Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Wednesday, December 19, 2012

Mkoa wa Manyara kuandaa Kongamano la Fursa za Uwekezaji Manyara

Mkoa wa Manyara una mpango kabambe wa kuandaa kongamano kubwa  la wadau  wa maendeleo wenye lengo la kutangaza fursa mbalimbali za uwekezaji zinazopatikana katika mkoa huo mara ifikapo january 18, mwakani (2013) likiwa na lengo la kuuendeleza mkoa huu, ambapo amesema bado uwekezaji ni mdogo ukilinganisha na fursa zilizopo.
 
Mkoa wa Manyara licha ya uchanga wake lakini una rasilimali  nyingi ambazo hazijaendelezwa, ikiwa ni pamoja na ardhi, inayofaa kwa matumizi mbalimbali, maliasili (misitu, wanyama pori, maziwa, mito na milima) aina mbalimbali ya madini  na watu walio tayari kufanya kazi kwa bidii.
 
Akiongea jana na waandishi wa habari ofisini kwake Mkuu wa Mkoa wa Manyara Bw. Elaston Mbwilo alisema kuwa  mkutano huo utawahusisha watu mbali ikiwa ni pamoja na viongozi wa chama na serikali, wafanyabiashara wakubwa kutoka kila Wilaya.
 
Bw.Mbwilo alisema Kongamano hilo litafanyika January 18, mwakani 2013.likiwa na shabaha ya kuwatafuta wazawa (wana) Manyara waliotoka nje ya hapo ili waweze kurudi na kuwekeza katika mkoa wao wa manyara, ikiwa na malengo mbali mbali ikiwa ni pamoja na kujadili kwa pamoja fursa  fursa zilizopo  katika mkoa wao.
 
“Kusaidia kuweka uelewa wa pamoja wa viongozi wa serikali  na wananchi  juu ya jambo hili ,ili wakawaelimishe  na kuwahamasisha  wananchi katika maeneo yao  ili kuweza kufikia lengo tulilolikusudia kikamilifu”alisema Mbwilo.
 
Akifafanua malengo mengine ya mkutano huo mkubwa alisema kutangaza fursa hizo  kwa wawekezaji  wa ndani na nje ya mkoa ,kujiandaa Kimkoa kushiriki katika mkutano wa kanda ya Kaskazini unaotarajiwa kufayika mwezi Mei mwakani 2013.
 
Aidha lengo la mkutano huo wa kanda ya kaskazini ni  kutangaza kwa pamoja fursa zilizoko katika mikoa hiyo ya kaskazini “hii ni njia ya pekee ya kuwavutia  wawekezaji wa ndani na nje ya nchi  kuja kuwekeza katika kanda hiiz’alisema Mbwilo.
 
Akifafanua  fursa za uwekezaji  na hali ya uwekezaji  katika mkoa huo, Mkuu wa Mkoa huyo alisema katika miaka10 iliyopita , kumekuwa na uwekezaji mkubwa katika ikiwa ni pamoja na uchimbaji madini ya tanzanite,kiwanda cha mbolea cha Minjingu,kiwanda cha  kusindika sukari kilichopo kiru mjini Babati,.
 
 
“Sekta nyingine ni sekta ya fedha  hususani mabenki  na wakala wa kampuni za bima  na katika sekta ya ujenzi (construction) ambayo inakua haraka hasa katika mji wa Babati, ambapo nyumba zinazojengwa ni kwa matumizi ya ya hoteli,nyumba za kulala wageni, nyumba za kuishi na za biashara”alisema Mkuu huyo wa mkoa.
 
Aidha kumekuwepo na uwekezaji katika viwanda vodogo vidogo hususani kusindika mafuta ya alizeti Katika mji wa Babati, kiwanda cha kusindika maziwa  na nyama kilichoko wilaya ya simanjiro na katika kilimo.
 
Alisema uwekezaji huo bado ni mdogo ukilinganisha na fursa zilizopo kwani Mkoa wa Mnyara una rasilimali  nyingi ambazo hazijaendelezwa,ikiwa ni pamoja na ardhi,inayofaa kwa matumizi mbalimbali,maliasili,(misitu,wanyama pori,maziwa,mito na milima )aina mbalimbali ya madini  na watu walio tayari kufanya kazi kwa bidii.
 
 “Rasilimali hizi zinaufanya mkoa kuwa na fursa mbalimbali za  uwekezaji,fursa zipo katika sekta zote hususani sekta za kiuchumi,(kilimo,mifugo,maliasili,utalii,madini,viwanda na biashara), huduma za kijamii (elimu,afya na maji) na michezo ,hivyo kuna kila sababu ya kuwakaribisha wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuja kuwekeza katika mkoa wetu wa manyara” alifafanua Mbwilo.
 
Akielezea baadhi ya matarajio ya miaka  kumi (10) ijayo alisema ni pamoja na matarajio makubwa ya kuimarisha na kukuzxa uchumi kupitia sekta ya kilimo, mifugo, maliasili zilizopo, ardhi viwanda na biashara.
 
Alisema miundombinu ya barabara, nishati na mawasiliano itaendelea kuimarishwa ili kufungua sekta za uzalishaji ziweze kutoa mchango wake kikamilifu.ikiwa ni sambamba na kuendelea kuboresha  huduma za kijamii  kwa kuongeza bajeti inayotengwa na kushirikisha wadau mbalimbali .
 
Hata hivyo alisema ili kufanikisha azma hiyo mkoa utaendelea kutangaza fursa zilizoko katika mkoa kwa njia ya machapisho na mikutano mbalimbali ya wadau,ambapo alizitaka taasisi, mashirika na watu binafsi kuja kuwekeza katika sekta za kuichumi na kijamii.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda