Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Monday, November 19, 2012

"......Muda wa Kutegemea Misaada kutoka Kwa Wahisani, Unafikia Ukingoni, Sasa Tufanye Kazi, NCA-Matere"


Wanachi wa Matere wakiwasikiliza kwa makini maofisa toka NCA
Na Nelsn Faustin.
Wakati Uganda ikipata dhoruba la kufungiwa misaada yote toka kwa nchi wahisani hasa Uingereza na Sweden kutokana na rushwa inayoitafuna nchi hiyo, Maofisa kutoka katika shirika la misaada la Norway-Norwegian Church Aid (NCA) Wakiwa katika siku yao ya mwisho wa ziara yao ya kutembelea shughuli mbalimbali zinazofadhiliwa na shirika hilo katika mkoa wa Manyara hasa zile zinazosimamiwa na Kituo cha pembe nne za utamaduni hapa Haydom(4ccp), wametoa wito kwa wanachi wote kujitahidi kufanya kazi kwa bidii bila kutetegemea wahisani kwani hadi sasa nchi wahisani zikiwemo Norway, Uingereza, Marekani, Sweden na nchi nyingine wahisani wanaozisaidia nchi za Afrika katika kuzikwamua katika umasikini mkubwa walionao.

Kwa kipindi kirefu sasa, dunia imekuwa ikilalamika juu ya msukosuko wa kiuchumi na hii pia imeathiri sana suala la misaada kwa nchi nyingi za kiafrika zinazoendelea ikiwemo Tanzania. Kutokana na hali hii, Mchungaji Blandina Faustine na Bw. Francis wakiongea na wananchi wa Kijiji cha Dominick katika kitongoji cha Matere baada ya kupata taarifa toka kwa kaimu mkuu wa shule ya Msingi Matere mara baada ya kukagua tank la maji la lita 10,000 mradi ambao umefadhiliwa na NCA kupitia Haydom 4ccp, maofisa hao wa NCA waliwaambia wanakijiji waliokusanyika katika hadhara hiyo kuwa, muda wa kuwasubiri wahisani ili kupata misaada kama ya fedha za miradi ya  maendeleo, chakula na misaada mingine unafikia ukingoni na ndiyo maana tangu mwaka 2005 hadi 2012 fedha nyingi zimekuwa zikitolewa kwaajili ya elimu ya kubadilisha mazingira tuliyonayo ili kujipatia maendeleo.

".....zile fedha walizokuwa wanatoa wafadhili wetu, hivi sasa wanazitoa kwaajili ya kuwapatia watu elimu ili kuwafanya watumie rasilimali walizonazo vizuri kwa manufaa ya sasa na ya baadaye ili waweze kujitegemea,,alisema Bw. Francis." Naye Mchungaji Blandina aliongeza kuwa vijana pamoja na wakina mama ambao wapo vijijini wanapaswa kuhakikisha kuwa wanajiunga kwenye VICOBA (mfumo wa benki vijijni) na vikundi vya utamaduni pamoja na kujishughulisha na ujasiriamali unaolandana na mazingira waliyonayo mbali na kutegemea misaada na kilimo ambacho kwa sasa kimeathiriwa sana na mabadiliko ya tabia nchi.

Katika kuhitimisha mkutano huo mfupi, mratibu msaidizi wa 4ccp aliahidi kuwa kutakuwa na mafunzo ya haki ardhi, VICOBA na mabadiliko ya tabia nchi. Lakini pia alisisitiza kuwa jamii haina budi kutunza miradi ambayo wanapewa ili idumu na kukidhi mahitaji ya sasa na ya baadaye. Safari ya ziara yao iliishia Sekondari ya Yaeda Chini ambapo wanafunzi walisisitizwa kusoma kwa bidii na kutumia fursa yao ya kuwa wanafunzi kwa kujiunga katika vikundi mbalimbali vijijini ili kuwasaidia vijana wenzao ambao hawakufanikiwa kupata fursa hiyo. 

NCA walimaliza ziara yao na kusifu sana juhudi za 4ccp katika kubadilisha maisha ya wananchi wa Haydom na vitongoji vyake.

Mungu ibariki NCA, Mungu ibariki, Haydom-4ccp, Mungu ibariki Tanzania.

"Nipo kwa sababu Upo"  
Kutoka Kulia ni Mchungaji Blandina Faustine akiteta jambo na Bw. Francis, aliyesimama ni Bw. Murge ambaye ni mwakilishi wa Wahadzabe-4ccP

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda