Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Monday, November 12, 2012

YANGA DAIMA NI MBELE, NA NYUMA KWETU NI MWIKO

Na Dr Beatus Chrisostomus Chikoti

Ilikuwa Septemba, siku ya kumi na tano,

Magazeti yalipamba, kuanza mtifuano.
    
Timu zote zilitamba, zitashinda michuano,
Mtetezi kajigamba, ataendeleza tano.

Kikapulizwa kipenga, fahari wakaumana,

zikapigwa sana chenga, na magoli kufungana.

Uwanja wa Sokoine, ndiko walikoianza,

eti mzungu wa nne, na watu wakawabeza.

Nazungumzia Yanga, walipoipata sare,

kila mtu kawazonga, eti wanacheza shere.

Baada ya siku nne, wakapigwa tatu Moro,

watani wapongezane, eti Dar mpaka Moro!

Na kama ilivyo ada, kwa mwanaume wa kweli,

kusaka jibu ibada, kwa yanayomkabili.

Wakatolewa mhanga, baadhi ya viongozi,

likamshukia janga, na Thomas mkufunzi.

Akaletwa mpya kocha, nae timu kaisuka,

akaziba zote pancha, na nidhamu wakashika.

Ushindi ukashamiri, vichapo vyatamalaki,

walojifanya jasiri, wakatandikwa mikuki.

Wimbi likaendelea, amani ikarejea,

japo ilitiwa doa, kagera kwa wana miwa.

Wakati hayo yajiri, kwetu sisi wenye nia, 

mambo yalikuwa shwari, kwa tunaowatania.

Wakaianza kwa kasi, ligi kuu Tanzania,

kama upepo wa kusi, ligi wakaipania.

Kama jiwe la manati, baruti wakafyatuka,

kama Usain Nati, kijana Mjamaika.

Mita mia walidhani, kumbe pumzi hawana,

hizi mbio marathoni, zataka mbinu mwanana.

Ujanja wao jijini, nje ya jiji vilaza,

wakienda mikoani, kupata sare kashinda.

Sare zikatamalaki, kama nne mfuatano,

na kuja kutahamaki, tuko mgongoni njano.

Mtibwa wakatamiwa, wakazindua utamu,

na Yanga tukanogewa, ligi twashika hatamu.

Toto wakagongelea, msumari kidondani,

na yanga waogelea, kwa nafasi kileleni.

Yanga daima ni mbele, nyuma sio lengo letu,

tusikiache kilele, tulinde umoja wetu.

PONGEZI WANA YANGA WOTE KWA MSHIKAMANO ULIOTUFIKISHA HAPA.

UDUMU HADI DURU LIJALO TUREJESHE KOMBE NYUMBANI.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda