taifa ambayo ndiyo iliyowapa kazi ya kuja Hanang’ na ndiyo itakayotoa majibu. Hata hivyo,Katibu wa CCM wilayani Hanang’ Allan Kingazi alipoulizwa kuhusu kuhojiwa na wajumbe hao wa kamati ya maadili ya Taifa kutoka Dodoma aligoma kuzungumza kwa kudai kuwa hayo ni mambo ya chama.

Haya mambo hayawahusu waandishi wa habari kama ni masuala ya kuwahusu wanachama wa CCM wilayani Hanang’ ningekueleza ila haya ya wajumbe kutoka Dodoma hapana labda uwaulize wenyewe,” alisema Kingazi.

Naye,Dk Nagu alipopigiwa simu jana ili azungumzie masuala aliyohojiwa na wajumbe hao hakupokea simu na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa simu na kutakiwa kueleza mambo aliyohojiwa hakutuma majibu yoyote.

1 comment:

 1. itapendeza zaidi kama huo uchunguzi utafuatiliwa.
  Tumesha zoea kuona fulani anachunguzwa ajili ya rushwa lakini hakuna cha maaana kitakachofuatilia na hii ndio Tanzania yetu .

  Dawa ni kung'oa serikali yote ya CCM .
  Tunahitaji serikali mpya na mawazo mapya
  kwenye kila idara.

  Imenisikitisha sana kuona matokeo ya form 4.

  Na pia ni muhimu kwa serikali kusikiliza wanachi na si wao kufanya watakalo.
  Time for change.

  ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda