Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Friday, November 30, 2012

Mfanyabiashara sugu wa dawa za kulevya akamatwa Simanjiro

Na Mwandishi wetu
Simanjiro

JESHI la polisi Mkoani Manyara linamshikilia mkazi mmoja wa Mkoani Arusha anayedaiwa kuwa ni mfanyabiashara wa kimataifa wa dawa za kulevya baada ya kukamatwa akiwa na kete 30 za dawa za kulevya aina ya Heroine.
 
Mfanyabiashara huyo alikamatwa jana, kwenye machimbo ya Tanzanite kitalu D Mirerani, Simanjiro, msako wa kawaida wa polisi wakiongozwa na Kaimu mkuu wa kituo cha Mirerani,Mkaguzi wa polisi Naftali Mnzava.
 
Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara,Kamishna msaidizi,Akili Mpwapwa alimtaja mfanyabiashara huyo kuwa ni Bw.Albert Gift (29) mkazi wa jijini Arusha.
 
Kamanda Mpwapwa alisema mfanyabiashara huyo anadaiwa kufanya biashara za dawa za kulevya, kwenye miji mbalimbali ya nje ya nchi ikiwemo Mombasa na Nairobi nchini Kenya, Kampala nchini Uganda na Lusaka nchini Zambia. 
 
Aidha alisema mfanyabiashara huyo alikamatwa akiwa na paspoti akifanya biashara hiyo ya kuuza dawa za kulevya aina ya heroine kwenye eneo hilo la machimbo ya madini ya Tanzanite mji mdogo wa Mirerani,Wilayani Simanjiro
 
“Polisi wa kituo cha Mirerani walikuwa kwenye doria ya kawaida katika migodi ya madini ya Tanzanite ndipo wakafanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo na bado tunamshikilia tukiendelea kumuhoji” alisema Kamanda Mpwapwa.
 
Alisema kuwa jeshi lake linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo kabla ya kumfikisha Mahakamani wakati wowote mtuhumiwa huyo mara baada ya uchunguzi wake utakapokua umekamilika.
 
Hata hiyo Kamanda Mpwapwa alitoa wito kwa wakazi wa mkoa huo kupitia dhana ya ulinzi shirikishi na polisi jamii kushirikiana na jeshi la polisi katika kuimarisha ulinzi na usalama kwenye maeneo yao.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda