Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Monday, November 12, 2012

Simanjiro yatakiwa kuweka mkakati wa kutoa tuzo kwa washindi bora wa kutunza mazingira


Na Mary Margwe-Simanjiro
   Uongozi wa Halmashauri ya Simanjiro Mkoani Manyara imetakiwa kuweka mkakati madhubuti wa kutoa tuzo kwa watu wanaoongoza kupanda miti ili kuongea hamasa kwa wananchi wanaotunza mazingira na hatimaye kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
 
Hayo yalisemwa jana na Brigedia Jenerali Kayombo alipokuwa akiongea katika  mji mdogo wa Mirerani kwenye mdahalo wa mabadiliko ya tabia nchi na namna ya kupunguza athari zake uliondaliwa na mtandao wa asasi za kijamii mkoani humo Macsnetna The Foundation for Civil Society.
 
Kayombo alisema ili kuhakikisha jamii inapenda kutunza mazingira kwa kupanda miti uongozi wa wilaya hiyo unatakiwa kujipanga kutoa tuzo kwa washindi wa upandaji miti ili kuongeza hamasa ya kutunza mazingira wilayani humo.
 
"Kila kitu  ni nia,uwezo na uamuzi, kwani ukiwa na nia ama uamuzi lazima mipango uliyojiwekea utaikamilisha tena kwa wakati ,hivyo Halmashauri Simanjiro hakikisheni suala hili ninakamilika haraka iwezekanavyo ili kuboresha mazingira yetu"alisema Kayombo.
  
Alisema mpango huo utakua endelevu ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi,ambapo alisema suala ambalo hivi sasa linazungumzwa na wasomi,wanasayansi,wanasiasa na jamii kwa ujumla, hivyo juhudi zinapaswa kufanyika ili kuhakikisha mabadiliko ya tabia nchi yanadhibitiwa.
 
“Tunapaswa kuhakikisha kuwa juhudi za makusudi,elimu na sera zinaendelea kutolewa kwa jamii kwani uelewa mdogo na dhamira ya wenye dhamana ni ya mashaka katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi hivi sasa,kwa kufanya hivyo tutafanikiwa kikamilifu na si vinginevyo,” alisema Brigedia Jenerali Kayombo.
 
Aidha mmoja wa watoa mada katika mdahalo huo, Bw.Jackson Muro alibainisha madhara ya mabadiliko ya tabia nchi  kuwa ni pamoja na ukame,magonjwa ya binadamu,mifugo,wanyama na mimea,mafuriko yasiyotegemewa,sunami  theluji kuyeyuka,kukosekana mvua na kina cha bahari au ziwa kupungua.

Alisema namna pekee ya kupambana na mabadiliko ya tabia nchi ni kutunza uoto wa asili ,kupunguza uzalishaji wa hewa na gesi,kupanda miti ili inyonye hewa ukaa inayopanda angani na kuchanganya mazao ya kawaida na misitu na si vinginevyo.

“Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na shirika la chakula duniani FAO mwaka 2005 ulionyesha kiwango cha ukataji misitu duniani umefikia hekta milioni 7.3 milioni kwa mwaka hivyo hewa ya ukaa kushindwa kufyozwa,” alisema Muro.

Naye,mmoja kati ya washiriki wa mdahalo huo,Bw.Kaanael Minja alimuuliza mkuu huyo wa wilaya kuwa nani anatoa kibali cha kukatwa mkaa wilayani humo kwani hivi sasa uuzwaji wa mkaa umeenea na hakuna hatua inayochukuliwa.
 
Hata hivyo,Brigedia Jenerali Kayombo alisema hakuna kibali kinachotolewa na mtu cha kukata mkaa kwenye wilaya hiyo,hivyo ushirikiano baina ya viongozi na jamii unahitajika uongezwe ili kukomesha hali hiyo kwani kijiografia Simanjiro ni kubwa. 
 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda