Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Thursday, December 6, 2012

Msiviogope Vyombo vya Habari-RC Manyara

Na Mwandishi wa Ohayoda,
Babati
 
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Bw. Elaston Mbwilo amezitaka taasisi mbalimbali kuhakikisha wanavitumia vyombo vya habari katika kutangaza mafanikio  ikiwa ni sambamba na kuelezea changamoto zinazowakabili na sio kuviogopa na kuona kama viko kwa ajili ya kutoa mambo mabaya..
 
Hayo aliyaongea kwenye kikao maalumu kilichowakutanisha waandishi wa habari pamoja na wadau wa habari wa Mkoa huo wa Manyara kilichofanyika kwenye ukumbi wa White Rose mjini Babati, ambapo alisema kufanya hivyo kutawasaidia katika kufikia malengo yao waliyoyakusudia.
 
Bw. Mbwilo alisema baadhi ya taasisi zimekua zikiogopa kuvitumia vyombo vya habari kwa kudhani kuwa vitatoa habari mbaya, jambo ambalo alisema baadhi wa watu ama taasisi hupendelea kuona vyombo vya habari vikiripoti habari nzuri na si mbaya, jambo ambalo alisema wanatakiwa kubadilika na kuona kuwa habari zote ni sawa isipokua iwe ya ukweli na si vinginevyo.
 
Alisema vyombo vya habari ndio vinavyounganishwa kila kitu katika kuhakikisha vinatoa hamasa kwenye shughuli mbali mbali za maendeleo kwa jamii ili kuweza kujua kinachoendelea ndani na nje ya nchi, hivyo ni vema taasisi zikahakikisha vinatumia nafasi yake katika kuvitumia vyombo vya habari  ili kuwapa haki wananchi.
 
“ Vyombo vya habari ndio kila kitu, vinasaidia kuchochea kuharakisha shughuli za maendeleo, hivyo hatuna sababu ya kuviogopa , mimi najua mnaopoga kuandikwa vibaya, jambo baya ni pale ambapo habari imeandikwa kinyume yaani nje ya ukweli, lakini iwapo imeandikwa ndani ya ukweli inakuaje unaogopa kuvitumia, tambueni kuwa hata Serikali, Bunge, Mahakama vyote vinatumia vyombo vya habari katika kujiimarisha hususani katika kusikika na kueleweka kwa jamii” alisema Mbwilo.
 
Mkuu huyo  pamoja na mambo mengine  alizungumzia suala la waandishi wa habari kujiunga kwenye vikundi vya kuweka na kukopa (SACCOS) vitakavyowawezesha kupata mikopo  sehemu mbalimbali na hatimaye kuweza kujisaidia wao wenyewe kikamilifu ili kujikwamua kiuchumi.`
 
“Hebu mjipange kuunda vikundi vitakavyoweza kuwasaidia kujiwezesha nyie wenyewe na hatimaye kujikwamua kiuchumi, kama mnavyofahamu ni vigumu kumuwezesha mtu mmoja mmoja  lakini ni rahisi kusaidia iwapo mtakua kwenye vikundi maalum, na hatimaye kufanikiwa katika kufikia malengo mliyoyakusudia” alisema Mbwilo.
 
Sambamba na hayo pia aliwataka waandishi wa habari kuhakikisha wanajituma katika kutafuta habari zaidi za wananchi wa vijijini,badala ya kusibiria kuitwa  kwenye ziara maalum,jambo ambalo linachelewesha wananchi kupata habari mbalimbali ambazo wangeweza kutarajia kupata.
 
Aidha alifafanua kuwa kalamu ya mwandishi wa habari ina uwezo wa kufika mbali kuliko kitu chochote, hivyo pia ina thamani kubwa sana kwa jamii katika kuwaletea maendeleo kwani ina uwezo wakuhabarisha, kuelimisha,kuburudisha na hata kukosoa pale inapohitajika.
 
“Hebu chacharikeni kujitoa katika kuwafikia wananchi kule vijijini ili kubaini mambo mbalimbali yanayowakabili, mara chache waandishi wa habari wamekua wakijitoa wenyewe katika kutafuta habari, wengi wao wamekua na tabia ya kusubiria kuitwa kwenye matukio makubwa, mimi ninachojua mwaandishi wa habari hasubirii kuitwa ambapo kufuatia hilo amewapongeza waandishi wa Mkoa wa Manyara kwa kuchacharika katika kutafuta habari mbalimbali “alisema Mbwilo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda