Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Thursday, December 6, 2012

Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Washirika wa NCA wafanyika TEC Dar es Salaam

Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Washirika wa NCA (Norwegian Church Aid-Annual Partners Consultative Meeting) unafanyika katika Kituo cha Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC) cha Kurasini ukijumuisha washirika mbalimbali wa NCA kutoka katika wilaya 43 nchini Tanzania.
Moja wa Washiriki akiongea wakati wa Mkutano wa NCA-APC 2012

Mkutano huo wa siku nne ulianza rasmi siku ya Jumanne tarehe 4 Desemba 2012 unahudhuriwa na jumla ya washiriki zaidi ya 100 kutoka kwa washirika wapatao 20 wa NCA, ukiwa na lengo la kuwaleta washirka wa NCA pamoja na kujua utendaji wa shughuli mbalimbali za mwaka na pia kukuza ushirikiano baina ya washirika hawa.
Washiriki wakiwa katika eneo la Maonesho la 4CCP ambalo limewavutia washiriki wengi sana
 Akiongea wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa APC, Mwakilishi wa NCA nchini Bi. Trine Thea alisema kuwa mkutano wa mwaka huu umevunja rekodi ya mahudhurio na tofauti kwani mwaka huu idadi ya washiriki imeongezeka sana jambo linaloonesha ukuaji wa shughuli za NCA nchini. 

Tofauti na Mikutano iliyopita ambayo imekuwa ikihudhuriwa na waratibu wa programu yaani Program Coordinators, Mkutano wa mwaka huu kwa mara ya kwanza umejumisha pia wahasibu na wasimamizi wa fedha wa washirika (Partners) kwani wao ni sehemu muhimu katika utekelezaji na kufanikisha shughuli zinazotekelezwa na kuwawezesha kufahamu kwa undani shughuli haswa zinazofanywa na Waratibu wa Programu na wamekuwa na semina yao kuhusu Mikataba inayosainiwa baina ya NCA na Washirika (partners), Usimamizi wa fedha katika uongozi wa miradi (Role of Finance in Project Management), Kupitisha na Kuhifadhi kumbukumbu za matumizi (Expenditure Authorization and Documentations) na kuandaa taarifa ya fedha ya mwaka (Preparations of Annual Financial Statements)
Mavazi ya Asili katika "banda" la Maonesho la 4CCP
Aidha katika mkutano huu pamoja na washirika wa NCA kutoa taarifa za shughuli mbalimbali wanazofanya katika maeneo yao, pia mada mbalimbali zimekuwa zikitolewa na kujaadiliwa na washiriki na pia kuna maonesho (Exhibition) ya huduma mbalimbali wanazotoa washiriki ambapo washindi wa maonesho hayo watapewa zawadi ikiwa ni pamoja na Mshiriki bora.

Kama wadau na washirika wa NCA, Programu ya Pembe Nne za Utamaduni Haydom yaani Haydom Four Cornrs Cultural Program (4CCP) inashiriki mkutano huu na kuwasilisha shughuli mbalumbali ilizozifanya kwa mwaka 2012 ikiwa ni pamoja na Kutoa elimu ya Haki Ardhi, VICOBA, Udhibiti wa Mabadiliko ya Tabia ya Nchi (Climatic Changes Mitigation), PETS na kujenga mahusiano baina ya jamii za Haydom ambazo zina historia, tamaduni tofauti na wakitofautiana jinsi wanavyotumia rasilimali zao hasa suala la Ardhi. Vile vile 4CCP inashiriki katika maonesho na maonesho ya 4CCP yamewavutia washiriki wengi hasa kwa kuwa ni tofauti na mengine kwa kuwa na vitu vya asili kama mavazi, vifaa na pia filamu inayoonesha historia, maisha na hatma ya jamii za Haydom.
Meneja Miradi wa NCA mama Tina Mosha (aliyesimama) akiteta jambo na Mratibu Msaidizi wa 4CCP Elimanata Awet na Kulia ni Nelson Faustin

Baadhi ya mada zilizowasilishwa ni pamoja na Thamani ya Hela (Value for Money) iliyowasilishwa na Helpage Internation, Mabadiliko ya tabia ya nchi, Peace Building and Interfaith, Gender Based Violance (GBV), Livelihood and Trade ambazo zimewasilishwa na wadau mbalimbali kama Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC), TEC, Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), BAKWATA, Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (ELCT) na washirika wengine.

Mkutano huu unatarajia kumalizika tarehe 7 Desemba 2012 tayari kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za mwaka 2013.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda