Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Monday, February 18, 2013

Engagement Party ya Flora Kauky: Kitu Simple, Elegant but Classic..... Hongera Swahiba

Juzi Jumamosi ilikuwa "engagement party" ya swahiba na jirani yangu Florah Kauky iliyofanyika nyumbani kwao Basotu CMSC. Ilikuwa nderemo vifijo na muhemuhe kwa pande zote mbili kwani ndugu, jamaa na marafiki walikuwepo...kutoka ukweni Karagwe na familia ya Kauky na zaidi marafiki zake Florah tulikuwepo. Lakini kikubwa zaidi siku hiyo nilikuja kufahamu kuwa mama yake Florah na mama yangu mzazi ni mtu na dada yake lol na muda wote tumefahamiana miaka nenda rudi hatukuwahi kulijua hilo, likaja swali....what if......? hahahaaa Mungu mkubwa tulikuwa maswahiba tu!
 Pata uhondo wa jinsi mambo yalivyokuwa siku hiyo, shughuli ilikuwa Simple but Elegant! Haikuwa na mbembwe nyingi waa gharama zisizo na msingi na kusudi likafikiwa

Bernadeta naye alikwepo

Si Florah akaja kutulaki ile tumefika? 

Alifurahije mtoto wa Kauky?

Timu y marafiki iliyotoka Haydom ikiongozwa na Bwana Harusi mtarajiwa (si wa Florah lakini) almaarufu kama ustaadh Jamal a.k.a Tarimo...mheshimiwa Jackson Tarmo Bajuta

Filipo Ammo naye akajichanganya, kumbe Filipo naye ni ndugu yangu kama Florah lol!

Baba na Mwana...Flora akiwa na Baba yake mzazi mzee Kauky

DADAZ

Robert Masanja (kushoto), Angela na Stella (kulia) walikuwa ndani ya nyumba. Mh Stella sijui alikuwa anampiga nani jicho kama kamera ilivyomnasa

Shughuli ikaanza

Babu "yetu" na shemeji na wageni wengine wakiingia ukumbiniKama sielewi elewi kilichokuwa kikiendelea kati ya Laura na huyu mshikaji...kumbe wanaangalia picha kwenye kamera duh

Baba Mkwe wa Flora akizungumza na waliokuwepo

Emmanuel mwenyewe (mwenye shati jeupe) akifuatilia mchakato mzima kwa kina

Mamaa Kauky aka Flora wa Emma

Emmanuel mwenyewe...from Karagwe to CMSC with love! kumbe walikutana Shinyanga Flora akiwa "shule"

Haya sasa, kitu kishafanyiwa "Booking Officially", emsii alisema ameshamfunga kamba!

Sherehe haikamiliki bila hii makitu aisee! Tulipigaje msosi!

Kwa mujibu wa MC, Emmanuel aliliangua "embe" na kulivundika, bado hajaruhusiwa kulila.

Turu naye hakukosekana, kitu cha "ngano" mkononi teh teh, alidakwaje njiani na manjagu kwa kuendesha "tuk tuk" bila leseni? Kwa ujumla ilikuwa fuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuun

Kaka na dadaz....huyu dogo nllikutana naye mwaka jana wakati napiga picha za bung'eda Gidmarir kilometa chache kutoka CMSC...

Kifuatacho ITV....................(sitaki kusema, ngoja tusubiri)
Hongera sana Flora, tunakutakia mafanikio mema katika kuelekea maisha mapya. Kama marafiki tunawatakia maandalizi mema kuelekea kufikia siku yenu;
Ni sisi marafiki zako...Robert Masanja, Stella Mshanga, Angela, Bernadeta, Jackson Tarmo, Laura, mama Mdogo Magreth Diyamet, Ringo, Godii, Turu, Filipo Ammo, Flora na Blogger mwenyewe

1 comment:

  1. Hongera sana dada.
    Nakutakia kila jema maishani.

    Umependeza kweli kweli .

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda