Kweli

NANYI MTAIJUA KWELI.....NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU....NANYI MTAKUWA HURU KWELI KWELI

Mbiu ya Jamii

Tangaza Biashara yako hapa...wasiliana nasi sasa kwa 0753038005

WELCOME TO HAYDOM CULTURAL FESTIVALS 2013

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA

NORWEGIAN CHURCH AID TANZANIA
PROUD PARTNERS OF HAYDOM FOUR CORNERS CULTURAL PROGRAMME (4CCP)

Thursday, November 22, 2012

MAGHEMBE Aunguruma Babati: "Wahandisi wa Maji Msiowajibika Kaeni kando"

Na Mary Margwe,Babati

 
 Wahandisi wa maji kote nchini wametakiwa kuwajibika kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji ambapo imebainishwa kuwa waandisi wasiowajibika wawapishe wanaowajibika, kwani wamekua wakichangia kwa kiasi kikubwa ucheleweshwaji wa maji kwa wananchi wasio na hatia.
 
Hayo yalibainishwa jana na Waziri wa maji Profesa Jumanne Maghembe, alipokua akizindua mradi wa maji katika kijiji cha Endagile kata ya mamire Wilayani Babati, Mkoani MANYARA, ikiwa ni moja wa miradi ya vijiji 10 kwa kila halmashauri  inayotekelezwa chini ya programu ya maji na usafi wa mazingira Vijijini.
 
Profesa Maghembe alisema  zipo baadhi ya Halmashauri zenye wahandisi wazembe ambazo zimekua zikichangia kwa kiasi kikubwa kuchelewesha kukamilika kwa miradi ya maji kwa wakati hali inayopelekea wananchi kuitupia lawama Serikali.
 
“Jamani hili suala liko wazi kabisa ninaomba wahandishi wasiowajibika watupishe kabisa, kwani watazisasabishia hata Halmashauri kukosa fedha za maji kwa kipindi kingine, kila mmoja ahakikishe anawajibika katika sekta yake kikamilifu kinyume na hapo watupishe kabisa”alisema Maghembe.
 
Kufuatia hayo alizitaka halmashauri zote nchini kuhakikisha wanafuatilia kwa ukaribu utendaji wa sekta binafsi ili kuona kama kuna uzembe katika utekelezaji ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua hata ikibidi mikataba yao isitishwe na kuwaondoa kwenye daftari la wataalm wanaoruhusiwa kufanya kazi hapa nchini.
 
“Kwa makandarasi wote wa ujenzi wa miundombinu ya maji, watekeleze majukumu yao kwa kuzingatia michoro, viwango na ubora unaostahili, kwani wizara ikishirikiana na ofisi ya waziri mkuu –TAMISEMI, itaendelea kufuatilia kwa ukaribu ili kuhakikisha kuwa halmashauri zinatekeleza agizo hilo” alisema Maghembe.
 
 Maghembe aliendelea kusema kuwa kupitia mradi huo wa Endagile amehimiza miradi ya vijiji 10 kwa kila halmashauri nchini kuhakikisha inakamilisha mapema utekelezaji wa miradi yake ili wananchi wapate huduma ya maji kwa wakati muafaka.
 
Aidha alifafanua kuwa kumekuwepo na ulegevu wa Sekretarieti  za Mkoa na Halmashauri kutofuatilia na kutosimamia kazi zinazotekelezwa na sekta binafsi, ambapo “ninaziasa sekretarieti  za mkoa na halmashauri kuwa kazi zinazotolewa na sekta binafsi zisimamiwe ipasavyo ili kukidhi viwango” alisema Maghembe.
 
Alisema ni vema kwa halmashauri na sekretarieti za mkoa kuhakikisha kuwa huduma zinazotolewa na sekta binafsi zinakidhi viwango vinavyohitajika na kwa zile ambazo zinafanya kazi kwa udanganyifu Serikali haitavumilia kuona fedha zinatumika vibaya kwa kulipa wataalam wa sekta binafsi ambao hawatekelezi majukumu yao ipasavyo.
 
 
“Iwapo itabainika kuwa halmashauri inachangia kuchelewesha wananchi wananchi kupata huduma ya maji kutokana na uzembe wa wataalam zitachukuliwa hatua kali na pia hata kunyimwa fedha kwa kipindi kingine”alisema Maghembe.
 
Aidha alisema alizitaka  Halmashauri na Sekretarieti za Mikoa kote nchini  kuhakikisha kuwa zinaajiri wataalam zaidi, katika sekta ya maji ili kuimarisha utekelezaji, usimamizi  na uendeshaji wa miradi ya maji Vijijini.
 
Naye Mhandisi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Vijijini Bw.Emmanuel Konkomo, alisema mradi huo ambao umezinduliwa utasaidia kuhudumia vijiji viwili vya endagile na mamire, ambapo uzalishaji wa maji katika mradi huo ni lita 190,080 kwa siku  na kutosheleza mahitaji kwa asilimia 240%.
 
Konkomo alisema mradi huo umegharimu jumla y ash. Mil 471,074,300, ambapo jamii ilifanikiwa kuchangia jumla y ash.mil.9,,mfuko wa maendeleo (LGCDG) sh.mil.66, huku programu ya maji ikitumia sh.mil.396,074,300.
 
Akizungumzia hali halisi ya wananchi wa kijiji cha endagile kabla ya kupata maji mjumbe wa kamati ya watumia maji milima kwaraa Bw.Peter Sabas alisema awali mahudhurio ya wanafunzi katika shule za msingi yalikua mabaya sana kwa sababu walikua wakitumia muda mwingi kwa ajili ya kutembea umbali mrefu kutafuta maji kwa matumizi ya nyumbani, badala ya kutumia muda huo kukaa darasani na kujifunza.
 
Hata hivyo alifafanua kuwa idadi kubwa ya kijiji hiko walikua wakisumbuliwa na magonjwa ya milipuko kama vile kuhara, kipindu pindu,amoeba  na minyoo,ambapo kwa sasa hali ni shwari.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Ohayoda