Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Friday, November 2, 2012

Matokeo ya Kura ya Maoni: Miaka 10 ya mkoa wa Manyara haujakidhi Mahitaji ya wananchi

Wiki iliyopita tulitaka kupata maoni ya wasomaji wa Ohayoda hasa wanaotoka katika mkoa wa Manyara kuwa, wakati mkoa wa Manyara ukiadhimisha miaka 10 toka uanzishwe mwaka 2002, Je kuanzishwa kwa mkoa huu kumekidhi mahitaji ya wananchi kiuchumi, kiutamaduni na kijiografia?

Asilimia 100 yaani wasomaji wote waliopiga kura kupitia Ohayoda walisema kuwa haujakidhi malengo/mahitaji ya wananchi huku waliotoa maoni yao kupitia group mbalimbali za mtandao wa kijamii wa Facebook kama Babati Forum, Mbulu Youth Group, Karatu Youth Group, Nyumbani Mbulu, Fikra Pevu na Tanzania Political Forum walitoa maoni tofauti wengi wakidai ugawanyaji ulifanyika kisiasa zaidi pasipo kuangali jiografia ya mkoa kwani makao makuu ya mkoa ni mbali kutoka wilaya nyingi hasa za Simanjiro na Kiteto. 

Na kuna waliodai kuwa kumewatenga wananchi wa Karatu kiutamaduni sawa na wale wa Simanjiro na Kiteto kwani Karatu ingepaswa kuwa Manyara na Simanjiro na Kiteto kubaki Arusha huku suala la wilaya ya Ngorongoro likiwa bado kitendawili

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda