Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Thursday, November 15, 2012

Norwegian Church Aid Watembelea vijiji vya Gidarudagew, Endaharghadatk na Mazangiri kukagua miradi wanayoifadhili

Shirika la Misaada la Kanisa la Norway (Norwegian Church Aid-NCA) leo limetembelea vijiji vitatu katika wilaya za Mbulu na Mkalama katika mikoa ya Manyara na Singida ikiwa ni sehemu ya kukagua miradi mbalimbali wanayoifadhili katika wilaya zaidi ya 40 hapa nchini.
Mwakilishi wa NCA Ndugu Francis Uhadi akiongea na wananchi wa Kijiji cha Endagew
Timu ya NCA yenye jumla ya watu 4 inaongozwa na Mchungaji Blandina Faustine, iliwasili Haydom leo asubuhi ikitokea Karatu na Mbulu ambako pia walikuwa wakikagua miradi mbalimbali inayofadhiliwa na NCA, baada ya kuwasili walitembelea vijiji vya Gidarudagew na Endaharghadatk vilivyopo wilayani Mbulu na kisha kijiji cha Mazangiri kilicho katika wilaya mpya ya Mkalama (zamani Iramba) ambako walikagua shughuli mbalimbali zinazofanywa chini ya 4CCP.
Mchungaji Blandina akikagua Ofisi na Masijala ya Kijiji cha Endaharghadatk

Wakiwa katika kijiji cha Gidarudagew, timu ya NCA iliweza kukutana na wananchi wa kijiji hicho ambako 4CCP imekuwa ikitoa elimu za Haki ardhi, madhara ya pombe na Athari za mabadiliko ya tabia ya nchi. Pia kupitia 4CCP, shirika hilo limefadhili ujenzi wa ghala la kuvuna maji ya mvua kwa ajili ya shule ya msingi katika kijiji hicho chenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 3 ambapo wanakijiji wanachangia mawe, matofali, kokoto na mchanga. Aidha 4CCP ilihamasisha ujenzi wa masijala ya kijiji ili wananchi waweze kupatiwa hati miliki za ardhi za kimila, NCA walijionea masijala hiyo ambayo ipo katika hatua za mwisho kabisa na itaanza kutumika hivi karibuni

Baada ya kutoka Gidarudagew msafara huo ulielekea katika kijiji cha Endaharghadatk, ambapo 4CCP inafanya shughuli kama ilivyo katika kijiji cha Gidarudagew, timu ya NCA ilitembelea ujenzi wa masijala ya kijiji hicho na pia ujenzi wa ghala la kuvuna maji ya mvua linalojengwa katika hosteli ya wasichana katika shule ya Sekondari ya Mama Kari ambapo timu hiyo ilifurahishwa na juhudi zinazofanywa na 4CCP, viongozi wa kijiji na wanachi kwa ujumla katika kushiriki kuleta maendeleo jambo linalotia moyo hata wafadhili kuendelea kuelekeza misaada zaidi kwao
Shule ya Sekondari ya Mama Kari

Katika kijiji cha Mazangiri kilichopo wilaya mpya ya Mkalama, msafara huo ulipokelewa kwa ngoma kutoka makabila ya wanyisanzu na wasukuma tofauti na vijiji vingine. Aidha katika kijiji hicho pamoja na shughuli ambazo 4CCP imezifanya kama ilivyo kwa vijiji vilivyotembelewa awali, kijiji hicho ni moja ya vijiji venye VICOBA zenye mafanikio makubwa zilizoanzishwa chini ya 4CCP na timu ya NCA ilipata taarifa kuhusu vikundi vya VICOBA kijijini hapo.
Vifijo na nderemo walipowasili Mazangiri

Akisoma taarifa ya VICOBA, mratibu wa VICOBA kijijini hapo Bw. Salimu Athumani alisema kuwa wamefanikiwa kuunda vikundi viwili vya VICOBA toka mwezi Februari mwaka huu na tayari kikundi kimoja kimeuza hisa zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 1.2 na kingine shilingi laki 8.5 huku wanachama wa vikundi hivyo wakitoa shuhuda zao jinsi walivyofaidika na VICOBA ambapo wapo waliofanikiwa kununua bati kwa ajili ya ujenzi, kusomesha watoto, kununua ng'ombe, plau za kulimia na mitaji ya biashara.

Moja wa wanachama waliotoa ushuhuda wao mbele ya timu hiyo ya NCA alisema kuwa alikopa Sh 30,000/= ambazo alizizungusha na halimaye aliweza kununua Plau ya kulimia. Aliongeza kuwa anaomba elimu hiyo ni muhimu ikawafikia hata vijiji vya jirani ili nao wafaidike.
Blogger naye akaona isiwe tabu, naye akajichanganya kuserebuka

Naye kiongozi wa msafara huo Mchungaji Blandina Faustine alisema kuwa amefurahishwa kwa mapokezi na shughuli inayofanywa na 4CCP kijijini hapo, hasa jinsi ambavyo VICOBA vimeweza kuwakwamua kiuchumi na kuwasihi wananchi wengi zaidi wajionge na vikundi hivyo ili waweze kunufaika na faida zitokanazo na vikundi hivyo.
Katika hatua nyingine, Mchungaji Blandina alitoa nepi za watoto kwa kina mama waliokuja na watoto katika mkutano huo na kuwasihi kina baba kuwasaidia kina mama katika malezi ya watoto na kuwasihi kuepukana na unywaji pombe.
Mchungaji Blandina na Francis wakisisitiza jambo Gidarudagew

Katika ziara hiyo, Bw. Francis aliweza kuwauliza wananchi katika vijiji hivyo masuala mbalimbali waliyofundishwa katika programu za 4CCP hasa Haki ardhi na Udhibiti wa Mabadiliko ya tabia ya nchi ambako wananchi waliweza kujibu na hata kuuliza maswali kuhusu masuala mbali mbali. Maswali mengi yalikuwa katika kijiji cha Gidarudagew ambako wananchi hao walikuwa na maswali mengi na kuomba wapelekewe elimu hiyo tena ili waweze kupata majibu ya maswali yao hasa juu ya umilikaji mali katika familia ambako wengi walipinga suala la haki sawa katika kumiliki mali baina ya watoto wa kike na kiume hasa waliokwisha kuolewa.
Mchungaji Blandina na Francis kutoka NCA wakipokea zawadi kutoka kwa wananchi wa Mazangiri

Kwa ujumla timu ya NCA imefurahishwa na jinsi 4CCP inavyofanya shughuli na wananchi, shughuli ambazo matunda yake yanaonekana moja kwa moja katika jamii tofauti na miradi mengine na kuipongeza 4CCP kwa jinsi inavyofanya kazi.

Naye mratibu msaidizi wa 4CCP Bi. Eliminata Awet aliwaambia wananchi wa vijiji hivyo kuchangamkia fursa wanazopata za kwaletea maendeleo ili waweze kusimama wenyewe na kutoa mfano kuwa ukibebwa siyo una ubakunja miguu bali ubebeke
"Sisi waafrika tuna kasumba moja kuwa wafadhili wanapotusaidia tunajisahau na wanapoondoka tunakuwa kama awali, tukibebwa tukafikishwa usawa fulani jamani na sisi tuweze kusimama wenyewe na siyo tukiachiwa tunaanguka chini" alisema Eliminata
Timu ya NCA na 4CCP wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Gidarudagew
NCA itahitimisha ukaguzi wao kesho kwa kutembelea miradi ya 4CCP katika bonde la Yaeda Chini na kisha kutembelea kituo cha Utamaduni cha Haydom kabla ya kuendelea na ukaguzi huo katika wilaya za Hanang na Babati.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda