Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Tuesday, November 27, 2012

Papaa.....Kwanini Nisife Leo?? Candle In The Wind--2

Na Samuel Sasali a.k.a Papaa

Tunakila Sababu Ya Kumshukuru Mungu Kwa Ulinzi Wake na Fadhiri zake kwetu Kila iitwapo leo. Maisha tuliyonayo si yetu ila mwenye nayo anapotupa nafasi ya kuyatumia hatuna budi kumshukuru. Juzi kati tumepoteza Mcheza Filamu hapa Tanzania, Weekend Rafiki Yangu Niliyesoma nae Chuo na Kufanya nae Missions nyingi sana ndani na Nje ya Chuo, na Nakumbuka sana mwezi wa nne Nikiwa Dodoma alitafuta namna mpaka tukaonana Mr. Raphael Lyela amepoteza Mtoto Wake Mchanga kabisa, Jana tumepoteza Sharobalo nae ameenda unadhani nani anafuata??kwa taarifa yako ni wewe au mimi.

Wiki 3 zimepita nimekuwa Mwanza, Mbeya, Singida na Arusha ndani ya Muda Mfupi sana kwa kutumia usafiri wa Anga na Mabasi na kukutana na ajali nyingi sana barabarani na watu wamepoteza maisha, kutoka salama nyumbani ni neema kufika kule unakokwenda ni Muujiza maisha tumepewa mara moja tu kisha hukumu. Siku hizi nimesikia mtu akifariki tunaongea "Its too soon Jamaa ameondoka". Nikajiuliza Soon inaisha lini???. Kuna vifo vya uzembe kweli vinavyosababishwa watu kupoteza maisha yao, kuna vifo vya watoto wa changa chini ya miaka mitano, Kuna vifo vya Kujitakia mtu kuamua kunywa sumu ama kusukumwa na kupelekea brain Concussion lakini swali la kujiuliza sisi tulio wahi tunataka tuishi mpaka lini ili iweje??

Kati ya Mambo ambayo huwa yananipa hamasa kwenye maisha ni kila ninapowaza siku mwili wangu utakapokuwa unaingia Kaburini unataka watu waseme nini juu ya mimi. Huwa najiuliza what If Mungu angekuwa amemwambia kila mtu deadline ya maisha yake ni lini je angeishi vipi kuelekea kwenye deadline ya maisha??. Umewahi waza kuwa deadline ya maisha yako ni leo mwisho??Kama Mungu angesema kila mtu anakufa lini tarehe ngapi na mwaka gani nina hakika watu wengi sana wangebadilika kuelekea kwenye siku yao ya mwisho, kwa kuwa kufa ni siri ya Muumba basi ipo haja ya kila siku kujipanga kuwa duniani siko kwetu kuna mahali tunakwenda, na tunakokwenda inategemea sana na unavyoishi duniani. Kama Ukifa baada ya kusoma Papaa On Tuesday hii unahisi utaenda wapi?kwani hujui unatakiwa kwenda wapi??unajua sana unakotakiwa kwenda ukiwa na roho mbaya unajua kwenu ni wapi, Ukiwa na vitabia vyako vya Siri Unajua kwenu ni wapi, Ukiwa Mla Rushwa unajua kwenu ni wapi, Ukiwa Mtu mwema unajua kwenu ni wapi, Ukiwa Mcha Mungu unajua kwenu ni wapi, kama Mungu angekuuliza swali leo "Kwanini Nisikuchukue Leo ama Kesho Ungejibu nini"??Uendelee kuishi ili iweje??
Ipo haja ya Kukumbushana, duniani tumekuja kwa makusudi maalum na tuko kwa makusudi maalum, kuchagua kama kwenda peponi ama jehanum ni leo. Your Destiny Determined By Your Today's Decisions. Kuna Siku nikiwa kwenye msiba wa rafiki yangu nikiwa na huzuni sana sababu jamaa tulikuwa na issue tunataka kuiandaa baada ya siku chache zijazo jamaa akafariki, nilijawa na huzuni, nikiwa nawaza hapo ghafla wazo likanijia, "yamkini mimi nikafuata kesho". Watu tunaogopa kifo kweli tunaogopa lakini cha kujiuliza tunaogopa nini???umewahi jiuliza kwanini watu waka tayari kesho kwenda Ulaya Kuliko Mbinguni??Ili Mungu akuache duniani ulitimize Kusudi la wewe kuumbwa kwako Kuna maisha lazima uishi ukiwa hapa duniani na uimalize kazi yako kisha tuseme, Mwendo ameumaliza Imani Ameilinda. Wengi wetu sana Mwendo hatumalizi na Imani Tunaipoteza tunakosa Value ya Kuwa duniani.
Watakatifu na Wenye dhambi, Wenye haki na Waovu, wema na Makatili wote wanatamani kwenda Peponi ni ndio maana kila anayekufa utasikia watu wanasema "Weka Pema Peponi". Tiketi ya Kwenda Peponi inapatikana duniani hapa hapa, kama ambavyo Tiketi ya Ndege inapatikana kabla hujapanda ndege, ama basi. Haiwezekani ukishakufa ndo Tunampangia Dereva Sehemu ya kwenda. Kama kweli unataka Kwenda Peponi mbona Njia inajulikana. Siku Usije Ukasema Ulikuwa Hujui kama Kuna Kukata tiketi mapema wakati leo ninakukumbusha kuwa Safari yako ni Kesho Umejiandaaje???

Ni vema tukakumbushana kujipanga na maisha ya kila siku duniani, ni vema tukakumbusha kuwa na fedha na elimu na utajiri duniani lakini ni vema tukakumbushana pia kuwa leo yamkini ni siku yako ya mwisho kuishi duniani umejiandaaje huko unakotaka kwenda??Umewahi kuwaza kuwa Siku Ukifa Mumeo ama Mkeo atatunzaje watoto mlionao??umewahi kuwaza kuwa mumeo ama mkeo ataolewa ama ataoa tena??umewahi waza siku kuwa wazazi wako wanaweza kutangulia na wewe ndio ukabeba Jukumu la familia??Umewahi waza kuwa huo ujauzito ulionao mtoto anaweza akafariki wakati wa kuzaliwa basi ipo haja ya kujipanga kiroho na Kimwili. Ili Mwisho wa Siku Tusisumbue Maaskofu kumwelekeza Mungu kazi ya Kufanya Kuwa "Weka Pema Peponi"


Mwalimu Wangu wa Kujitolewa wa Saikolojia Chris Mauki aliwahi niambia Njia Mojawapo ya Kukabiliana na Stress ni Kujiandaa na tatizo kabla halijatokea ili linapotokea inakuwa ulishalitarajia kutokea. Niliwahi andika kwenye Papaa On Tuesday moja kuwa Ukiuandaa Moyo, Lakufika Likikufika unakuwa na amani...gonga hapa kama hukusoma....http://samsasali.blogspot.com/2011/11/papaa-on-tuesdayukiuandaa-moyo-na.html. Kuna watu Kati yetu Watakapokuwa wanakufa watakuwa wameacha alama kwenye maisha ya watu, Je ni alama gani utakuwa umeicha kwenye mioyo ya watu??Inawezekana umekuwa busy kufanya kwa ajili ya maisha yako binafsi, umekuwa ukitafuta fedha kwa ajili ya wewe na familia yako, umekuwa mtu wa kula bata usiku mpaka mchana, je unadhani hilo ndilo kusudi na Mungu kukupa uzima na fedha ulizonazo??Nini umewahi fanya kwenye Jamii kwa ajili ya watu na Mungu pia na kugusa mioyo ya watu na Mungu??Kama Uhai Ungekuwa unanunuliwa kwa Tigo Pesa ama Mpesa ama Airtel Money ungekuwa na Jeuri, Jiulize swali hili ni Kwanini Mungu akupe sababu ya Kuishi hadi wiki Ijayo???
Uwezo wa Kutengeza ama Kuharibu katika maisha tunao wakati tukiwa wazima na sio Wafu. Kusindikizwa na Umati Mkubwa wa Watu siku Ya Msiba na Misafara Mirefu Haitasababisha Mungu abadili uamuzi wa Kukupeleka Unakostahili Kwenda. Wanadamu Tumepewa Kuishi Mara Moja Kisha hukumu. Kuna chochote Cha Faida unakifanya ambacho kinaweza mshawishi Mungu Kuwa asikuchukue Leo??Kila Mtu atavuna alichoamua Kukipanda duniani.

Kuogopa Kufa hakutasaidia Usife.

Think Differently Make a Difference.

0713 494110
samuel_sasali@yahoo.com
Facebook. Samuel Sasali

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda