Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Wednesday, January 9, 2013

Tumerejea kutoka kwenye Mapumziko ya Mwisho wa Mwaka

Heri ya mwaka mpya 2013 wapenzi wasomaji wa Ohayoda!
Kwa takribani mwezi mzima timu nzima ya Ohayoda ilikuwa katika mapumziko ya Krismasi na Mwaka mpya hivyo wasomaji wetu wamekosa mambo mengi ambayo yamekuwa yakitokea katika jamii yetu, mambo ambayo wamekuwa wakitegemea Ohayoda kuwa mstari wa mbele kuwaletea.


Aidha tunapenda kuwashukuru wasomaji wetu kwa kuwa nasi toka tulipoanza takribani Mwezi Mei mwaka jana, wasomaji wetu wamekuwa sababu ya sisi kupata ujasiri na ari ya kusonga mbele na kuthubutu kuwaletea mambo kem kem wakati mwingine kukumbana na vitisho, kukatishwa tamaa na hata kukosa sababu au msukumo wa kufanya kutoka ndani..

Mwaka 2012 umekuwa na mafanikio makubwa sana kwetu, kwanza kabisa uthubutu wa kuanza hatua ya kwanza na kuandika makala ya kwanza...kisha ya pili....ya tatu...huku tukiwa hatujui hatua inayofuata itakuwaje na wasomaji wetu watatupokea vipi, baada ya mwezi moja, ilikuwa ni zaidi ya muujiza kwani hata pasipo matangazo na tukiwa tunaandika kutoka Haydom, Ohayoda ilipasua anga na kujipatia umaarufu mkubwa na kukusanya wasomaji mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi, tukazidi kupata msukumo na kuendelea kuandika makala na habari mbalimbali tukazidi kusonga mbele.......

Kati ya habari ambazo zilikuwa na mvuto kwa wasomaji wetu mwaka 2012 ni pamoja na Mashindano ya Urembo ambapo Miss Haydom Lucy Stephano aliweza kuiwakilisha vyema Haydom katika ngazi zote hadi kufikia kushinda taji la Miss Photogenic Tanzania 2012. Habari ya Hhando Samo kujiteka na kusababisha dhahma kubwa katika mji wa Haydom na Viunga vyake, Makala za sintofaham, ujio wa Balozi wa Namibia nchini, Tamasha la Utamaduni Haydom na Makala Mbalimbali ya utamaduni hasa Historia na Maisha ya Wairaqw, wadatoga, Wanyiramba na Wahadzabe.

Kubwa zaidi ambalo pengine wasomaji wetu hawakupata fursa ya kufahamu ni Ohayoda kusinda tuzo ya Ubunifu iliyotolewa na Shirika la Misaada la Kanisa la Norway (Norwegian Church Aid-Tanzania), tuzo ambayo bila wasomaji wetu tusingeweza kuipata na hii tuzo ni kwa ajili ya wasomaji wetu, ni zawadi ambayo wasomaji wetu wametupa kwa kutambua mchango wetu katika kuleta mabadiliko chanya katika jamii yetu na kuweza kujenga jamii yenye haki, usawa, uwazi. amani na utulivu. Ni imani yetu kuwa kwa mwaka 2013 tutazoa tuzo nyingine nyingi zaidi.

Mwaka ndio umeanza ikiwa ni siku ya nane toka mwaka 2012 uishe, tunatamani kuwaletea mengi lakini bbila ushiriki wako hatutafika malengo yetu, tafadhali kama unalolote la kushirikiana nasi, iwe ni kutoa habari au kushiriki katika uandishi wa makala mbalimbali iwe ya kisiasa, michezo, elimu, utamaduni, afya au hata matangazo, usisite kuwasiliana nasi kwa namba za simu hapo juu. USHIRIKI WAKO NI ZAIDI YA MUHIMU

Mungu Ibariki Afrika
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Ohayoda
Mungu ubariki mwaka 2013 uwe na mafaninikio makubwa kwetu wote. Amen

2 comments:

  1. Heri ya mwaka mpya wasomaji wote wa Ohayoda. kwa kweli nashukuru kuona umerudi uwanjani nili miss vipi Ohayoda wakati huu wa likizo. anyways nakutakia kila lakheri na baraka zote zitokazo kwa Mwenyezi Mungu. Nguvu mpya mwaka huu wa 2013. Wasomaji na wapenzi wote wa Ohayoda tuko hapa kupokea Habari moto moto kutoka Haydom Mbulu, Babati, Manyara, Tanzania na sehemu nyingine nyingi. nakushukuru kwa kazi nzuri ulioifanya 2012. Kila lakheri 2013. Long live Ohayoooooooooda.......

    ReplyDelete
  2. Kwa niaba ya timu nzima ya Ohayoda tunawashukuru wasomaji wetu hasa Afrodenzi, ninyi ndio sababu ya sisi kuendelea kuandika na kuwaletea habari na matukio yote haya muhimu.

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda