Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Thursday, November 15, 2012

Wazee Magugu Walalamika kulishwa Viporo

Na Mary Margwe, Babati
Wazee wanaolelewa katika kituo maalum cha kulelea  wazee wasiojiweza chini ya Wizara ya Afya, kilichopo katika Kijiji cha Sarame Kata ya Maguu, Mkoani Manyara, wamedai kuwa wanalazimika kula chakula kilichopoa (kiporo) kwa kisingizio cha  kukosekana (uchache) wa wahudumu kituoni hapo, ambapo wamedai viporo vinawajaza matumbo.
Waandishi wa Habari wakiongea na bibi .Khadija Omary (105) kulia anayelelewa katika kituo cha kulelea wazee,  kilichopo katika Kijiji cha Sarame Kata ya magugu  Wilayani Babati, mkoani Manyara, chini ya Wizara ya afya,  akimenya karanga,  ambapo debe moja analipwa kiasi cha sh.500, amedai kuwa hiyo fedha inamsaidia katika kununua dagaa, mchicha ama nyama, kwa kile alichokidai kuwa kituo hicho wanapikiwa naharage kila wakati huku yeye amedai kutotumia na kusema yanamjaza tumbo.(Picha na Peter Ringi)
 Hali hiyo imebainika jana wakati wa ziara maalumu  ya waandishi wa habari wa Mkoa wa Manyara, mara baada ya kupatiwa mafunzo maalum ya uandishi wa habari za Vijini, waliotembelea kituoni hapo na kujionea hali halisi ya wazee hao ambapo wazee hao wameiomba Wizara ya Afya kuhakikisha inaboresha hali halisi ya chakula katika kituo hicho, hasa ukizingatia kuwa kituo hicho kipo chini ya Wizara hiyo ya Afya.
Wazee hao wamedai  kuwa, baadhi yao wanalazimika kula milo miwili  ikiwa ni asubuhi na mchana tu, badala ya mitatu kama ilivyo kawaida, kwa kile walichodai kuwa jioni wanashindwa kula chakula kilichopoa maarufu kwa jina la “kiporo” kutokana na hali halisi yaliyonayo ya kutokua na meno.
Akiongelea hali halisi ya maisha ya wazee kituoni hapo, mmoja wa wahudumu muuguzi wa Afya kituoni hapo Bi. Doska Luka, alikiri kutokea kwa hali hiyo na kusema kutokana na uhaba wa wahudumu, “asubuhi muda usiozidi saa 2:00  tunawapikia uji, mchana tunawapikia ugali, kwa kuwa wahudumu tuko wachache mchana kunapika chakula cha moja kwa moja hadi jioni ambapo wanakula chakula kilichopoa (kiporo).” alisema Bi. Luka.
Bi.Luka alisema wengi wao usiku wamekua wakishindwa kula chakula hicho kutokana na ubaridi wa chakula husika, kwa kile alichodai kuwa kituo hicho kina uhaba mkubwa wa vyombo vya vya kutosha ikiwa ni pamoja na vyombo kuhifadhia chakula ili kisipoe (hotpot) na hivyo kupelekea kupata malalamiko mengi toka kwa wazee hao.
  Alisema hali halisi ya kituo hicho kilichopo ndani ya Wizara ya Afya, Bi.Luka  alisema kama inavyoeleweka kwa walio wengi wazee wengi wanakua na tabia mbalimbali kama wengine kukataa kuoga lakini iwapo chakula kitakua chamoto kila mtu anapenda kula basi ndivyo hivyo na wao wanahitaji kula hivyo na si vinginevyo kama ilivyo hivi sasa.
Akielezea changamoto kinachokikabili  kituo hicho alisema ni pamoja na uhaba wa vyombo vya kulia chakula, chakula cha kubadilisha badala ya ugali kila siku, mahitaji ya  vitanda  20 kwani vilivyopo kwa sasa ni chakavu .
Alisema changamoto kubwa ni maji ambapo  huwa wanategemea zaidi kuvuna maji ya mvua, jambo ambalo amesema wamekua wakitembea umbali wa km.3 hadi kufika  mji mdogo wa Magugu kwa ajili ya kufuata maji.
Hata hivyo alifafanua kuwa kituo hicho kilianzishwa mnamo mwaka 1975 ambapo kina wazee wapatao 13 na watoto wapatao 7, na kupelekea jumla ya watu 20, wanaokitegemea kituo hicho.
Naye Bi.Khadija Omary (105) ambaye alisema alitokea Kijiji cha Gumanga Mkoa wa Singida alisema ni vema ndugu zao wawe wanawatembelea ili kubaini baadhi ya kero ndogondogo zinazowakabili, ambapo kwa upande wake analazimika kufanya kazi ya kubangua karanga ambapo kwa debe moja analipwa ujira wa sh.500 ili kuweza kupata fedha ya kununulia mboga nje ya maharage ambayo yamedaiwa kuliwa kila siku, abapo kwa upande wake amedai yanamjaza tumbo.
Hata hivyo kufuatia changamoto hizo wazee hao wamefurahishwa na kitendo cha waandishi wa habari kuwatembelea kituoni hapo na kupata nafasi ya kutoa kero zinazowakabili na kuiombaWizara ya Afya kuhakikisha kuwa inawakumbuka katika kuwapelekea mosaada mbalimbali ikiwa ni pamoja na wahudumu ili waweze kula chakula chamoto kama wanavyokula wananchi wengine wa kawaida.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda