Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Tuesday, January 22, 2013

Hatimaye Mgogoro kati ya H/Mji Babati na Tanga General wafikia ukingoni

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Babati Mkoani Manyara,Mohamed Omary Farah,akizungumza mbele ya madiwani wa mji huo baada ya kuandikiana makubaliano ya kupatana nje ya Mahakama baina yao na kampuni ya Tanga General iliyokuwa inamiliki shamba la Babati Sisal Estate (kushoto) ni Mkurugenzi wa kampuni hiyo Mustafa Mohamed na (kulia) ni Mkurugenzi wa Mji wa Babati Stella Pascal (Picha na habari kwa Hisani ya Joseph Lyimo)

MGOGORO wa kesi ya muda mrefu,baina ya kampuni ya Tanga General Ltd waliokuwa wamiliki wa shamba la Babati Sisal Estate na Halmashauri ya mji wa Babati umefika ukingoni baada ya pande hizo kupatana nje ya Mahakama. Makubaliano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita,mbele ya madiwani wa halmashauri ya mji wa Babati wakiongozwa na Mwenyekiti wao Mohamed Farah na mkurugenzi wa kampuni hiyo, Mustafa Mohamed na mwana hisa mwenzake Dhiru Chauhan.


Shamba hilo lenye ukubwa wa ekari 4,399 ambalo lilikuwa linalimwa katani hivi sasa ekari 4,149 zitamilikiwa na halmashauri ya mji wa Babati na kampuni ya Tanga General watamiliki ekari 200 zilizobaki. Kampuni hiyo ilimiliki shamba hilo ikilima katani, tangu mwaka 1955 hadi mwaka 1983 walipositisha ulimaji huo na mwaka 1999 Rais Benjamin Mkapa akaifutia umiliki kampuni hiyo na shamba hilo kukabidhiwa halmashauri. 


Kutokana na hali hiyo, kampuni hiyo ilifikisha suala hilo Mahakama Kuu, kitengo cha ardhi mjini Arusha mwaka 2005 na kufungua kesi namba 22/2005 wakipinga ufutwaji wa umiliki kwa kudai kuwa ubatilishaji haukufuata taratibu za kisheria. Katika kesi hiyo,kampuni hiyo ilikuwa inaomba irudishiwe eneo hilo au ilipwe fidia ya sh800 milioni na mahakama hiyo ikaona utaratibu haukufuatwa hivyo walipwe fidia ya sh 49 milioni ila shamba hilo libaki kwenye halmashauri hiyo.

 
Hata hivyo, kamapuni hiyo haikuridhika na hukumu hiyo, hivyo ikakata rufaa mwaka 2005 kwenye Mahakama ya rufaa kwa ombi la rufaa namba 22/2005 wakipinga hukumu hiyo kwa kudai kuwa hawakutendewa haki. Wakati kesi hiyo ikiwa inasubiriwa kupangiwa jaji,ndipo jana mbele ya Baraza la Madiwani wa halmashauri ya mji wa Babati na Mohamed na Chauwan wakatia saini makubaliano ya kufuta kesi na kugawana shamba hilo. 


Akizungumza baada ya kufikia makubaliano hayo, Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Babati, Mohamed Omary Farah aliwapongeza Mohamed na Chauhan kwa uamuzi wao wa kufikia makubaliano hayo nje ya Mahakama. Farah alisema watu hao ambao ni wazaliwa wa Babati, wameonyesha uzalendo kwa kitendo chao cha kuamua kufuta kesi hiyo kwani walianza mazungumzo hayo tangu mwaka 2011 baada ya kuchaguliwa kushika nafasi zao za udiwani.


“Hivi sasa kupitia hitimisho la mgogoro huu wa muda mrefu mji wa Babati umezaliwa upya kwani wananchi watapata fursa mbalimbali kupitia viwanja ambavyo vitakuwepo kutokana na shamba hilo,” alisema Farah.
Hata hivyo, Mwenyekiti huyo aliwataka watumishi wa idara ya ardhi kupitia mipango miji, kuhakikisha kuwa wanawaelekeza wananachi ipasavvyo kuhusiana na ujenzi kwani makubaliano hayo ni ushindi kwa mji wa Babati.
Alisema kuwa eneo la shamba hilo litagawanywa kwa wananchi ambao watauziwa na kununua viwanja ili waweze kujenga nyumba za kuishi na nyumba za biashara kwa ajili ya kuuendeleza mji wao usiwe wazi.


Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Tanga General Ltd, iliyokuwa inamiliki shamba hilo Mustafa Mohamed, alisema anashukuru mgogoro huo umefikia mwisho hivyo watafuta shauri lao Mahakamani.
“Nawashukuru wote waliohusika hadi tukaweza kufikia muafaka huu nje ya Mahakama,akiwemo Mwenyekiti wa halmashauri ya mji na wengineo hivyo tunachohitaji ni ushirikiano kwa yote tuliyokubaliana,”  alisema Mohamed.
Alisema kupitia makubaliano haya anataraji haki itapatikana kwa wote kwani ni muda mrefu mgogoro huo umekuwepo hadi kusababisha baadhi ya shughuli zao kusimama ila wanashukuru kila mmoja ameridhika kuhusiana na shamba hilo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda