Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Tuesday, January 29, 2013

Mtwara wameweza, hata kwetu inawezekana

Hatimaye serikali kwa mara ya kwanza katika Historia ya Nchi hii imesalimu amri kwa wananchi baada ya wananchi wa Mtwara kupinga kusafirisha Gesi ya Asili kutoka Mtwara na kupelekwa Dar es Salaam. Sitaki kuingia kwa undani na kuhukumu nani yupo sahihi au la, na suala la umuhimu wa kusafirisha gesi hiyo badala ya kujenga mitambo huko huko Mtwara badala ya jijini Dar es Salaam maana yawezekana Serikali ilikuwa na nia njema kabisa ya kusafirisha gesi hiyo ili iweze kutumika hata zaidi ya kuzalisha umeme, lakini hoja ya msingi hapa ni kuwa wananchi wamechoshwa kupelekeshwa na wameamua kuhakikisha rasilimali zao zinatumika kwa faida yao.
Moja ya Mabango ya wana Mtwara wanaopinga gesi kwenda Dar

Wananchi wa Mtwara wameonesha tofauti kubwa sana na Watanganyika tuliowazoea, waliweka itikadi za kidini na kisiasa pembeni na kuamua kusimamia rasilimali zao kwa faida yao huku wakijifunza kutoka kwa ndugu zao wa kanda ya ziwa ambao kuishi kwao karibu na migodi ya dhahabu badala ya kuwaletea neema kumekuwa kama laana, wameachiwa mashimo na madini ya zebaki.
Haya ndiyo maazimio yaliyofikiwa baina ya serikali na wenye nchi hao ambao sio jeshi la polisi (kupitia mabomu ya machozi na maji yanayowasha) na hata viongozi wa juu wamethubutu kuwatuliza.

  • Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Mstaafu Simbakalia kawaomba radhi wananchi wa Mtwara.
  • Waziri Nchimbi kutumia lugha kibabe na vitisho dhidi ya raia pamoja na taarifa isiyokuwa na tathmini halisi na yenye uwiano pale alipotolea mfano askari aliyevamiwa dukani/baa yake na kuibiwa pesa kiasi cha sh. 1,895,000/= na kupoteza mali ya sh. 200,000,000/= (milioni mia mbili) na kusababisha watu wagune.
  • Kawambwa kawahimiza wazazi kuwaruhusu watoto kwenda shule kupata elimu sanjari na chuo cha VETA kutoa masomo ya mitaala ya gesi sanjari na uchomeleaji baharini.
  • Tibaijuka amezungumzia kuhusu upanuzi wa mji wa Mtwara na kuleata kauli mbiu ya "Amani na Maendeleo" kutoka kwao Kagera.
  • Mwakyembe amezungumzia upanuzi wa bandari kavu na ujenzi wa reli Mtwara, Liganga, Mchuchuma hadi Mbamba Bay na kuahidi kuja Mtwara kila baada ya miezi 3 na kujadili na kutathmini changamoto.
  • Waziri Mkuu ametoa udhuru wa Waziri wa ujenzi Dk Magufuli ambaye alitakiwa kuwepo lakini hakuweza kuhudhuria.
  • Bi Mapunjo kaahidi mipango mikubwa ya ujenzi wa viwanda mkoani Mtwara.
  • Mbilinyi kaainisha idadi ya makampuni yaliyoonyesha nia ya kuja kuwekeza Mtwara (sina hakika sana kama ni Mtwara)
Wana Mtwara wameonesha inawezekana, wakati natafakari haya nikawaza ni jinsi gani mikoa ya pembezoni ilivyosahaulika japo ni ya muhimu sana katika ustawi wa nchi yetu. Ukiwauliza wakazi wengi wa mikoa hasa ya Manyara na Singida hasa Dongobesh, Haydom, Mkalama, Basotu, Nduguti, Mbulu, Bashnet, Ilongero, Mtinko na maeneo ambayo bado barabara ni za vumbi watakuambia kuwa hata hawafikirii suala la lami achilia mbali viwanda.
Manyara na singida ni wakulima na wazalishaji wakuu wa alizeti, vitunguu maji, vitunguu saumu na ngano kuliko sehemu yoyote ile nchini, lakinii hakuna viwanda hata vya kusindika vyakula. Ni wakati muafaka wa huduma hizo kuwepo badala ya kusubiri mpaka wananchi wachoke ndipo uamuzi wa dharura ufanyike huku maisha ya watu wengi yakiwa yamepotea.
Ni wakati muafaka kuwa badala ya kusafirisha ngano, akina Bakhresa waje wajenge viwanda vya unga Basotu, Katesh au Haydom. Na badala ya kupeleka mahindi Arusha, tunahitaji viwanda vya kusindika unga wa mahindi Mbulu, Haydom, Karatu, Singida na Babati. 
Singida nako pawepo na Kiwanda cha kusindika nyama za kuku maana sehemu kubwa ya kuku wanaotumika hapa nchini wanatoka Singida kama ambavyo Mtwara kuna viwanda vya korosho. 
MTWARA WAMEONESHA INAWEZEKANA, HATA HUKU KWETU NAKO INAWEZEKANA!

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda