Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Friday, November 2, 2012

Ukishindwa Kuchukuliana na Flegmatics, You are a Complex Human Being, Work on It, Unlessotherwise The World Shall Turn a Hell to You.Na Nelson Faustin.
Best Wishez Bro. Obama.
Tunaposhangaa kwa nini watu wanashindwa kuishu na Flegmatiki type of a Human Being ni kutokana na kwamba, hii ni haiba pekee ya watu ambao japo kidogo wanakiburi lakini "they have a listening Ear", hata ukiwa ni mgumu kiasi gani, hawa watakuwezesha kuwaelewa na kuishi nao, lakini ukiona huwezi kuishi  nao kabisa na hata usaidiweje hutaweza kuishi nao, basi wewe ni a complex human being na unahitaji sana ukaribu wa mtu wa kuku saidia au uamue kuchukua jukumu la kujikubali na kubadilika. Ni rahisi sana kwa sangwini kubadilika na kuishi na flegmatiki lakini ni ngumu sana kwa  Koleriki na Melankoli kubadilika kama akiamua kutokubadilika. 

Tule pamoja Mana-Thanks
Mara nyingi Flegmatiki ni msaada wa pekee sana kwa Koleriki na Melankoli kwani ni wepesi sana kufanya mambo yanayoumiza wengine lakini flegmatiki yupo kwaajili ya kuyaponya makovu hayo kutokana na sauti yao ya upole. Kama kwenye mahusiano mmoja ni flegmatiki na mwingine ni Koleriki basi ujue hapo kama flegmatiki ni mkaka na mdada ni Koleriki ujue basi huyo mkaka anakazi ya kupoza kila pain ambayo mwandani wake anasababisha, na kama makaka akibahatika namna ya kuchukuliana na huyu mdada kisaikolojia they will never part, lakini kwa experience yangu ni kuwa, relationship nyingi hata baina ya ndugu zinavunjika si kwamba watu hawapendani bali tu wameshindwa kuelewana na kuchukuliana.

Flegmatic Asiposema-Analia.
Tumalizie kwa kuangalia zile njia zilizobaki za namna ya kuishi na Flegmatiki bila ya kumsababishia maumivu. Ishu si kuishi tu bali ni kuishi kwa kukubalika na jamii bila tatizo. Najua si rahisi sana kuwa na maisha ambayo ni smooth, ila kila mmoja anapaswa kufahamu kuwa "kila mmoja wetu ana kazi ya kumsadia mwenzake ili kufanya maisha yaende.
 • Unatakiwa kuwa na utulivu unapohusiana nao. Si watu wa kujitoa kwa ukamilifu katika mahusiano na hivyo inasababisha watu kuona hakuna "special touch", lakini ukiwapa nafasi ya kuweka hisia zao vizuri, utafurahi sana.
 • Jitahidi sana kuwaamini na kujiamini unapokuwa nao, usikubali kuwaonesha kuwa huwaamini bali wape nafasi ya kukuona kuwa wewe ni tegemeo na hata wao wanakitu cha kufanya.
 • Usiwakasirishe kwani wakikasirika, ni ngumu sana kuwatuliza. Fanya kila njia kuwaweka katika mazingira ya kutokukasirika, na ukiona hawakasiriki basi usishinikze kukasirika kwao.
 • Mpongeze ili awe na ujasiri wa kufanya vizuri zaidi, hapa unawapa nafasi ya kuweka aibu pembeni kwani aibu huwafanya wasifanye mambo mengi.
 • Kama kuna kitu  kitaleta mabadiliko, basi waambie mapema ili wajiandae kwa kupamabana na hali yao ya kutokupenda mabadiliko ili mabadiliko yatakapotokea basi waweze kukimbizana na mabadiliko hayo, kinyume na hayo utawaburuza sana.
 •  Thamani ya maisha yao ni muhimu sana, kwanza ile hali yao ya usafi ipo ndani na nnje, katika kuhusiana nao, wape heshima yao kwa kuheshimu mawazo yao, kusema kwao kwa upole kunafaa sana kama utawasikiliza.
 • Jitahidi kuwa mkarimu kwao. Ni watu ambao, hata siku moja kama wanashida si watu wakusema, ikitokea umemfahamu Flegmatiki, basi tumia nafasi hii kuwapa kile unachodhani kuwa wanakihitaji hata kama hawajaomba.
 • Ewe unayefahamu kuwa wewe ni Koleriki, jittahidi sana kutokuwaburuz, ukiwaburuzwa huwa wanakinai mazingira na ukikaa vibaya watakukinai na wewe mwisho wa siku watakuwa na kiburi kisichoisha. 

Hadi hapo, tumefikia mwisho wa  masomo haya kila moja kwa nafasi yake. Sasa kuanzia wiki ijayo tutajifunza masomo yafuatayo.
 1. Namna ya kuboresha ujuzi wako wa Haiba, How do you edit your negatives.
 2. Je, Unaweza kubadili Haiba yako?
 3. Can you change someone's Behaviour/personality.
 4. Kwa nini TUNAKWAZANA  kutokana na utofauti wetu wa Haiba?
 5. Je, Kuna faida yeyote ya kufahamu tabia yangu? Na je, ni dhani kujibiisha katika kujibadilisha for others.
 6. Je, kuna kazi za aina gani kwa kila kundi?
 7. Mimi ninamchanganyiko wa Hulka/tabia, Nifanyeje?
 8. Nataka nifahamu tabia ya mtu kwa muda wa Sekunde tano, Nafanyaje?
 9. Mahusiano yachague Hulka? Shall I marry my fellow Sangwine? e.t.c
 10. Je hulka za wanaume na wanawake zinatofautiana??
Na mengine mengi, ni somo ambalo kama huna haja ya kuishi maisha yenye utoshelevu, basi hulihitaji, lakini kama unataka kuishi maisha yenye utoshelevu, basi  jitahidi upate elimu hii, tunakupa bure lengo letu ni kufanya maisha mahali mazuri pa kuishi. Sisi sote tunahitahi elimu hii, kama kila mtu akiipata, basi tutaishi vizuru sana. Upatapo mawaidha haya, basi wajullishe na wengine.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda