Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Monday, February 11, 2013

Mapigano makali yazuka katika bonde la Yaeda Chini

Wakati hali ya amani nchini ikizidi kuwa tete na mapigano yakiripotiwa maeneo mbalimbali nchini, mapigano makali yameendelea kwa muda ya siku 3 katika bonde la Yaeda Chini wilayani Mbulu baina ya wafugaji waliovamia maeneo na wenyeji wanaoishi katika bonde hilo

Mapigano hayo yamezuka wakati ambao huko mkoani Geita ambako wakristo na waslamu wanapambana kuhusu uahalali wa "wakristo" kuchinja na kusababisha umwagaji wa damu. Haya yanatokea wakati vurugu za gesi huko Mtwara bado zikiwa zinarindima katika vichwa vya wananchi na mapigano baina ya wakulima na wafugaji huko Dumila mkoani morogoro.

Mapigano ya huku Yaeda Chini yamedumu kwa siku tatu ambapo jana Mkuu wa Wilaya ya Mbulu ndugu Anatoly Choya alitembelea eneo la mapambano ili kumaliza mapambano hayo ambayo yametokea baada ya wafugaji wawahamiaji kuvamia maeneo ya malisho na mashamba ya wenyeji na kuzua mapambano hayo yaliyodumu kwa muda siku 3.

Wenyeji hao ambao wamechoshwa na uvamizi huo wa mara kwa mara unaofanywa na wafugaji hao ambao hupeleka mifugo yao katika bonde hilo kuanzia mwezi Desemba na kuondoka mwezi Aprili huku wakiharibu mazao na maeneo ya malisho ya wenyeji

Aidha Mkuu wa Wilaya ya Mbulu amewaagiza wavamizi hao kuondoka mara moja na hali ya amani imerejea katika eneo hilo ambalo ni makazi  ya kabila la Hadzabe.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda