Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Wednesday, January 23, 2013

MAMBO YA DIGITALI: MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA UNAPOTAKA KUNUNUA KOMPYUTA AU LAPTOP.

Mara nyingi nimekuwa nikikumbana na hili swali, "ninataka kununua laptop, ipi ni nzuri? Ni swali ambalo pengine na wewe umekuwa ukijiuliza, mtaalamu wa teknolojia ya Habari na Mawasiliano Victor Mbombo leo anakujuza kwa undani.

Kwa Mwanafunzi, Mfanyabiashara, Mpigapicha (Photographer au videographer) Michezo ya Kompyuta (Computer Games), Mtumiaji wa Nyumbani /matumizi ya kawaida.

1. Wanafunzi 
Mambo makuu kwa mwanafuzi ni bei na kubebeka kwa laptop yenyewe. Laptop inayoweza kubebeka kutoka darasa mpaka darasa, au darasani mpaka kwa Sam muuza chipsi, ndio cha msingi , kwa hiyo kwa wanafunzi wengi huwa ni Notebooks ambazo hazina gharama kubwa, ni ndogo, inatumia nishati ndogo na ni kati tshs 450,000-700,000. Ubaya wake ni kwamba hizi huwa na screen ndogo na hutumia single-core CPUs ambazo zimepunguzwa nguvu.

Option nyingine ni laptop yenye inchi 13, nyembamba, ambayo ubebekaji (portability) yake (uwezo wa kubebeka) ni mzuri, na inapendeza zaidi wa kuandikia au kutumia ukiwa umekaa sehemu tulivu na sio haraka haraka. CPU zake ni dual-core na mara nyingi huja na optical drives. Mfano mzuri ni MacBook za Apple zenye inchi 13.

Nini Cha Kuzingatia: Walau iwe na 1GB ya RAM; 160GB au zaidi za HDD; inchi 13 au chini ya hapo.

2. Mfanyabiashara
Wale ambao mara nyingi huwa barabarani huitaji mashine iliyo haraka, inaydumu na chaji na zaidi ya yote

ThinkPad za Levono na Latitude za Dell ni mifano miwili mizuri ya laptop zilizotengenezwa zikimlenga mfanyabiashara (au kwa lugha rahisi, anayesafiri mara kwa mara) . Bidhaa zote mbili zina security nzuri na imara, pia hardware za in-built software zake zinafanya kazi vizuri na OS (Operating System) yoyote mfano windows, Ubuntu, etc (lakini sio Mac).

Ya kuzingatia: 2GB mpaka 4GB za RAM; 160GB au zaidi kwa Hard Disk; 12 mpaka 15-inch display; Windows Vista Professional au Windows 7 Professional; mobile broadband modem.

3. Mpigapicha na/au Videographer
Wachezaji wa games sio watu pekee wanaohitaji processor yenye nguvu, graphics za ukweli na hard disk space kuuuubwa. Kwa wale ambao wanatengeneza high-definition video or high-resolution photographs huitaji mashine inayojitosheleza hasa! Nimekuwa mpenzi mkubwa sana wa video producing. Miaka ya nyuma nikaanza kujifunza After Effects, FinalCut, etc. Ila kilichosumbua ilikuwa ni mashine. PC yangu RAM 1GB, hard disk 80 GB na vikolombwezo vingine vya kimaskini.

Nikaishia kwenye Windows Movie Maker 

MacBook Pro inch 15 mpaka 17 zile za Apple ndio maarufu na nzuri kwa kazi hii (japo ni ghali). MacBook ni nzuri pia kwa sababu software ya Final Cut, ambayo ndio maarufu DUNIANI kote kwa kutengeneza video, inapatikana kwenye Mac pekee. (Adobe’s Photoshop inapatikana kwenye platform tofauti tofauti, hivyo usijali).

Cha msingi hakikisha SANA SANA SANA kuwa una RAM kubwa…….. 8GB za RAM ndio penyewe. Pia hard disk ya 500GB ingependeza sana, kwa sababu redering in real-time inahitaji RAM/processor faster na inakula space hasa.

Cha kuzingatia: 4GB-8GB of RAM; Hard Disk ya 320GB yenye uwezo wa 7,200rpm, yaani 7,2000r per minute (usijali kama huelewi inamaanisha nini, wewe mwambie muuzaji hivyo ukiwa na uso mkavu..bhaaaas); 17-inch or larger display.

4. Wachezaji Games
Games za sasa hivi zinafika mpaka 20GB na hiyo setup tu! Mambo yanaanza kuwa mengi kama video card, sound drivers, na makolombwezo kibao! Kama wewe ni gamer, basi utahitaji desktop computers, zenye flexible upgradeability, faster components, na yenye uwezo wa kupoa haraka.Ila kwa siku za hivi karibuni, laptops zinazowafaa gamers zina-hit sana.

Ningependekeza kuanzia Core 2 Quad za Intel na Core i7 CPUs kwa 3D gaming, kwa sababu zina GPU nzuri ,kama GeForce N260 za Nvidia.

Ya kuzingatia: 4GB mpaka 8GB za RAM; 320GB au zaidi kwa Hard Disk; display ya inchi 17 au zaidi; bila kusahau the most important, discrete graphics GPU.

5. Mtumiaji wa Nyumbani
Mtu yoyote ambaye hayupo kwenye vipengele nilivyovitaja hapo juu anafiti hapa.Mtumiaji huyu huitaji desktop machine ambazo sio movable, Mashine hizi hutengenezwa kwa asili ya kukaa sehemu moja, ile jikoni, sebuleni, chumbani.

Zile laptop za inchi 15 bado ni maarufu ingawa zile za inchi 14 na 16 zinakuja juu siku hizi. Kila mtengenezaji wa PC hutofautiana na mwingine na huzidiana kila mmoja katika sehemu tofauti. Usikimbilie kununua mashine kuuubwa na kutumia hela nyingi. when all you needed was a simple one! 

Ya kuzingatia: 2GB mpaka 4GB za RAM; 250GB au zaidi kwenye Hard Disk; Display ya inchi 14-16; DVD burning optical drive (kwa asili ya ku-burn CD).

hayo ndio ya kuzingatia uendapo kukunua PC. Kuwa makini na kujua ni kundi lipi size yako.

1 comment:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda