Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Friday, November 16, 2012

The story of my hero, my role model and a true legend

I WAS TO POST THIS LAST FRIDAY BUT.........IT'S NOT TOO LATE
Mwaka 1999 wakati nipo kidato cha kwanza, akiwa anaumwa sana (unaweza kugoogle huu ugonjwa SYSTEMIC SCHLERODEMA) huku akiwa ni mwalimu wa shule ya msingi Endaharghadatk, alifanya mtihani wa kidato cha nne kama Private candidate. Baada ya kumaliza mitihani miwili ya English na Kiswahili akiwa anajiandaa kuingia kwenye mtihani wa Geography akapata taarifa kuwa wezi wamevamia nyumbani na kuiba ng'ombe na kwa kuwa nyumbani alikuwepo mama tu ilibidi asiendelee na mtihani arudi nyumbani.
Baada ya matokeo kutoka, kwa yale masomo aliyoyafanya "He did wonders". Alikuwa private candidate pekee wilaya ya Mbulu kupata A, alipata A ya English, B ya Kiswahili na D ya Geography.
This is the story of my hero, my role model and a legend. Wiki chache baada ya kuzaliwa aliianguka motoni na kuungua vibaya kichwani (kisogoni) na alipona kimiujiza baada ya kuuguza jeraha kwa muda mrefu, hakuna aliyetarajia kuwa angeweza kupona. Baada ya kumaliza darasa la 8 wakati ule Dongobesh Middle School, alichaguliwa kujionga na shule ya Sekondari ya Ufundi Moshi lakini kwa kuwa alikuwa mtoto wa mwisho wa kiume, mama yake alimfuata na kumtoa shuleni kuwa tofauti na kaka yake ambaye naye alichaguliwa kujiunga na shule ya sekondari ya Ilboru iliyopo Arusha, yeye alitakiwa abaki nyumbani na kama taratibu za kimila ndiye atakayebaki na wazazi nyumbani. Hakuwa na la kufanya bali akatii amri ya mama yake ambaye alikuwa mkali kupindukia.
Baada ya kurudi nyumbani kwao Injur nje kidogo ya Haydom, akapata kazi ya kibarua katika Hospitali ya Wamisionari iliyopo Haydom (Sasa ni Haydom Lutheran Hospital) na kufanya kazi kwa miaka kadhaa na baadaye akaomba kwa siri kujiunga na chuo cha Ualimu Korogwe. Baada ya kuhitimu hapo ikabidi aombe apangiwe karibu na nyumbani ili walau atulize hasira za mama yake. Akapangiwa shule ya msingi Hayloto na baada ya muda akawa mwalimu mkuu wa kwanza wa shule ya Msingi Endaharghadatk.
Pamoja na kuwa katika mazingira ya kijijini lakini "he was well informed", alikuwa na maktaba iliyojaa vitabu vya kila aina hivyo kuwa na upeo mkubwa sana zaidi ya watu wote waliokuwa wanamzunguka. I was privileged kukulia katika mazingira hayo kwani aliniambukiza kupenda kusoma hata kabla sijaanza shule ya msingi, nilianza shule nikiwa najua kusoma na kuandika na tofauti na watoto  wengi kijijini ambao huanza darasa la kwanz wakiwa na miaka 11 hadi 13, nilianza shule nikiwa na miaka 7. Alikuwa mbunifu na siku zote aliwaza miaka mingi mbele, alikuwa mtu maarufu sana katika wilaya nzima ya Mbulu japo alikuwa mwalimu tu. Alikuwa mwalimu, mtafiti na mwanamichezo, hadi dakika ya mwisho hakuacha kufanya kazi na ameacha "legacy" kote alikopita na dhahiri ni kazi kubwa sana aliyoifanya katika kuanzisha kituo cha utamaduni Haydom (4CCP. Ni ukweli usiopingika kuwa mawazo na mwongozo wake vilikuwa msingi wa kituo hichi, japo hajaweza kuona matunda yake lakini naamini alipo anajisikia fahari kwa kazi aliyoifanya. Kila shule aliyofundisha ilipata mafanikio makubwa sana kimichezo na kitaaluma hasa katika kata za Maghang na Maretadu. Akiwa Maretadu alikutana na swahiba wake mwalimu Francis Amnaay ambao kwa pamoja waliibadili kata hiyo changa wakati huo na miaka michache baada ya kuondoka, kama ilivyo kwa kata ya Maghang, nayo ikafa ghafla.
Mwaka 1993 alianza kuugua ugonjwa ambao kwa wakati ule haukufahamika na hivyo kudhoofu sana na mwaka 1998 ndipo ilipogundulika kuwa anaugua ugonjwa unaoitwa Systemic Schlerodema, ugonjwa ambao unasababishwa na mwili kutengeneza kinga ambayo inashambulia tishu na seli za mwili (Auto Immune), ugonjwa ambao hauna kinga wala tiba na namna pekee ya kupambana nao ni kujaribu kushusha kinga ya mwili jambo linalosababisha ashambuliwe na magonjwa mengine kirahisi.
Kwa miaka 17 alipambana na ugonjwa huo akiwa na imani na alitekeleza majukumu yake yote ipasavyo. Miaka ilivyozidi kwenda hali yake ilizidi kudhoofu hasa mifupa ilikuwa imelainika na kwenye joints zilikuwa zimesagika na kkungana hali iliyopelekea kufanyiwa upasuaji mkubwa wa nyonga (total hip replacement) na kuweza kutembea tena.
Lakini hali yake ilidhoofu sana na kulazwa katika Hopsitali ya Kilutheri ya Haydom kwa zaidi ya mwaka, na hatimaye kupewa rufaa ya kwenda Hospitali ya KCMC ambako alilazwa kwa mwezi moja. Kilikuwa kipindi kigumu sana kwangu, alikuwa kwenye maumivu makali sana na siku moja usiku majira ya saa 8 wakati wagonjwa wote wamelala aliniomba nimkalishe nitafute kalamu na karatasi niandike atakayoniambia. Nilidhani ni maigizo, "mwanangu nimepambana sana na sasa nimefika mwisho...................." aliongea mengi wakati huo nikilia machozi nisiamini kinachotokea. "Nimekwisha kulipa madeni yote hakuna mtu anayenidai" huku akiniambia watu anaowadai nifuatilie na kama hawaelewi niachane nao. Alimaliza kwa kusema "haya ni mambo ya kawaida na ni lazima yatokee, usiogope, be a man",, niliogopa sana, nilidhani usiku huo angelala moja kwa moja, lakini asubuhi akaamka amechangamka. Madaktari wakapita round, moja akaniita pembeni na kunieleza kuwa hawezi kupona, ugonjwa umekwisha athiri moyo, mapafu na figo na kunishauri nifanye mpango arudi nyumbani apate "paliative care"
Tukarudi nyumbani, tukakaa kwa wiki 3 hivi, jumatano moja akaniambia nirudi Dar nikaangalie shughuli zangu kwa kuwa nimekaa naye sana. Ilikuwa huzuni kuondoka na kumwacha, nilitaka niwe naye hadi dakika ya mwisho kumbe hakutaka nishuhudie akiondoka. Nilifika Dar jumamosi, nikakaa jumapili tu, jumatatu jioni nikajulishwa kuwa amezidiwa sana na alfajiri ya jumanne Tarehe 9 Novemba 2010 akamaliza safari yake humu duniani.
Amefanya mengi sana kwa ajili yangu, familia lakini kwa jamii kwa ujumla. Lakini jambo ambalo ni kubwa kuliko yote ni kuwa nina uhakika yuko mbinguni. Katika kipindi chote cha mateso yake hakuacha kumwita Mungu hasa siku za mwisho. Nakumbuka usiku wakati maumivu yamemzidi na dawa hazina msaada alinisihi tuombe na dakika 10 kabla hajalala aliomba na kisha kuwaambia waliokuwepo kuwa sasa nipo tayari. Saa moja kabla ya kulala hakuwa na maumivu na muda wote alikuwa akiimba nyimbo na kusali na hata saa yake ilipowadia alifumba macho na kulala.

Ni miaka 2 sasa, lakini bado siamini kama kweli hayupo. Alinipa mwongozo na dira ambazo ndizo zinazoniongoza leo hii. I wish to be just as good as half of him. He was the only person in the world who believed in me, he made me feel i can become anything i want to be, he made me a dreamer and do and think differently. I am who I am today because of HIM. I know wherever he is now, he is proud of me, sina deni moyoni na yote niyafanyayo ni kumuenzi yeye.

Kilikuwa kipindi kigumu sana, siwezi kuwasahau marafiki, ndugu na jamaa waliokuwa karibu na kutusapoti. Ninadeni kubwa sana kwa binamu yangu mpenzi Naomi, Shangazi, Wema, Fadhili na familia yao yote, Dr. Delfina Robert alikuwa nami muda wote, siwezi kumsahau, Walimu wote wa wilaya ya Mbulu hasa kata ya Haydom, Halmashauri ya wilaya ya Mbulu, Wauguzi na madaktari wa HLH hasa Old Ward na ICU. Siwezi kuwasahau Glory Membi na Pendo Satiel kwa kuwa nami kipindi chote alichokuwepo Haydom, Uongozi wa HLH, jamii nzima ya 4CCP hasa Anna Kari na Eliminata. Ole Bjorn Rekdal na Astrid Blystad, Dr. Yusufu Lawi wa UDSM, wafanyakazi, wauguzi na madaktari wa Mikocheni Mission Hospital, MOI hasa Dr. Mcharo. Marafiki zangu wa karibu Nelson Faustin, Gody Michael Rweyemam, Urio Aaron, Mwipa Anderson Kippa, Imani Robert n mdogo wangu Paschal Emmanuel kwa kuwa nami wakati akipata matibabu DSM na kutoa damu kwa ajili yake, marafiki wote waliokuja kumwona akiwa hospitali hasa Eppy Aloyce aliyekuja all the way hadi KCMC, wanaHaydom wote ambao siwezi kuwataja moja moja, marafiki zangu wote hasa GAIM na ambao hata hatujawahi kuonana wa Facebook. Najua njia hii haitoshi kuwashukuru na nina deni kubwa sana kwenu wote, sina namna kubwa zaidi ya kuwashukuru kwa niaba ya familia yetu. Shukrani za pekee ni kwa timu nzima ya The Bridge Ltd iliyonisapoti kipindi chote, nina deni kubwa sana kwa Gideon M Alfred, David Kagoma na Prosper Alfred Mwakitalima kwa kunisapoti kipindi chote. Zaidi ya yote ninamshukuru sana Mungu kwani hata katika mauti bado anabaki kuwa Mungu na ukuu wake unadhihirika.

There can be many with Phds but to me, he is the best, the best father anyone can dream to have, a best teacher any student can wish for, a mentor and above all the greatest friend. I haven't seen Jesus with my eyes but I know my dad, if Jesus was greater than him then Jesus is trully supernatural.
Dad, I love you and I miss you!
Thank you for the impact you had in my life!

Rest in Peace my Hero! RIP YESAYA GASERI
"A true champion is the one who fights until the last second of his/her life" 

6 comments:

 1. Ni story ya kweli amabayo inahuzunisha sana Amani, lakini pia inatufundisha sana..Really nimeingia katika uhusika wako pia na kufeel ulichokuwa unafeel... Nafikiri Mungu huwa na Makusudi yake.. believe it Mungu amempumzisha mahali pema ni jamabo la kujifunza jinsi ya kupambana na maisha in whatever circumstances.. Pole sana na Mungu awatie nguvu wakati wote .

  ReplyDelete
  Replies
  1. Thank you Robert, kwa Neema ya Mungu twasonga mbele na kuenzi yale aliyotuachia

   Delete
 2. A moving, well written,touching, and a must read story. It has given me a new perspective and a great lesson. Thanks for this and RIP YESAYA GASERI. The man i knew very well but only to know that he is no more after reading this- Two years now!

  ReplyDelete
 3. devotha john massayDecember 26, 2012 at 4:41 AM

  pole sana Amani, what you have written is true about your hero!, i know him very much, he was real a designer i found one of his letter with my father, it was very attractive which make any one who read it to laugh, because of his way of life when he was a life i also believe that he is now near by God and praying for you and his people in general, so what we are supposed to do is to ask him to pray for us

  ReplyDelete
  Replies
  1. Nashukuru Devotha, Nitafurhi nikiweza kuisoma hiyo barua hahahaaa kama siyo Confidential lakini

   Delete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda