Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Friday, February 8, 2013

Huku KKKT wakimlilia Baba Askofu Laizer, kule Jimbo Katoliko Moshi wamlilia aliyekuwa askofu wa Jimbo hilo Mhashamu Askofu Amedeus Msarikie.

Wakati bado tukikumbuka kifo cha askofu Balina wa shinyanga, taarifa zilizoko katika vichwa vya wakristu wengi sasa na dunia kwa ujumla, ni kuhusu vifo viwili ambavyo vimetokea kwa wakati mmoja. Nikiwa nimekaa naangalia ITV nikasikia habari za kifo cha askofu wa KKKT diyosisi ya kaskazini kati. Nikiwa najaribu kuwasiliana na rafiki zangu wa hapa na pale mara nikakutana na habari za R.I.P baba Msarikie. Huyu alikuwa askofu wa jimbo la Moshi kwa kipindi cha muda mrefu. 

Ni kipindi kigumu sana kwa wakristu wa madhehebu yote haya mawili kutokana na kazi kubwa ambayo miamba hii imefanya kwa kanisa la Tanzania na kwa dunia kwa ujumla. Uimara wa shule mbalimbali za Jimbo katoliki la Moshi ambalo ndo linaloongoza kwa kuwa na shule nyingi za din ambazo zinahudumia watanzania wote na wote wanapata huduma bora bila ubaguzi, Hizi ni juhudi za pekee za baba Msarikie. 

Wakati wa askofu Laizer yapo mengi makubwa ambayo baba huyu aliyasimamia kwa umakini mkubwa sana hasa shule, huduma ya afya na hata kushauri katika masuala mbalimbali ya serikali bila woga. Lakini pia alisema neno wakati wa Babu Wa Loliondo na Kikombe chake Cha Tiba.

Baba Askofu Thomas Laizer.
Hii si rahisi sana kuondokewa na miamba hii ambayo michango yao kwa taifa hili ni mikubwa sana na ni imani yetu kuwa sote tutawakumbuka sana.

Hatuna budi kujifunza kutokana na kazi yao. Mungu umewapenda zaidi, atupe Neema ya kuona thamani ya kazi mliyoifanya na kuishi yale mahusia ambayo mmekuwa mkiyafanya.

Bado hatujapata taarifa za mazishi ya baba Askofu lazier lakini kwa mujibu wa Fr. Cyril Lawrence kwenye wall yake ya Face book ni kuwa,  Mazishi ya Mhashamu Askofu Mstaafu Amedeus Msarikie yatakuwa siku ya Alhamisi tarehe 14/02/2013. Ibada ya Misa itaanza saa 4 kamili asubuhi. Mwili wa marehemu utawasili Jimboni Moshi siku ya Jumatano ukitokea Nairobi na siku hiyo kuanzia saa 10 jioni kutakuwa na Masifu ya Jioni yakifuatiwa na kutoa heshima za mwisho, sala na mkesha na heshima za mwisho zitamalizika dakika chache kabla ya Ibada ya Mazishi kuanza saa 4 kamili asubuhi siku ya Alhamisi. 

Wapumzike kwa amani - Amina!........

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda