Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Wednesday, December 19, 2012

Halmashauri Hanang yalipa Madeni

Halmashauri ya Wilaya ya Hanang’ Mkoani Manyara imetumia zaidi ya mil.150  kutoka kwenye makusanyo yake ya  ndani  kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo  ikiwa ni pamoja na kulipa malimbikizo ya madeni mbalimbali katika kipindi cha mwezi Julai hadi Septemba mwaka huu.
 
Hayo yalielezwa na Mkurugenzi mtendaji wa Halamashauri ya Wilaya ya Hanang’  Mkoani Manyara,Bw.Felix Mabula  wakati alipokua kwenye kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo.
 
Bw.Mabula alisema  Halmashauri hiyo imetumia jumla ya sh.152,738,566.7 kwenye shughuli mbali ikiwa ni pamoja na kulipa malimbikizo ya madeni kwa watumishi wa ngazi ya kata na vijiji ambapo sh.mil.20 zilitumika kuwalipa watumishi kama fedha za uhamisho, matibabu, gharama za mafunzo(masomo), pamoja na posho za kujikimu.
 
Aidha alifafanua kuwa sh.mil.67.9 zilitumika katika kuwalipa wananchi wa Bassotu fidia mara baada ya kuchukuliwa maeneo yao na halmashauri hiyo kwa lengo la ujenzi wa taasisi kama mahakama, hospitali, shule na masoko.
 
“Kama mnavyofahamu sh.mil.20 pia Halmashauri yetu ilitumia katika kuchangia shughuli za miradi ya maendeleo (cofunding) ndani ya wilaya yetu”alisema Bw.Mabula mbele ya baraza hilo la madiwani.
 
Alisema ndani ya hizo sh.mil152, sh.mil19.2 zilikwenda  kwenye serikali ya kijiji na kata  ikiwa ni asilimia 20% ya sehemu ya mapato yao ya ndani,ambapo halmashauri hiyo  ilifanikiwa kuondokana na deni la sh.mil  15.5  kwenye mfuko wa mikopo wa serikali za mitaa .
 
 
Aidha Bw.Mabula alisema kuwa Halmashauri yake imechangia kiasi cha sh. mil. 10  kwa ajili ya mfuko wa wanawake na vijana, ambapo alisema fedha hizo zote zililipwa kati ya kipindi cha mwezi Julai hadi Septemba mwaka huu ikiwa ni makusanyo ya vyanzo vya ndani ya halmashauri hiyo.
Hata hivyo pamoja na mambo mengine Mkurugenzi huyo aliwataka wataalam wa halmashauri hiyo kuacha tabia ya kuwaingilia  wakandarasi ili kuepuka baadhi ya mambo yanayoweza kujitokeza.
 
“Jamani wakandarasi wasiofikia viwango sisi huku hatuwataki kabisa na nyie wataalam msiwe sehemu ya majibu ya wakandarasi  kwani mtaweza kusababisha shughuli zikaenda kinyume na inavyotakiwa waacheni wenyewe msiwaingilie “alisema Bw.Mabula

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda