Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Saturday, November 3, 2012

Ulemavu Kwake Si Hoja, Mungu Alijua kwa nini ndo mana Akampa kufanya haya...,Wewe na Mimi Tunajifunza nini toka kwake??....


Na Nelson Faustin,
Naivasha-Kenya.
Source: http://www.bbc.co.uk/swahili/medianuai/2012/10/121029_ulemavu_ipalei.shtml
 http://ipalei.tvheaven.com/

Kwaajili ya sifa na utukufu wa Mungu, japo watu wanasema hujafa hujaumbika lakini kwa Godfrey Ipalei mwenye umri wa miaka 44 hana mke na anishi peke yeke lakini anajifanyia kila kitu mwenyewe licha ya ulemavu wake wa kukosa nusu ya mikono yoye miwili yani viganja vyote viwili vinavyoufanya mkono uwe na maana kubwa ya utendaji, lakini kauli ya hujafa hujaumbika ni tofauti kabisa kwani anaamini hii ni hali ambayo utukufu wa Mungu ulimfanya awe kama alivyo na wala hana tatizo na hali hii zaidi sana anakila sababu ya kumshukuru Mungu na
kufanaya kila kila kitu bila kujilaumu, kusingizia wala kutegemea kuwa, he can't do something simply because he is hand caped.


Katika hali ya kawaida, wewe na mimi lazima tujiulize, kwa nini kuna vitu ambavyo hatuwezi kuvifanya wakati kuna walemavu wanaweza kuvifanya?? Si kazi nyepesi sana kupambana na  hali ya kuwa na ulemavu lakini wapo wanaoweza kupambana na hali hizo na zaidi sana kubadilisha maisha yao.


Si hivyo tu embu tuangalie kwa ufupi mambo ambao Godfrey huwa anaweza kuyafanya bila wasiwasi wowote kitu ambacho humfanya aseme kuwa, "Ulemavu si Hoja kwangu", baada ya hapo tufanye tathmini ya niini tunafanya kama watanzania katika kubadisha hali zetu za kimaisha??? Lazima kwa pamoja tufikiri na kujiuliza, licha wa walemavu hata watu wa kawaida katika nchi yetu ya jirani ambayo kwa sasa tunahofia kufungua boda kwani watatupita gap, sisemi kuwa hapa kwetu hawapo wakufanya mazuri zaidi yao lakini tuweke mambo wazi tu ni kwamba, hawa wenzetu wamatupiga gap na tunahitaji kukimbia wakati wenzetu wanatembea.


Gody anweza kufanya mambo mengi sana yakiwemo, kuongea na simu bila wasiwasi wowote tena black berry, kutumia computer bila wasiwasi kabisa, kupika kwa ustadi mkubwa, kujifanyia usafi wa mwili na kuvaa vizuri tena suti, zaidi sana ameandika kitabu kinachoitwa, "Mlemav? Si mimi."  ambacho kimechapishwa na Oxford Press ili kuwasadia wale wotea ambao ni walemavu wabadili mitazamo yao juu ya ulemavu wao. Ni mwalimu wa kompyuta na anafundisha vizuri sana. 

Hoja za msingi, 
  • Wewe kama ni mlemavu wa viungo, umeamua kufanya nini na ukashindwa?
  • Je, Ulemavu wako ni hoja ya kukufanya kuwa ombaomba?
  • Ewe ambaye ni mzima, umewasaidia walemavu wangapi kujua kujitegemea au umewonesha kuwa hawawezi?
  • Mangapi ambayo wewe na mikono na miguu yako na uzima wako wote umeshindwa kufanya lakini wenzako tena walemavu wameweza?
  • Kwa Tanzania, wangapi ambao ni walemavu na kwa sasa bado ni wategemezi japo ulemavu wao si severe kama wenzetu?
Siwasemi walemavu vibaya, lakini ni changamoto tu kuwa, kila kitu kinawezekana labda kwa wale ambao hawawezi kabisa, hao wasamehewe lakini kuna ambao wamechukulia hili kama ni tatizo kubwa sana na hawawezi tena. Big up kwa ndugu zangu walemavu ambao bado wanapambana kutokana na ulemavu wao baldo waafanya mamabo mengi ya kujikwamua kiuchumi. Japo ulemavu unatofautiana lakini kama wewe au ndugu yako ni mlemavu wa aina ambayo inaweza ikavunilika na kufanya kitu, basi tutiane moyo na kufanya kazi kwani ni njia ya kufanya maisha kuwa na umaana zaidi.


Take the challange.
Wenzetu wanasema, Ipalei has proved Disability is not Inability, they can also do it...mimi nauliza, How many can do it like them?


And how do you manage? It is easy friends, you just have to dare.


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda