Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Wednesday, December 19, 2012

Mwenyekiti Wareta (CHADEMA) apeta kura za maoni

Katika juhudi na harakati ya kuhakikisha kuwa wanamng’oa  madarakani mwenyekiti wa Kijiji cha Wareta kata ya Nangwa Wilayani Hanang', Mkoani Manyara, kupitia tiketi ya CHADEMA, Bw.Nicomedi Gojonjo, hatimaye zagonga mwamba na kuibuka tena kwa kishindo madarakani licha ya kumuhusisha na tuhuma 12 bado ameendelea kupeta.
 
Hali hiyo ilijihirisha mbele ya Mkuu wa Wilaya hiyo Bi, Christina Mndeme huku mamia ya wananchi wa Kijiji hicho cha wareta wakiwa wamefurika kujua hatma ya mwenyekiti huo juu ya hizo tuhuma 12 zilizokua zikimkabili, ambapo wajumbe wa halmashauri ya kijiji hicho walidai kuwa kwa muda mrefu walikua wakimshauri kuacha baadhi ya mambo anayotuhumiwa bila kusikia  na hivyo wajumbe hao kukosa imani naye na kumtaka aachie madaraka .
 
Akizungumza mbele ya mamia hayo Mkuu huyo Bi.Mndeme alisema kwa kawaida mkutano wa aina hiyo huwa ina agenda moja tu ambapo mkutano huo  umeitishwa kwa mijibu wa sheria ya serikali za mitaa, ambapo alisema kila jambo lina utaratibu wake, hivyo kitendo cha kumtoa madarakani mwenyekiti pia kuna taratibu zake licha ya kumhusisha na tuhuma hizo pia bado ana wajibu wa kuzijibu mbele yenu na kisha kumpigia kura za ndio na hapana, hiyo ndio hatua ya mwisho.
 
Akisoma  tuhuma zilizokua zikimkabili mwenyekiti huyo, Kaimu Katibu tawala wa Wilaya ya Hanang’ Mkoani Manyara ambaye ni katibu tarafa ya Katesh Bi.Zuena Omary, namba kwenye mabano alisema ni pamoja na (1) kukosa vikao vya halmashauri kwa muda mrefu Agosti mwaka jana hadi sasa.
 
Bi.Omary alisema tuhuma ya  (2) wananchi kukosa mikutano ya hadhara tangu mwenyekiti huyo alipoingia madarakani hadi sasa,  (3) kukosa taarifa ya mapato na matumizi  ya miradi ya kijiji toka achaguliwe hadi sasa, (4)mwenyekiti huyo amekodisha shamba la kijiji  msimu wa kilimo cha 2012-2013 bila kushirikisha wajumbe wa halmashauri ya kijiji na mkutano mkuu.
 
Aidha aliendelea kutaja kuwa ya (5) kukosa taarifa ya kesi ya kijiji iliyoko mjini Babati  na Arusha  toka amechaguliwa hadi sasa, (6)mwenyekiti huyo kufanya marekebisho ya mipaka  ya shule ya sekondari wareta bila kuwahusisha wajumbe wa halmashauri  wala kiongozi wa shule na wataalamu  wanaohusika, (7)kupuuza  malalamiko ya wazazi wa shule ya sekondari wareta  kuhusu wanafunzi, walimu na miradi ya shule
 
Aidha Bi.Omary alifafanu tuhuma zingine kuwa ni (8) kamati zilizochaguliwa kisheria  na za muda  hazifanyi kazi bila taarifa, (9) mwenyekiti huyo kufunga kisa na wananchi wa kitongoji cha Labay  kazi ya mradi wa maji  ya mita na lambo, (10)mwenyekiti kutengwa na familia yake  na kwao na wananchi wa kitongoji cha Getak kwa sababu za kimila na hivyo kuwafanya wananchi kukosa imani naye.
 
Pia tuhuma ya  (11) alisema  mwenyekiti huyo kuishi nje ya kijiji  na kila anapohitajika haonekani kila siku ambapo yeye akiwa ana kitu anachohitaji ndio anaonekana, ambapo tuhuma ya (12) ni katika utekelezaji wa maamuzi ya serikali ana muingilia mtendaji wa kijiji.
 
Aidha kilingana na mwongozo kilichofuata kilikua ni mwenyekiti huyo kupewa nafasi ya kujitetea juu ya tuhuma zilizokuwa zikimkabili na kufuatiwa na kupigiwa kura ya ndiyo na hapana , ambapo kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Wilaya ambaye pia ni afisa utumishi alimtangaza Bw.Nocomedi Gujonjo kuwa ni mwenyekiti halali kwa kujizolea kumla ya kura za ndiyo zitapazo 102 huku kura za hapana zikiwa 57, huku kura 6 zikiwa zimeharibika kati ya wapigakura wapatao 165.
 
Kufuati hali hoyo mkuu huyo wa Wilaya alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wananchi kwa kupiga kura na  kumpongeza mwenyekiti huyo ikiwa ni sambamba na kuwataka wananchi hao kuvunja makundi.
 
“ Kama nilivyosema awali wananchi ndio watakaokuwekama ama kukuondoa madarakani na si vinginevyo na sasa hali imejionyesha kuwa wananchi bado wanakuhitaji uwatumikie nawe hakikisha unatoa ushirikiano ikiwa na wao kutoa ushirikiano kwako ili kuweza kusukuma gurudumu la maendeleo kwa lengo la kujenga wareta mpya isiyo na makundi ”alisema Bi.Mndeme.
 
Aidha alisema kuwa wakati wa marumbano umekwisha sasa ni wakati wa kutafuta maendeleo,hivyo hakikisheni itikadi zenu mnaziweka pembeni kabisa kwani maendeleo hayana itikadi.
 
Naye Mwenyekiti huyo Bw.Gujonjo aliwapongeza wananchi hao kwa kumchagua kuwa mwenyekiti ambapo aliahidi kushirikiana nao bega kwa bega katika kuhakikisha maendeleo ya Kijiji cha wareta yanapatikana kupitia uongozi wake.
 
Wakiongea kwa nyakati tofauti nje ya mkutano huo, wajumbe wa halmashauri ya kijiji walisema hakuna haja ya wao kuendelea na uongozi huo na kuahidi kujiuzuru mara moja ili kuepukana na matatizo yanayoendelea kupitia mwenyekiti huyo

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda